Mliobobea na Kutukuka katika ‘Critical Thinking ‘ kwa Kauli hii ya Spika Job Ndugai mmegundua nini Kinachokuja?

Nafikiri bwana mkubwa mjengoni pale anatatizo fulani, na kama atakosa ushauri mzuri basi tutegemee kuyaona mengi sana katika kipindi chake kichache kilichobaki kuliko tuliyoyaona muda uliopita.
Ukimcheki toka ule uchaguzi wa ndani wa ccm, alionekana kuwa mkali mpaka akamzimisha kwa muda mwenzake kwa kumtandika bakora, lakini cha kushanganza baada ya kuingia mjengoni akaendelea kujisifia kuwa kwao ugogoni kutumia bakora ni sahihi na aliendelea kujisifu badala ya kuomba msamaa kwa kosa alilomfanyia mwenzake.
Vitisho viliendelea tena, kwa Zitto, kwamba angeweza hata kumfungia asitinge mjengoni hata kwa kipindi chote cha miaka mitano. Mifano mingine ni hili la akina Mdee na Lema.
Kwa hali ya kawaida, sidhani kama hili linaanzia hapohapo Mjengoni, kuna uwezekano mkubwa sana lina relate na family matters, yaani kama haupo na furaha kutoka nyumbani kuanzia watoto wako, mweza wako na wanaokuzunguka basi ni vigumu sana muda mwingine kuweza kumudu kazi za kiofisi. Sisi wa maofisini tunayaona haya kila siku.
Kuhusu hili la Prof, litamsumbua sana ndugu huyu kwa sababu ya msimamo wa Prof na ndiyo maana anafanya juu chini hata kumchonganisha na ndugu Rais ili jamaa aachie ngazi na iwe furaha yake na pengine atasimama pale Mjengoni na kusema kazi amemaliza na kujisikia wa furaha zaidi. Lakini what will be next kama hasipojiuzuru? Je kejeri juu ya Prof zitaendelea ama atatafuta angle nyingine na hata ya kukwamisha shughuli za Serikali kiasi kwamba Prof atoke tu.
Ingalikuwa ndani ya mjengo kungalikuwapo na idadi ndogo sana ya wale wa ndiyo basi ningalishauri wamuondoe ndugu huyu kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nane.
Huyu jamaa amesahau mkuu alichofanya wizara ya afya? Hatamtengua CAG ili aone mwisho wake
 
Kwamba kuna mtu anataka kufanya yake madudu ya kupiga mshiko lakini CAG ni kikwazo kikubwa
 
Shetani mkuu na mdogo wake wamekaliya misumari, walidhani CAG ni mtu wa ajabuajabu kama wao. Kinacho waudhi hawa washamba ni CAG kuibua hadharani wizi mkubwa wa mali ya watz. Hii tuhuma inawapa shida sana ukizingatia wanavyo penda sifa sana za kijinga. Watz tuko pamoja na CAG. Shetani na mdogo wake sasa ni muda wao na wao wanaisoma namba
 
Kauli ya Spika inatoa tafsiri kwamba Raisi anachukizwa kuona matumizi mabaya ya fedha zetu, yakiwekwa hadharani!

Hii inamaanisha Rais anasimama upande wa wanyongaji na sio upande wa wanyonge kama ambavyo tumekuwa tukiaminishwa.

Kusema kweli inaumiza na kuleta maswali mfulululizo kichwani kuhusu hawa viongozi wetu!
Ndio maana wanasemaga uwongo hauna maisha marefu mkuu!!!
TUNAPIGWA KWELI KWELI SIO TULIPIGWA KWELI KWELI!!
 
Mku kwa uelewa wangu ninachokijua Assad hana kosa ndio report imepokelewa na wahusika.
Kama hawataifabyia kazi hiyo ripoti ndo tutajua ni nani mwenye mamlaka kati ya Spika na Rais kwani Assad ameshamaliza kazi yake.

Spika kumwambia ajiuzulu wakati ajua ripoti ipo mezani kwake ni kuwatuchanganya sisi Wananchi
Hakuna Kauli ya Mheshimiwa Spika Job Ndugai ‘ iliyonitisha ‘ kama hii aliyoitoa ambayo nainukuu hapa isemayo…” CAG Assad anampa wakati mgumu sana Mheshimiwa Rais ajiuzuru tu mwenyewe “.

Baada ya kujua kuwa Rais siyo tu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli bali ni Taasisi ambayo ina Watu wengi au Vyombo husika hapo ndani yake nilipoirudia hii Kauli ya…” CAG Assad anampa wakati mgumu sana Mheshimiwa Rais ajiuzuru tu mwenyewe “ Mimi kama GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE nimeanza ‘ Kuogopa ‘ na sasa nina mambo ya ‘ Kutisha ‘ ambayo yamejaa Ubongoni mwangu.

Naomba wale ‘ Wabobezi ‘ wa Tafakuri Tunduizi ( Critical Thinking ) au wenye uwezo wa Kuwaza ( Kufikiri ) mbali zaidi na kwa Uchambuzi wake wote waje wanisaidie kuwa kwa Kauli hii ya Spika Ndugai kuna nini kinachoenda Kujiri au mpango gani unaandaliwa kwa CAG Assad na mengineyo?

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Kauli ya Mheshimiwa Spika Job Ndugai ‘ iliyonitisha ‘ kama hii aliyoitoa ambayo nainukuu hapa isemayo…” CAG Assad anampa wakati mgumu sana Mheshimiwa Rais ajiuzuru tu mwenyewe “.

Baada ya kujua kuwa Rais siyo tu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli bali ni Taasisi ambayo ina Watu wengi au Vyombo husika hapo ndani yake nilipoirudia hii Kauli ya…” CAG Assad anampa wakati mgumu sana Mheshimiwa Rais ajiuzuru tu mwenyewe “ Mimi kama GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE nimeanza ‘ Kuogopa ‘ na sasa nina mambo ya ‘ Kutisha ‘ ambayo yamejaa Ubongoni mwangu.

Naomba wale ‘ Wabobezi ‘ wa Tafakuri Tunduizi ( Critical Thinking ) au wenye uwezo wa Kuwaza ( Kufikiri ) mbali zaidi na kwa Uchambuzi wake wote waje wanisaidie kuwa kwa Kauli hii ya Spika Ndugai kuna nini kinachoenda Kujiri au mpango gani unaandaliwa kwa CAG Assad na mengineyo?

Nawasilisha.
Ni kweli wezi wamekaa kikao dhidi ya mlinzi wa kodi zetu(CAG). Na wametafuta mtu baradhuli wa kupiga kilele ili wenye akili ama busara kidogo tu wapime upepo unaenda je. Raia kwa wengi wao washaona CAG ndio mzalendo namba moja wa taifa hili na kwamba hana maneno ya kisiasa ya kuzuga ila anatembea katika njia nyembamba ya ukweli.
Sasa kazi imebaki kwa yule mkuu wa kaya anajipambanua kisiasa kuwa ndie mzalendo namba moja atakaa upande gani. Ama akae na genge linalojiita taasisisi ya uraisi linalomtuma spika kulinda ufisadi wao usiwekwe wazi au abaki na umma mkubwa uliojipambanua kukaa na CAG popote alipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watueleze mbona siku hadi siku serikali I narudi nyuma kwenye compliance ya matumizi ya fedha? Wao wanashikilia issue ya dhaifu kuwa ndio itutoe kwa mstari. Waje na majibu isue ya kumwacha au kutoa CAG ni yao wao. Mbona wanatumbua tu kila siku safari hii wamekutana nampemba na sio Mchagga au msukuma wanakoma. Hawa hata kujilipua wanaweza
 
MSIGWA, tafadhal hebu tujuze kuhusu ili swala eti haujasikia fununu hapo ndani kwamba Baba mwenye hiyo nyumba nyeupe halali kutwa nzima anasonya kisa CAG?
Maana huku ndugai dhaifu anatuaminisha kuwa CAG anampa wakati mgumu jiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kauli ndo inazidi kulionyesha kwamba bunge si tu ni dhaifu bali ni bunge bovu.
Kauli hii inamaanisha kwamba kabla ya kuja press conference alienda kwa Magu akampa maelekezo ni nini cha kuongea, yaani mkuu wa muhimili mmoja anaenda ku-seek instructions kutoka mkuu wa muhimili mwingine? Kama si kuwekwa kwapani ni nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna sehemu walioandika katiba yetu walitenda haki kwa uadilifu mkubwa ni kwenye kipengele cha CAG. Waliona mbali sana. CAG is a very strong person as per kipengele hicho cha katiba. Kwa wapenda haki wote duniani, kazi anayoifanya CAG Assad ni ya kutukuzwa sana na ni mtu anayestahili kuombewa mno ili aendelee kurithisha uzalendo huu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo katika nchi yetu. Mungu ambariki sana
 
Neno Bunge dhaifu alilenga serikali,akitaka bunge liiwajibishe serikali.
Akisema atarudia neno bunge dhaifu ni kuwaamusha wabunge kufanya kazi ya kuiwajibisha serikali kwa mahesabu mabovu yenye walakini nyingi.
Kama mlengwa ni serikali basi Magu atakuwa na wakati mgumu.Shortcut ni huyo mhasibu mkuu kuachia ngazi.Awapishe wafanye yao.
 
Back
Top Bottom