Mlinzi wa Lowassa, Aloyce Tendewa atimuliwa kazi...

Bw Tendewa a tendewe haki...kavujisha siri ya kuhamishwa kwake...!!! Hivi sie kwa macho yetu tusingejua mlinzi wa Mamvi siku hizi hayupo? Ingeendelea kuwa siri kwa muda gani? Mie EL simkubali kabisa, ila naomba TISS wafikirie tena sio mbaya ku review fikra....! Kwa tunavyowajua isijekuwa hata hiyo inaotwa siri wameivujisha hao hao kumzunguka! Msiendekeze sana undava! !
 
Mwana usalama yoyote atusaidie kwa ufafanuzi kuhusu sheria na taratibu za TISS.
Webgine humu mnakisiaa tu.
 
Huyu lowasa sijui atatoka lini vichwani mbona rungwe na wengine hawatamkwi, imekuwa lowasa kila mara, yaani lowasa anavyotajwa ni kuliko jina la Mungu, yashapita hayo tufanye kazi kuinua nchi yetu, mnabwabwaja mwishowe mtajiona wapumbavu tu, yeye kiiiimya
 
QUOTE="Ndakilawe, post: 15006847, member: 47759"]Kwa Lowassa kuna maziwa...![/QUOTE]na asali
 
ALIYEKUWA mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, amefukuzwa kazi.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi kutoka vyanzo vyake vya uhakika vilivyo serikalini, zimedai kuwa Tendewa amefukuzwa kazi na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa na vyanzo vya uhakika vya gazeti hili, ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.

Inadaiwa kuwa Tendewa baada ya kuvuliwa jukumu la kumlinda Lowassa alibaki na kinyongo moyoni kwa sababu hakuridhika na hatua hiyo hivyo alivujisha taarifa hizo kwa vyombo vya habari jambo lililoelezwa kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya gazeti hili, Tendewa alipewa barua ya kuachishwa kazi juzi jioni baada ya kuvuja kwa uhamisho wake kwenye vyombo vya habari.

“Alikuwa bado anataka kuendelea kumlinda mzee (Lowassa), lakini kuna vitu alishindwa kuvitekeleza kwa ufasaha kwa hiyo kitendo cha kuondolewa kilimuudhi akaamua kupeleka taarifa gazetini jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao za kazi za kiusalama,” alidokeza mmoja wa maofisa aliyezungumza na gazeti hili.

Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kwamba, pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa Lowassa.

Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.

Mmoja wa watoa habari wa gazeti hili aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.

Hata hivyo, alisema bado kuna utata kuhusu mtu aliyesaini barua ya kufukuzwa kazi kwa Tendewa ambaye kwa wadhifa wake ilipaswa kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu lakini badala yake imesainiwa na ofisa wa cheo cha chini.

Jitihada za kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Taifa, Othmani Rashid, hazikuweza kuzaa matunda hadi tunakwenda mitamboni na hata Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Viongozi, Ben Mashiba naye hakuweza kupatikana.

Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa.

Rekodi zilizoonwa na gazeti hili za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.

Aidha, rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.

Historia hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.

Baada ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza.

Chanzo: Mtanzania
Habari ina ukakasi unao karibia na uongo katika habari nzima.
Kwanza hakuna TIS kuna TISS, tofauti hiyo ni muhimu kwa mtoa habari abayeitunga habari yenyewe.
Halafu TISS haifanyi mambo yake public.
Yaani mtu anafukuzwa kazi, anaenda public kulalamika, sijawahi kusikia kitu hicho, hiyo si Idara ya Maji.

Mtoa habari anasema ati wamejaribu kumcontact Tashid Othman!!
Du, hiyo ni first.
Yaani mtoa habari anawasiliana na Shushushu Namba Moja nchini?
Tena, sijawahi kusikia.

Tatu, mtoa habari anasema ameona rekodi ya utumishi ya huyu jamaa Tendewa, unless yeye mwenyewe yuko TISS, hii inawezekana, na kama nilivyosema hii Idara si Idara ya maji.
Personal files za watumishi wote ni classified na they are not for public consumption.

Hii habari kwa ujumla ni riwaya, invyoelekea.
 
Siamini Kama kafukuzwa ..maana mtu elite Kama Yule huwezi kumfukuza hadi kwa idhini ya Amiri jeshi mkuu
Siamini gazeti la mtanzania wanaweza kuandika uongo wa kiasi hicho, unless kutokana na hii thread amri jeshi amuonee huruma kama ni kweli, ila kama TISS ni indipendent organ basi hata mimi namhurumia mzee Tendewa
 
Siamini gazeti la mtanzania wanaweza kuandika uongo wa kiasi hicho, unless kutokana na hii thread amri jeshi amuonee huruma kama ni kweli, ila kama TISS ni indipendent organ basi hata mimi namhurumia mzee Tendewa

Ninachotambua ni kwamba serikali ime terminate mkataba wake na sio kweli kwamba amefukuzwa kazi ndio maana nikasema sikubaliani na gazeti straight aulize chanzo chake vizuri
 
Kkama ni kweli kafukuzwa hawezi pata shida maana alikuwa mjasiriamali toka akiwa butiama nakumbuka alikuwa na bar nzuri sana ilikuwa inaitwa mpapai na ndio bar za mwanzo za kisasa
 
Ninachotambua ni kwamba serikali ime terminate mkataba wake na sio kweli kwamba amefukuzwa kazi ndio maana nikasema sikubaliani na gazeti straight aulize chanzo chake vizuri
Hivi ku terminate mkataba inatofauti gani na kusimamisha kazi?
 
Hivi ku terminate mkataba inatofauti gani na kusimamisha kazi?

Huyo mtu alishalipwa stahiki zake,isipokuwa aliomba afanye kwa mkataba,alikubaliwa ila kwa sasa sio yeye tu wako watumishi wengi wa umma mikataba yao imesitishwa na wala isiwe hoja ya kumtetea sana Tendewa kwa sababu tu alikuwa mlinzi wa fulani au kwakuwa gazeti limeandika. He,wale ambao wamesitishiwa mikataba na hawaandikwa gazetini watahisi nini? Mzee Kova naye mkataba wake ulikuwa bado miezi sita,mbona amesitishiwa? Lazima tukubali kuwa kama serikali ilisema hakutakuwa na ajira za mkataba serikalini basi waondoke na kuwaachia wengine ambao ni bora kama wao au zaidi yao kufanya hizo kazi
 
Gazeti la Mtanzania naona kama linaungaunga maneno kwani alijaweza ku balance story, alijaweza kumhoji huyo mlinzi mwenyewe na kupata maelezo yake kama kweli kafukuzwa ama laa, pia alijaweza kumhoji mkuu yeyote rasmi kutoka katika hiyo idara ya Usalama wa Taifa istoshe pia aijaweza kueleza kuwa hiyo habari imeandikwa na nani.
Hayo machache yananifanya niamini hiyo habari sio ya kweli na ninaweza kufikiri inachochea watu wadhani wote waliokuwa karibu na Lowasa wanaanza kushughulikiwa. Napendekeza hiyo habari ipuuzwe kwa kiwango cha kutosha kupuuzwa.
 
ukitoka huko mkoani Iringa ukirudi kituoni kwako Temeke pale kwa yule Bosi wako wa Kike Mhaya msalimie sana mkuu. ni matumaini yangu kuwa siku hizi umeshakua na umepunguza " ulevi " wako ule au? kwanini lakini Bosi wako aliamua kukutuma huko kwa Wanyalu? au ulikiuka ile miiko yenu ya kazi zenu? nasikia kuwa kama ukiwa Dar halafu ukatupwa bush mikoani ni sawa sawa na umekuwa " demoted " je kuna ukweli gani katika hili mkuu? unasalimiwa na mkeo Bunju / Mbweni na washua zako Tegeta mkabala na shule ya kishua ya FEZA.
Ha ha ha ha,nyie watu wawili nasoma conversation yenu
 
Back
Top Bottom