elizabeth639
New Member
- Feb 13, 2020
- 4
- 3
TUHUMA ZINAZOMHUSU Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof. Ndomba HAZINA UKWELI WOWOTE
Nikiwa mmoja wa wadau wa maendeleo ya TANZANIA, nimesikitishwa sana na tuhuma zilizoelekezwa kwa mkuu wa taasisi ya teknolojia ya Dar es Salaam, Prof. Ndomba.
Napenda kuwasilisha hoja kinzani ya habari zinazohusu mkuu wa Taasisi wa teknolojia ya Dar es Salaam zinazolenga kudhoofisha juhudi za mkuu huyo wa Taasisi, Prof. Preskedis Ndomba. Baada ya kutafakari hoja za mwandishi (ambaye siyo academician) na maneno yanayojirudia katika hoja zake, na aina ya maneno anayoyatumia katika lugha zote anazotumia kila mara, nimeridhika kwa asilimia kubwa kuwa ni mmoja wa watumishi wa DIT.
Kurejea hoja yetu:
Tukubaliane kuwa, si jambo la ajabu kuwa na mawazo na hisia zinazokinzana kati ya watu wawili tofauti. Kama kila ushauri ungekuwa unakubaliwa na kiongozi, ni wazi kuwa matokeo ya maamuzi yake yangekuwa yanayotia wasiwasi. Naamini kwamba Prof. Ndomba ni msikivu sana. Ofisi ya Mkuu wa taasisi iko wazi tofauti na baadhi ya watendaji wengine wa taasisi kama hii. Mimi ni shahidi katika hili. Kama ni ushauri wa busara na wenye kukidhi dira ya Taasisi, ningeshangaa kama ningesikia Prof. Ndomba anaukataa. Hizi anazoziita facts, kimsingi hazina proofs hata kidogo, maana hata mfano wa anazoziita facts hajaziweka hapa. Anachotaka ni kuiaminisha umma wa watanzania kwamba yeye ndiye mwenye kuchambua hizo facts bila kuieleza umma anaojaribu kuaminisha.
Kama mwandishi huyu angekuwa anajua sheria kama anavyojinadi, angejua kwamba Prof. Ndomba, ambaye amekuwa katika kitendo cha rasilimali watu kwa muda mrefu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yenye wasomi lukuki, angepata kashfa ya kutishia kufukuza watu. Ifahamike kwamba kila kiongozi anapitia changamoto nyingi hasa ya kuchukuliana na watu mbalimbali, na njia iliyo rasmi ni kupitisha changamoto kama hizo kwenye organs zinazokubalika kwa mujibu wa sheria. Hivyo kwa kupeleka mtumishi kwenye disciplinary committee (kamati ya kinidhamu) ni utaratibu halali tena wa busara ili kumpa mtumishi huyo nafasi ya kufahamu mapungufu yake na ikibidi kukabiliana na tuhuma husika. Mwandishi anataka kuaminisha umma kwamba hiyo kamati pia ina mapungufu! Mwandishi afahamu kwamba, kamati ya nidhamu ndiyo njia njema kumpa nafasi mtumishi kujitetea. Kwa miaka yote ambayo Prof. Ndomba amekaa DIT hakuna mtumishi hata mmoja aliyefukuzwa kazi, pamoja na mapungufu mengi ya watumishi kiutendaji ambayo mkuu huyo anayapata na kuchukuliana nayo. Nirejee kusema tena, kwa utaratibu huo, Prof. Ndomba atakuwa anamtendea mtumishi huyo haki zote na pengine kumsaidia. Hii inaonyesha mwandishi ndiye hana elimu ya sheria za kazi.
Kwa madai ya kujengea hofu wafanyakazi, napenda kumfahamisha mwandishi huyo kwamba, anayejijengea hofu ni yeye mwandishi mwenyewe, maana watumishi wa Taasisi hii ya teknolojia wanajua haki zao ambazo kwenye mabaraza ya wafanyakazi ambayo yanayo uwakilishi wa kila sehemu wanahudhuria. Katika kikao chochote, mwenyekiti anayo madaraka yake. Kama hoja inayojadiliwa haiendani na ajenda ya wakati huo, ni haki ya mwenyekiti kuongoza. Hata kama maamuzi ya mwenyekiti ndiyo yanayopitishwa, mwandishi huyu anaitukana wajumbe wa vikao hivyo kwamba hawawezi kujenga hoja zao kama zinatofautiana na za mwenyekiti. Niweke wazi kwamba, pamoja na ukweli kwamba hoja za wajumbe wa vikao yanaweza kufautiana lakini katibu wa vikao husika anaandika maamuzi ya wajumbe. Na kikao kinachofuata, wajumbe hurejea minutes na kupitisha zote. Mwandishi kwa kumbukumbu zake aiambie umma kwamba ni minutes za kikao kipi cha ndani ya taasisi ambayo kikao kilishindwa kupitisha kwa sababu siyo hoja zao? Mwandishi atupe heshima zetu kama watumishi wa taasisi na siyo watu wanaoweza kuburuzwa kama anavyoiaminisha umma wa watanzania!
Mwandishi anasema Prof. Ndomba anadhalilisha hata wasaidizi wake! Hivi, kwa akili ya kawaida, unaweza kuamini kuwa Prof. Nsimama na Dr. Najat wanaweza kukubali kudhalilika? Unadhani kwamba hawa viongozi wetu wangeshindwa kukemea hilo? Kwa taarifa ni kwamba, hata kama kungekuwa na tofauti zao, ambayo sitarajii kuwa yasiwepo, Prof. Nsimama anajua wapi anaweza kujisemea na siyo kukusubiri wewe uwe msemaji wake.
Mwandishi huyu anaonyesha mapungufu yake katika uelewa wa kisheria. Katika Taasisi hii kuna ASA, THTU, RAAWU, ambao kama wafanyakazi wananyimwa stahiki zao, vyombo hivyo vingewasemea watumishi hao. Kwa mfano, maswala ya extra duty yako kisheria na yanatolewa kwa miongozo na barua husika inayosema hilo. Kwa kumbukumbu zangu, sikumbuki mtumishi yeyote ambaye anakubalika kupata hizo extra duties akakosa. Siyo kila kazi ya msingi inatolewa extra duty. Mfano, mtumishi anayetumika katika kazi yake ya msingi ya ajira hawezi kudai extra duty! Hoja kama hizi zinaletwa katika baraza la wafanyakazi na yanajadiwa na kupatiwa majibu. Nitashangaa kama mkuu wa taasisi anaweza kutumia kodi na pesa za walala hao kumlipa mtumishi extra duty ambaye tayari analipwa mshahara kwa kazi yake ya msingi. Hivi, mwandishi anaposema Prof. Ndomba analipa kiasi kidogo, kiasi kikubwa ni kipi? Tufahamu kwamba kila kazi inayo malipo yake stahiki na halali. Kuna madai mengine hata yanaweza kutengenezwa kwa namna ambayo siyo halali. Kama kiongozi asipokuwa makini anaweza kuipelekea taasisi na serikali hasara. Namshauri mwandishi aulize ofisi zote zinazopitia na kupitisha malipo ajue mambo yanayokuwa huko! Kila malipo yanafanyiwa ukaguzi na lazima yakidhi sifa!
Madai mazito ya kwamba Prof. Ndomba hana utu, na kwamba hajali maslahi ya wafanyakazi ni ya mwandishi mwenyewe na bahati mbaya hajayaweka wazi. Kwa kweli niseme kwamba, kwa aliyekuja DIT miaka ya nyuma na sasa ataona tofauti. Nilidhani hapa kwa kutengeneza pavement za DIT tungeona kama mafanikio na kwamba sasa yale madimbwi yamekwisha. Ajabu hili kwa mwandishi ni mapungufu! Sidhani kama anajua mikakati mikubwa ya taasisi. Kwa maswala ya ofisi kwa watumishi, ni kwamba, kuna miradi mikubwa miwili mikubwa ambayo inaandaa kutolea majibu mambo ya hostels na ofisi. Lakini pia, kila semester wataalamu wanakuja kupiga dawa katika hostels zote za DIT kama mwandishi hana habari huko alipo, amuulize estate manager kwanza kabla ya kukurupuka kuandika upotoshaji huu!
Na ajabu kuona sasa DIT LIBRARY ilivyo sasa baada ya kufanya kazi usiku na mchana, badala ya kumpa pongezi Prof. Ndomba, lakini yeye anamlaumu. Sisi watumishi wengine tulioshiriki kwa vitendo na tumefurahishwa na hili. Tulipitia kila wakati hatua zote n ahata kutoa ushauri bila kujali taaluma zetu. Kila penye malengo lazima tunapaswa kushikamana kama Taasisi. Kama ni sifa kwa Prof. Ndomba ndiyo mwandishi anaona shida, basi sisi kama watumiaji wa library na waumishi, hili tunastahili sifa wote. Kwa kudai kwamba tulitaka ifunguliwe na waziri mkuu, kwetu sisi ndiyo, tulipenda iwe hivyo. Ninaamini Waziri Mkuu naye angependa kufanya hivyo. Namshauri mwandishi aitembelee library hata sasa na ataona tofauti.
Inashangaza kuona haya mafanikio kwa mwandishi ni mabaya tu. Binafsi sina taarifa ya kwamba Prof. Ndomba anafanya DIT kuwa stepping stone, ila kama ikiwapendeza wateuzi, watakapokuwa wamempa nafasi ingine kubwa zaidi, tunaomba wampendekeze mwenye maono kama haya ya Prof. Ndomba.
Nimshauri mwandishi awe anaandika ualisia na siyo maoni elekezi. Mwandishi anasema, Prof. Ndomba anapenda kila kitu kiandikiwe paper. Labda mwandishi ana uelewa finyu katika hili. DIT kuna tofauti kubwa ya watumishi, tofauti ya elimu, umri, lakini pia taaluma. Mwandishi ajue kwamba, hakuna Project yoyote ya EU ambayo inaopatikana bila uandishi wa proposal. Na isingekuwa rahisi kwa kuipata hiyo project ambayo mwandishi anadai kama haina project concept paper. Kwa kifupi paper kuwekwa ili iwe rahisi kueleweka kwa wana taasisi ambao mwisho wake ndiyo watendaji wa hiyo project ni jambo jema kabisa. Mwandishi ajikite kwenye taaluma yake na siyo hizi za kitaaluma ambayo hana uelewa nayo.
Niombe mwandishi ajue kwamba dhana ya Teaching Factory ni la taasisi pamoja na kwamba inasimamiwa pia na Prof. Ndomba. Katika hili, wale wote ambao hawajitumi na walizoea kudanganya katika tawala zilizopita wanaona ni taabu sana. Teaching factory, inatoa mianya kwa taasisi kushirikisha wadau wengine katika kufundisha waalimu na wanafunzi pia. Hatua ya sasa itakuwa ngumu kwa wenye mawazo kama haya ya mwandishi kuelewa. Namsihi ajishirikishe na mkuu wake wa karibu au wadau tulioielewa dhana ajifunze.
Prof. Ndomba amewapa wengi elimu ya miradi ambayo yeye binafsi ameandaa semina ya kufundisha hili na baada ya elimu hiyo, kuna wana taaluma wengi wameisha ingia katika miradi mingi ya ndani na nje. Kwa kujua hiyo potential iliyopo DIT ndiyo maana tunayo mradi wa world bank ambayo DIT inanufaika, TELMS, na mingine mingi ya ndani.
Waalimu wengi waliokuwa wanahangaika kufundisha nje ya taasisi kwa kukosa miradi kwa sasa wanajikita kwenye miradi. Nina Imani mwandishi amejipima ameona hana viwango vya DIT ya sasa na anajihami. Namshauri mwandishi arejee mikakati na ajione kama anafaa kubaki katika miradi mikubwa ya DIT au aanze mradi mwingine wa binafsi aliyoizoea.
Binafsi, nashangazwa kuona Mh. Pro. Ndalichako anahusishwa katika hili eti kwa swala la family friend. Hili nimuombe waziri wetu, mama yetu mpendwa, ufahamu kwamba hili ni wazo la binafsi na siyo ya DIT community!
Niombe wanataasisi tubaki na umoja wetu. Wakuu wetu wasichoke na sisi na kujua kwamba tuna watu wenye mawazo tofauti na changamoto zetu.
Asanteni