Mkutano wa Nape Iringa: Wananchi kuhuduria wakiwa wanalia huku wameshika vichwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Katika kudhihirisha kuwa wananchi wa kusini wameichukia CCM kesho wakazi wa iringa mjini na viunga vyake wamedhamiria kuungana na kuhudhuria katika mkutano wa ccm utakaofanywa na NAPE wakiwa wameshika vichwa huku wakilia mkutanoni kama ishara ya kuichoka ccm pamoja na maisha magumu

Hili lilianza jana kama tetesi mitaani lakini likajithibitisha leo baada ya kamanda ALLY BANA kuliibua kwenye mkutano wao leo pale KIHESA chini ya kamanda KABWE NA MILLYA na wananchi kukubali kwa pamoja kitu ambacho nimeshindwa kujua ni kwa kiasi gani hawa makamanda wana intelligencia ya kufahamu nini kinaendelea mitaani hasa kwa wanachi wa kawaida

MY TAKE

Nape kesho jiandae tena ujipange kwani yawezekana ukazomewa na hata kutolewa mbio kama mwizi kwani sio siri tena wananchi wamewachoka magamba na sio vijana tu, hata wazee na wanawake

CCM poleni sana
 
Kama kawaida yake, Nape atakusanya waalim na wanafunzi na kuanza kutoa maagizo kwa watendaji serikalini. Walimu wamekuwa victims wa mikakati ya Nape!
 
Iringa town,maeneo ya Ipogolo,Kitanzini,kihesa,Frelimo,Mlandege,Kitanzini,Don Bosco,Mkwawa nawaamini kuwa mtampa Nape stahili yake. Asifurukute hapo mjini
 
Napata tabu sana kuamini kuwa Chadema wameshindwa kabisa kuhujumu mikutano ya Nape mpaka watumie mbinu iliyopitwa wakati kiasi hichi!!!!!!!!!???? Haya maajabu ya mwaka!! Nanaambuwa baada ya juhudi kubwa za kuzuia watu wasijitokeze kushindwa sasa wanawasihi watu waende mkutanoni kwa style hiyo!!! Kimsingi leo cdm wametangaza sana mkutano wa Nape kiasi kwamba atafunika bovu kesho....

Katika kudhihirisha kuwa wananchi wa kusini wameichukia CCM kesho wakazi wa iringa mjini na viunga vyake wamedhamiria kuungana na kuhudhuria katika mkutano wa ccm utakaofanywa na NAPE wakiwa wameshika vichwa huku wakilia mkutanoni kama ishara ya kuichoka ccm pamoja na maisha magumu

Hili lilianza jana kama tetesi mitaani lakini likajithibitisha leo baada ya kamanda ALLY BANA kuliibua kwenye mkutano wao leo pale KIHESA chini ya kamanda KABWE NA MILLYA na wananchi kukubali kwa pamoja kitu ambacho nimeshindwa kujua ni kwa kiasi gani hawa makamanda wana intelligencia ya kufahamu nini kinaendelea mitaani hasa kwa wanachi wa kawaida

MY TAKE

Nape kesho jiandae tena ujipange kwani yawezekana ukazomewa na hata kutolewa mbio kama mwizi kwani sio siri tena wananchi wamewachoka magamba na sio vijana tu, hata wazee na wanawake

CCM poleni sana
 
Angalia CCM walivyo wanafiki; Unadhani hawataki? Ni kama Ufisadi Wanaukemea kama vile hawautaki

208906_378887195503865_2107890536_n.jpg
 
Nape hawezi kuitetea sisiemu. Haibebeki ile.

Nape achana na gunia la misumari hilo, hayo mazee ya CCM kuiba hayataacha mpaka tutakapopuliza kipyenga 2015 kwa nguvu ya umma na kuisambaratisha CCM na kuwafikisha mahakamani waliofisadi wote ambao CCM imezidi kuwakumbatia kama vile Chenge, Lowasa, Mkulo na Maige.
 
Huyu bwana ni mwepesi sana anasema mambo anayo jua hayatekelezeki

mfano; Anajua fika kuwa maisha ya watu ni magumu na wafanyakazi wana madai mengi sana serikalini ambayo inaendekeza zaidi anasa anawapiga marufuku kujadili siasa ili hali anajua siasa ndizo zilizo tufikisha hapa tulipo.

kimsingi Nape bado sana kauli zake mara nyingi zina utata
 
Namuonea huruma jamaa huyu.Sijui ni nani anayemkubali. walisema nabii hakubaliki kwao sasa huyu hata ugenini?
 
Nape pekee hataweza kuinusuru CCM na anguko kuu, ni jukumu la wanaCCM wote kupigania jahazi lao lisizame.
 
Back
Top Bottom