Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Zamani wa Monduli (CCM) Hayati Edward Lowassa anazikwa leo Nyumbani kwake, Monduli. Mazishi haya yamehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Waombolezaji wametoa Salamu za Mwisho kwenye Jeneza la Hayati Lowassa, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kisha famili ya Lowassa, viongozi wengine wa kitaifa pamoja na Viongozi waandamizi kutoka vyama vya upinzani, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe.

Mazishi haya yataendeshwa kwa Sehemu mbili, Kidini na Kiserikali. Kwa upande wa Dini, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa ataongoza ibada hiyo, kisha Jeshi la Wananchi la Tanzania litashiriki sehemu ya pili ya Mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi, Hayati Lowassa atapigiwa mizinga 17 kwa heshima yake.

Saa 6:25 Mchana, Maafisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali wanauingiza Mwili wa Hayati Lowassa Kaburini. Zoezi hili linafuatiwa na kuweka mchanga kaburini kama sehemu ya kuaga.

Saa 6:55 Mchana, maafisa wa JWTZ wameanza shughuli za kufunika kaburi. Mizinga 17 imepigwa.

Kinachofuata sasa ni hotuba ya viongozi mbalimbali. Pamoja na wengine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Samia Suluhu Hassan amezungumza, lakini pia Freeman Mbowe, mwenyekiti wa CHADEMA taifa amezungumza.

Hayati Edward Lowassa alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam, Februari 10, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

IMG_9966.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

IMG_9967.jpeg

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mazishi ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024

IMG_9968.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

Buriani Edward Ngoyai Lowassa!
 
CCM ni kundi kubwa sana la watu wasio na haya.

Jinsi walivyokuwa wanamtusi, wanamnyanyasa Lowassa na familia yake, walivyomuita "maiti", wakamtweza kwa Kila Hali, leo wanajifanya kububujikwa na machozi.

CCM walimdhadhalilisha sana Lowassa kiasi kwamba Leo tunapowaona wameongozana kwenda kwenye mazishi yake, tunajiuliza, KULIKONI???
 
Back
Top Bottom