Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,385
- 3,183
Habari wanajukwaa,poleni na majukumu ya siku ya leo
Yupo mkuu wa shule ya sekondari Maweni iliyopo Tanga jiji ambaye amelalamikiwa na walimu kwa muda mrefu lakini Afisa elimu sekondari amekua akimgwaya/akimuogopa mkuu huyo wa shule.
Ninasema anamuogopa kwasababu yupo mkuu mwingine wa shule ya sekondari Kihere alishashushwa cheo kwa tuhuma za ubadhirifu.
Katika tukio jingine,Mkuu huyo wa shule ya sekondari Maweni anatuhumiwa KUTUMIA VIBAYA fedha za ujenzi ambazo zilitoka TAMISEMI kwa lengo la kujenga madarasa.Matumizi yamekua mabaya kiasi kwamba hata hela ya kumlipa fundi haipo. Pia hata samani zilizokwisha lipiwa kwa mzabuni hazijafika shuleni hapo hadi sasa kwa zaidi ya miezi miwili
Fundi huyo amelalamika kwa Afisa elimu huyo imeshindikana kupatiwa ufumbuzi kwa muda wa zaidi ya wiki tatu sasa.
Hata hivyo fundi huyo ameenda TAKUKURU kutokana na matukio yanayoashiria rushwa katika malipo yake hayo. Pamoja na hayo, mkuu huyo wa shule hajawajibishwa na mamlaka iliyomteua
Afisa elimu huyo alishafika shuleni hapo wiki iliyopita akiwa na Afisa utumishi,injinia wa jiji,mkaguzi wa ndani,mwanasheria wa jiji lakini kilichotokea ni jambo la ajabu kwani Afisa elimu ameishia kuwaambia walimu kwamba hawatapata fursa kwani wameonekana kuwa hawamtaki mkuu wa shule
Inasikitisha pale ambapo mtu anafanya ubadhirifu usiokua na kificho halafu haguswi wakati wapo wenzake waliofanya hivyo wameshawajibishwa
Kero hizo za mkuu wa shule pia zilishajadiliwa na Afisa elimu taaluma mkoa wa Tanga wiki iliyopita lakini malalamiko hayo hayajafanyiwa kazi bado
Walimu hao wanaomba itumwe tume huru kutoka TAMISEMI ije ione maajabu ya mkuu wa shule ambaye anafanya UBADHIRIFU MKUBWA katikati ya jiji bila kuogopa na hashikiki na mkurugenzi,Afisa elimu jiji na Afisa elimu mkoa.
Pia Walimu wamedai kuchoshwa na uonevu,ubabe na matusi ya mkuu huyo wa shule ambapo walishamfikishia Afisa elimu sekondari jiji tangu mwaka jana
Suleiman Jaffo,njoo upambane na mwanamke huyu maana wakuu wa idara Tanga jiji hawana misuli inayoweza kumng'oa pale alipo.
Pia ukiweza kumuwajibisha Afisa elimu bwana Gwakisa itakua funzo kwa wakuu wengine wa idara wenye upendeleo
Taarifa zaidi zitakuja kupitia uzi huu