Mimi nimpenzi wakusikiliza taarifa za habari TBC, ila kila ninapo msikiliza mkuu wa mkoa kauli zake uwa nahisi anafikiri watanzania ni wajinga na wasio na akili. Kwamfano leo ktk taarifa ya habari TBC alikuwa akisema juu yakupanua "huduma za afya kwa kuongeza vitanda na majengo ya wodi za wagonjwa tu". Binafsi huu nauwita upumbavu kama sii ujinga kabisa. Jamani hivi kweli kwa mwenye akili huu sio ule mtindo wakujenga madarasa meng ila walimu,vitendea kazi, namazingira ya ufundishaji haya fai. Hivi kweli watanzania wataendelea mpaka lini kufa kama kuku wa mdondo kwa kukosa uduma bora za afya? Hivi hawa viongoz wanafikiri watanzania hawakwenda shule na wote wanafoji vyeti kama wao? Nihuyuhuyu mkuu wa mkowa aliwahi kunukuliwa akisema wanafunzi wapande kwenye malori ya mchanga kupunguza adha wanaipata wanafunzi ktk usafiri, hivi do we have intelligency unity kuwapima viongoz b4 hawajawa viongozi? Mbona taifa linakosa dira na mwelekeo kwakuwa naviongoz vipofu kama hawa? Mwalimu J. K. Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikushauri jambo lake la kijinga na wewe ukalikubali basi anakudharau" mwisho wakumnukuu. Taifa hili limekuwa lawajinga nawapumbafu just kwakusikiliza mambo yakipumbavu nakijinga toka kwa wajanja wachache ndani na nje ya nchi. Tumeusaliti utaifa wetu, tumeusaliti na utu wa mtanzania nakwa hakika hakuna atakaye pona. Mungu ibariki Tanzania.