Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Liberia ajiuzulu !

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
?Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Liberia ambaye amekuwa akituhumiwa kumpendelea Rais Ellen Johnson Sirleaf amejiuzulu, siku chache kabla ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo. James Fromayan anatuhumiwa na hasimu wa Rais Ellen Johnson Sirleaf, Winston Tubman anayegombea urais wa Liberia kwa tiketi ya chama cha CDC, kuwa anampendelea kiongozi huyo. Fromayan amesema kwamba ameamua kujiuzulu kwa ajili ya maslahi ya Liberia ili Tubman asipate kisingizo cha kutoshiriki katika kinyang'anyiro cha duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mgombea huyo wa chama cha upinzani cha CDC alitishia kujiondoa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais itakayofanyika Novemba 8 iwapo uongozi wa Tume ya Uchaguzi hautabadilishwa.

*

*
 
Back
Top Bottom