mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
NEW DELHI,INDIA
MAHAKAMA nchini India imemhukumu kifungo cha jela maisha mwanafunzi raia wa Kenya kwa kosa la kubaka.
Eric Mulinge Nethuli mwenye umri wa miaka 26, alipatikana na hatia ya kubaka Mkenya mwenzake mwenye umri wa miaka 22 mnamo mwaka 2016.
Mahakama ilisema, kijana huyo ambaye alikuwa akisoma na mwanamke huyo alialikwa kwa ajili ya chakula cha usiku na akaitumia fursa hiyo kumbaka.
Mulinge alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya pili ya uongozi katika chuo binafsi nchini India mwaka 2016. Mwanamke aliyebakwa alitoa taarifa katika kituo cha Polisi na hatua za kumkamata mhalifu zikafuata.
Mahakama ilimhukumu Mulinge miaka sita na nusu jela chini ya vifungu 342,352, 506 sehemu ya kwanza ya sheria ya India inayoelezea sheria ya unyanyasaji wanawake na jela maisha chini ya kifungu cha 376 ambavyo atavitumikia sambamba.