Mkurugenzi wa jiji la Dodoma epuka mtego wa Diwani huyu

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma

Naomba kuuliza swali... Kuna watu wapo juu ya sheria?

Leo tarehe 6 March asubuhi kulikuwa na zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa kiholela katika kata ya Kizota maeneo ya Mbuyuni na Stendi ya mnada mpya.

Wafanyakazi kutoka manispaa wamefanikiwa kubomoa nyumba za wananchi katika maeneo hayo.

Suala la kushangaza ni kitendo cha Diwani wa Kata ya Kizota kumkingia kifua mtu mmoja ambaye amejenga frame katika eneo la stendi ya mnada mpya.

Zoezi la kubomoa nyumba hiyo ya frames ilianza vizuri kwa kufanikiwa kubomoa upande mmoja wa jengo. Wakati zoezi hilo likiendelea wananchi walimpigia simu mmiliki wa frame hizo ambaye alifika haraka sana eneo hilo akiwa na Diwani wa Kata ya Kizota.

Baada ya Diwani kufika hapo aliwaamulu wasimamishe zoezi hilo.

Baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo waligadhabishwa sana na double standard hiyo hadi kufikia hatua ya kutaka kuleta vurugu.

Kabla ya zoezi hili kufanyika, mhusika alipewa onyo ya kusitisha ujenzi wakati jengo hilo likiwa katika hatua ya msingi. Lakini alikaidi na kuendeleza ujenzi.

Wananchi wanajiuliza ni kwa namna gani serikali itekeleze maamuzi ya kisheria kwa kupendelea wenye nacho na kuwatupilia mbali maskini?

Mwaka jana Waziri mkuu alisitisha ujenzi wa frames zilizokuwa zimejengwa katika eneo la uwanja barabara ya kuelekea NBC Dodoma baada ya frame hizo kuwa zimekamilika kwa asilimia .

Najiuliza inakuwaje watu wajenge hadi kufikia hatua hizo bila kudhibitiwa? Wakurugenzi na watendaji wa idara ya ardhi mnafanya kazi gani huko maofisini?

Waziri wa ardhi na mamlaka zingine tafadhari chukueni hatua stahiki maana wanasiasa hasahasa madiwani ni vyanzo vikubwa vya migogoro ya ardhi.
 
Hii ni hatari sana kwa kweli. Kama uongozi umewashinda wakae pembeni
 
Umemtaja mkurugenzi, lakini kuna mtu humu amemlalamikia huyo mkurugenzi kwamba kawatapeli viwanja, sasa sijui huyo diwani anaweza kuchukuliwa hatua na huyo mkurugenzi?
 
Back
Top Bottom