Mlevi aleta gumzo bar baada ya kutoa offa...

mafian

Member
Nov 15, 2011
45
5
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo.
 
kudadadeki ndo wangeelewa maana ya emergency door,cjui wangenionea wapi
 
Mara akatokea bonge na kumfuata jamaa akaanza kumpiga makonde.
Jamaa: Bonge huwezi kunipiga peke yangu wakati wengine humu ndani wananiangalia, mpige kila mmoja aliyeko humu ndani. Watu wakaanza kupigwa!!!
 
Japo muhudumu zilikua zimefyatuka asiweze muelewa nia yake yeye ninani alijichanganya mala kinyaji mala supu naye yupo tu nzuri iyo ila inabidi uwe baunser
 
tehetehe!!! imetulia, lakini kweli kila mmoja alipe alichokula na kunywa!!!!!!!!!!!!!!!!1111
 
mlevi kalewa chakali, hata tundu la ufunguo katika mlango haoni anaangaika kuingiza ufunguo afungue mlango.Trafiki kasimama pembeni anamwangalia mlevi huyu! hatimaye anamfuata na kumshika bega, anamwambia "hebu suburi kidogo bwana,unataka kuniambia una mpango wa kuendesha gari katika hali hii?" Jamaa akageuka, akamwangalia askari yule juu mpka chini, kisha akamwambia " Huna akili nini wewe yaani wewe unadhani naweza kutembea katika hali hii?
 
walevi wana mambo bwana! Wengine wawili walikuwa wanakunywa mmoja akatoa kioo kidogo akajiangalia, akamwambia mwenzie "hii sura sura kwenye kioo sio ngeni lakini nimesahau nilipoiona" Mwenzake akampokonya kile kioo, akajiangalia akamwambia " wee umelewa nini, huyu si mimi!!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom