Mwalimu kazi yake ni kufundisha. Kusoma na kujifunza ni kazi ya mwanafunzi akisaidiwa na mazingira mazuri ya kujifunza hasa nyumbani. Kama mtoto wa shule ya kata anarudi nyumbani anakuta ng'ombe wanamsubiri awapeleke malishoni akirudi atembee kilometer kadhaa kutafutwa maji, je huyu atasoma kweli? Mwalimu anafanya sehemu ndogo sana ya mafanikio ya mwanafunzi "kumwonyesha maji yako wapi na hawezi kuwalazimisha wayanywe". Hivyo hawa waalimu wameonewa.Mambo mengine yote yalikuwa sawasawa ikiwa ni pamoja na walimu wa kutosha na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia? Jamani naomba job description ya ma-DC.