Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aagiza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akamatwe na polisi popote alipo



Naangalia hapa AZAM TV,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kisare Makori,anasema ameamua kumkamata Meya wa Halmashauri ya Ubungo na kuagiza Polisi wamuweke ndani sababu amekiuka taratibu za kazi kwa kuwaleta wanachama wa CHADEMA wa kanda ya Pwani na kuwatembeza katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo,anasema kwa sheria na taratibu,wenye mamlaka ya kukagua miradi ya maendeleo ni wajumbe wa kamati ya Maendeleo wa Halmashauri chini ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.Hivyo kitendo cha Meya kutembelea miradi ya maendeleo bila madiwani wa kamati husika ni kuvunja sheria,na dawa yake ni kukaa ndani na kufunguliwa mashtaka.

Ameagiza Sumaye na viongozi wengine wa CHADEMA kanda ya Pwani walioambatana na Meya,nao wasakwe na jeshi la Polisi na kutiwa ndani popote pale walipo,ili waweze kujibu ni kwanini walikuja kutembelea miradi ya maendeleo bila idhini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Mkuu wa Wilaya anasema kitendo cha Meya kutumia ukumbi na majengo ya halmashauri kukutana na viongozi wa CHADEMA ni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma,hivyo ameagiza Meya huyo kukaa ndani kwa masaa 48 kabla ya kufunguliwa mashtaka,huku akisisitiza Sumaye na viongozi wengine wasakwe.

My Take:Hivi hapa juzi kati,Mwenyekiti wa "Chama Dume" akifanyia mkutano wa Chama chake Ikulu?Na akasema sbb chama chake ndio kina dola,ni kawaida kufanyia mkutano huko?Kama Meya naye ni kiongozi wa Chama,kuna shida gani akifanya kama alivyofanya mkuu!!?

Ulevi wa madaraka, kaz IPO!
 
Mambo ya gvt usiwe unayavamia tu taarifa hazitokagi zote kama unavyofikiria huwa ipo zaidi ya sabb, usifikiri hata bashite alienda cloud kuvamia kwa mambo yake na jima hut ss tunajua ipo zaid ya sabb pale mawingu ndo maana nikakushauri usitoe maneno kwa facts chache na hii ni sabb ambayo watz huwa tunashindwa mambo mengi
eti mambo ya government nisiwe navamia! Hivi akili zenu huwa zinaondolewa zinawekwa wapi? Katika akili zako unaamini kwamba Bashite alivamia Clouds kwa sababu za madawa ya kulevya kama mnavyoaminishwa? Hii serikali ilipopanua magoli watu wanafunzi wakawa waswagwa kama ng'ombe imewaharibu sana! Tuambie sasa mkuu wa wilaya ya Ubungo alikuwa na sababu gani kuliko hizo za kijinga alizoeleza mbele ya public?
 
Kichekesho cha mwaka ichi
nilikua lockup chumba kimoja na meya wa ubungo nimetoka mda huu kweli power corrupts and absolute power corrupts absolutely'' ukiongoza kwa mihemko mwisho utaumbuka mwisho wa ubaya ni
aibu.
 
Shida chadema nao wamezidi upole,serikali ya ccm inafanya vita na chadema ila wao chadema wamelala,amkeni chadema anzeni kujibu mapigo tunaishi na maccm kamata chinja ndio suruhisho.
 
Mbona Katibu Mkuu wa chama Tawala huwa Anatembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo na ajawai kukamatwa wala kuwekwa ndani
 
Kwani huyu DC na yule Mhandisi wa Urambo mbona wanatumia jina moja??????? Vyetiiiiiii
 
Hivi huyu jamaa akili anazo kweli au ndio kutafuta kiki dah sometimes nacheka tu hamaaa kweli bongo nyoso
 
Hivi hawa viongozi wa hivi mkulu kawatoa wapi. Ila hayo mambo ya hivyo anayapenda kweli, na unaweza kushangaa anapandishw cheo kuwa RC. Chuki kama hizi zinahatarisha usalama wa nchi.
 
Hakuna cha ajabu hapo...vijana kama hawa anawapenda sana Rais John Pombe Magufuli...! Idadi ya maDC na maRC mfano wa huyu kilaza inaongezeka kwa kasi na muda si mrefu Wakuu wa Mikoa wote 30 watakuwa kama Alfred Bashite wa Dar es Salaam na Wakuu wote wa Wilaya 170 watakuwa aina ya huyu Makori Kisare wa Ubungo.

Hapo timu itakuwa imekamilika, timu ambayo imepewa jukumu la kuwasimamia viongozi waliochaguliwa na wananchi kuanzia Wabunge hadi Madiwani wakiwemo mameya wa majiji na kuwashughulikiwa ipasavyo. Pia wamepewa uwezo wa kuamuru hao wawakilishi wa wananchi wakamatwe na kuwekwa mahabusu kwa muda watakaopenda.
 
Wewe Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ni Kikunguni tu, Huna Mandate wala Uwezo wa Kumkamata Waziri Mkuu Mstaafu! I wish Nikutane ya wewe Nikuchape Makofi Mawili matatu Umsukule Ukutoke Maana wewe Ushachukuliwa Msukule na Magufuli Unaongea kwa Makalio badala ya Kinywa!
Mkuu msamehe tatizo lake huyu bwana ni mihemko. Hatambui Waziri Mkuu hata akiwa mstaafu anakuwa na hadhi ipi JK alikuwa anatoa semina elekezi JPM anasema anabana matumizi sasa madhara yake ndiyo haya kiongozi wa ngazi ya wilaya anatoa maamuzi kama kichaaa
 
Back
Top Bottom