Mlimani city waanza kubagua watanzania?

Hata kwenye mabaa yetu ya mtaani wanawazuia machinga sembuse vibatavuzi kuzuiwa

Kwenye jiji la Arusha kwa wale ambao wameshafika sehemu inaitwa Maasai Camp watakuwa wanajua kwamba hamna mtu anayeruhusiwa kuingia pale kwa miguu maana yake lazima uwe na gari ili uweze kuingia na sababu maalun=mu ni kwamba ili kuzuia vibaka na flycatchers ambao still ndio wanaojaza hiyo sehemu ya starehe na vibaka tele!
 
Wawinda wazungu Arusha wako kila mahali!! Sio flycatchers tu! Via via thursdays...... vijana wa siku hizi na white species!!!!
 
Mtoa pesa ni kutoka botswana ila ametumia makaburu kuendeleza eneo hilo katika upangishaji na kadhalika , kiko eneo la udsm ila mkataba ni wa miaka 50 ndio itakuwa rasmi mali ya udsm

upo hapo
 
Kwenye jiji la Arusha kwa wale ambao wameshafika sehemu inaitwa Maasai Camp watakuwa wanajua kwamba hamna mtu anayeruhusiwa kuingia pale kwa miguu maana yake lazima uwe na gari ili uweze kuingia na sababu maalun=mu ni kwamba ili kuzuia vibaka na flycatchers ambao still ndio wanaojaza hiyo sehemu ya starehe na vibaka tele!

Nao huu ni ubaguzi tu
 
Mtoa pesa ni kutoka botswana ila ametumia makaburu kuendeleza eneo hilo katika upangishaji na kadhalika , kiko eneo la udsm ila mkataba ni wa miaka 50 ndio itakuwa rasmi mali ya udsm

upo hapo

Unamaana kwa kipindi chote hiki hawa jamaa wanakamua tu mihela na UDSM hawalipwi pango au ardhi wanayo tumia kuchumia kwa miaka hiyo 50?
Duh si mchezo waTZ ndo tulivyo baada ya miaka hiyo 50 si majengo yatakuwa yamesha choka jamaa watakuwa wamepata faida mara dufu...
 
Kama mambo ni hivyo sishangai kwa sababu kuna wakati yaliibuka malumbano baina ya uongozi wa UDSM na wanafunzi waliokuwa wakihoji umuhimu wa mradi huu. Wanafunzi walikuwa wakidai kuwa mradi hauna uhusiano wa moja kwa moja na core function za chuo na hauna faida ya moja kwa moja katika shughuli za chuo hicho.
Inawezekana kuwa ten percent ndiyo imeshawishi watu kusaini contract ya mradi huu
 
Mama Lao, Nadhani unachokiongea hapa kina mantiki.

Lakini kwa maoni yangu..umeendeleza ule ule mtindo wetu watanzania kuona kitu na kulalamika baadaye. wewe ulivyoona dereva wa Bajaji anaambiwa arudie getini, ulichukua hatua gani? kwa vigezo vyangu..mi sikujui lakini kama una uwezo wa kubonyeza keyboard..basi wewe ni middle class au zaidi kwa hiyo hata uelewa wako ni mpana.

Yes, from your story, alichofanyiwa mwenye Bajaji si sawa, lakini hata wewe ulichofanya si sawa. Kwenda kuongea na dereva wa Bajaji kweli ulitegemea nini? Kwanini hukwenda kuwaona wausika moja kwa moja?

Kwa maoni yangu: Ungeenda moja kwa moja ukaomba kumuona meneja wa Mlimani city na kumuuliza kama kuna sheria/utaratibu huo ambao umewekwa na wao. Au ni walinzi waliamua kuweka utaratibu wao. Iam sure huyo meneja angekupa jibu sahihi na wewe baada ya hapo ndo ungefanya conclusion kuwa either kuna ubaguzi au vipi.

So next time ukiona tatizo kama hilo..siyo kuja JF na kumwaga "the dataz za ubaguzi wa makaburu". Do something siyo kulalamika tuu. Huwezi jua hata huyo meneja wa Mlimani City anaweza kuwa hajui walinzi kama wanawanyanyasa watu wa bajaji... Kwa kufanya hivyo, ungekuwa umewasaidia madereva na perhaps yule boss angeona kwamba kuna watu waelewa kwenye nchi yetu ambao wanafuatilia mambo. Na indirectly, ungekuwa umesaidia wengi dhidi ya manyanyaso ya walinzi..

Jamani changes ni initiave zetu wenyewe...Tusipende kulaumu tuu kwa yale ambayo we can influence changes.

Mada yako hapo juu, inaweza kuwa na ukweli, lakini ukiangalia..ni ule ule mwendelezo wa watanzania wa "kupenda kulaumu"

NEXT TIME, DO SOMETHING!

Masanja,

Usimlaumu sana huyo si mwandishi habari ndio maana hakuona umuhimu wa kubalance kwa uongozi wa mlimani city. Hata hivyo kwa kufuata tu kanuni ya "No body should be condemned unhead" nafikiri ni vema uongozi wa mlimani city ungeulizwa ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo,kwani accusation za ubaguzi ni mbaya.
 
Mama lao, wewe na wengine mmeona huu ni u baguzi wa mtu wa hali ya chini labda kulingana na hali zenu za kiuchumi. Kwa Tanzania mtu anayemiliki Bajaj au anayeweza kuikodisha siyo mtu wa hali ya chini.
Mlimani city kuna watu wengi tu wanaingia bila usafiri wowote ule na ukiangalia vizuri kwenye parking lot yao kuna sehemu zimetengwa maalum kwa kupark pikipiki na baiskeli.Je pikipiki na baiskeli ni za thamani zaidi ya Bajaj?
Haikuwa sahihi kukimbilia kwenye judgement kuwa mwenye Bajaj amebaguliwa kwa sababu ni "maskini", halafu pia kichwa cha habari chako kimeeleza kuwa wanaobaguliwa ni watanzania.Je kuna foreigner ameruhusiwa kuingia na kibajaj?
Pia mama lao hukuitendea haki Mlimani city kuiweka hadharani kuwa inabagua watanzania just kwa kupima vitendo vya walinzi, kwa mtindo huo utasema hata benk zinabagua na taasisi zote za serikali.maana walinzi huwa wanatabia zao fulani za kilinzi, na kiutawala huwezi kulaumu organisation policy kwenye media kwa kucourt maneno ya mlinzi.
Watanzania tuna kila sababu ya kujidai at least tukiwa nyumbani, tusijisikie wanyonge nyumbani kwetu.
 
Kama mambo ni hivyo sishangai kwa sababu kuna wakati yaliibuka malumbano baina ya uongozi wa UDSM na wanafunzi waliokuwa wakihoji umuhimu wa mradi huu. Wanafunzi walikuwa wakidai kuwa mradi hauna uhusiano wa moja kwa moja na core function za chuo na hauna faida ya moja kwa moja katika shughuli za chuo hicho.
Inawezekana kuwa ten percent ndiyo imeshawishi watu kusaini contract ya mradi huu

Mkuu cha kusikitisha zaidi yale majengo yenyewe si imara wameweka mabord tu ya mbao kwa hiyo tutegemee baada ya hiyo miaka 50 yatakuwa yamesha oza na kuharibika na wao watakuwa wamesha pata faida mara dufu....sisi tunaachiwa gofu tu.
 
Nadhani ujenzi wa mbao haimaanishi kuwa jengo halitadumu. Tuangalie mfano wa Sweden au Marekani.
 
Huu ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi katika mahoteli yetu ya kitalii pamoja na utaratibu uliopo ni vizuri wakawa wanawafanyia watu wa rangi zote basi. Mfano unaweza kuingia hoteli kubwa labda umevaa simple au casual wear kwa mfano T- shirt , Kaptura na Sandals unazuiliwa kwa sababu mwafrika akipita mzungu hawawazuii. Mimi nadhani hata na huyo mzungu aliyevaa hilo kaptula na singlet naye azuiliwe pia yaani inaboa sana. Wa akina dada hata kama anaenda kutumia pesa zake atahisiwa uchangudoa kwa sababu tu ni mwafrika. Sasa hayo ya Mlimani City ni muendelezo tu wa ufisadi na itafikia wakati tutazimiwa sigara vichwani mwetu.
 
Ush...usijali ilikuwa usiku kwa hiyo sikuweza kupata maelezo.
Dereva wa bajaj wa kituo cha Mlimani city aliniahidi kwamba leo atafanya initiative ya kwenda kwenye vyombo vya habari na mimi nikaahidi kucreate awareness through JF.
Of course kitakachofuata utakiona...huu ni mwanzo ....Ijumaa njema

Mana Lao..Kwa mtazamo wangu naona kuna haja ya kufatilia hili jambo kwa undani ili kujua kama bajaj kuzuiwa ndio taratibu zilizowekwa au la. Kwani napata wasi wasi kuwa kimsingi tulizoea kuona bajaj zikitumiwa na watu wenye ulemavu ingawa kutokana na mchachariko wa maisha watu wameziingiza katika biashara. Hivi akija mlemavu na bajaj yake hapo Mlimani City anataka kufanya shopping nae atazuiwa?

Naomba tupate undani wa hili jambo ili hata watanzania wenzetu wenye ulemavu ambao wanaweza kuingia na bajaj zao wasije kunyanyaswa!!!!
 
Nadhani ujenzi wa mbao haimaanishi kuwa jengo halitadumu. Tuangalie mfano wa Sweden au Marekani.

Ni juzi tuu rafiki yangu mmoja anayefanya kazi NBC branch ya Mlimani City aliniambia roof ya hiyo Benki ilikuwa inavuja maji baada ya Mvua kunyesha ila menejimenti ya mradi huo ulikubali kurekebisha hiyo defect!
 
Nadhani ujenzi wa mbao haimaanishi kuwa jengo halitadumu. Tuangalie mfano wa Sweden au Marekani.

Kweli kabisa lakini kwenye hizo nchi unazizitaja na hali ya hewa inachangia kuyafanya majengo ya aina hiyo yadumu. Hili joto la kwenye nchi zetu, sidhani kama hizo mbao zitadumu
 
kuna wakati wezi wa power window walibuni mtindo wa kupita kwenye parking arkade kubwa kubwa kama mlimani na sea cliff kwa kutumia bajaj...wakifika wanapaki na magari wanaiba power windows ,side mirror,taa ets ..then wanatokomea..na bajaj ikitokomea dakika huipati kwa kuwa inapenya sana...

hata taxi haziruhusiwi kupaki ndani huwa zinapaki nje...
 
PM.

Mkuu shukran wewe umesaidia kutoa mwanga wa huu utata, yaelekea ( kwa mtazamo wangu) tatizo suala la usalama kuliko "ubaguzi" kama tunavyo dhani....
 
Wa akina dada hata kama anaenda kutumia pesa zake atahisiwa uchangudoa kwa sababu tu ni mwafrika.
Vidada vyetu navyo vimezidi kuwinda wazungu vinatutia aibu ndio maana wanafukuzwa.......mimi siwezi kwenda sehemu kuna vidada vya aina hiyo nikiwa na mgeni wangu.....
..........mlimani city sawa tu naona wabongo ustaarabu hakuna wizi ulaghai mtu kaenda kustarehe atoke akute gari lake limekwapuliwa kiooo inatia hasira......waende huko huko kwa wezi wenzao Buguruni,Mwananyamala......
 
Back
Top Bottom