Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Mtafaruku wa Mkuu wa Shirika la Fedha duniani kushawishika na mwanamke wa kiafrika mwenye mtoto wa miaka 9 akiwa mfanyakazi hotelini na kuishia kulazimisha mapenzi bila ridhaa yake. Ninachoshangaa wanawake wa kiafrika kumbe ni moto wa kuotea mbali, mpaka tajiri mwenye ndoto za kuwa Rais wa Ufaransa ameishia kupoteza kazi yake ya sasa, kuacha kampeni za kugombea urais ufaransa na kubaki kusubiria kesi ya kumbaka mwanamke mweuzi wa Guinea ya pembe ya afrika, sasa anasota gerezani huku ulimwengu ukiona kama ni ndoto ya kuwazika tu lakini ndio hali halisi ilivyo.