Oroka msoro
JF-Expert Member
- Dec 24, 2022
- 573
- 434
Hawa watu wanajikuta wajuaji ilhali hakuna wanachokijuaSasa hivi sehemu za Marekani na Japan zina baridi ambayo haijawahi kuonekana. Mwaka huu Uingereza ilikumbwa na joto ambalo lilisababisha mataruma kupinda.
Tunaposema kuwa tabia nchi itabadilika tunamaanisha kuwa kutakuwa na ukame ambao hatutarajii, mara moja moja zitanyesha mvua kubwa kuliko tulivyozea, tutakuwa na vimbunga kuliko kawaida. Athari nyingine ni kuwa kutokana na kukatwa miti maji yanayoingia mtoni yanakuwa na matope mengi hivyo kupelekea mabwawa kujaa mapema. Mtera na Kiwira zinakosa maji kutokana na matope kujaa. Nyie endeleeni kubisha maana majuto ni mjukuu.
Amandla.....