Mkurugenzi NHIF tuhurumie sisi wanachama

mi_mdau

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,104
1,476
Kama mnakumbuka magazeti kadhaa ya jumamosi yalikuwa na habari zinazoelezea matumizi mabaya ya takribani bilioni 30 za kitanzania yaliyofanywa na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF). Fedha hizo zilitumika vibaya, pamoja na maeneo mengine, kwenye manunuzi yasiyofuata taratibu.

Pia kama mnakumbuka kuna post iliwahi kutolewa humu kipindi cha nyuma kidogo ikimtuhumu Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo wa wakati huo ambaye ndiye bado yuko mpaka sasa kwa mambo mbalimbali ikiwemo ufujaji wa fedha, ubabe, kuhamisha wafanyakazi hovyo hovyo, upendeleo usio na tija na mengineyo. Kama malalamko haya yote yasingechukuliwa kwa masihara na wahusika basi pengine fedha hizi na hata nyingine ambazo hatuzijui, na ni zetu sisi wanachama zisingepotea.

Leo hii wanachama tunaendelea kulalamikia kiwango kidogo tunachowekewa kama limit ya kiwango cha matibabu huku baadhi ya watendaji wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu huyo asiye na maadili na mwonevu wakifuja fedha zetu kujinufaisha.

Ni wakati sasa kwa wahusika kuchukua hatua sahihi ili pesa zetu wanachama zitunufaishe wengi na si wachache. Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo ameshatuhumiwa pia kwa kujichukulia maamuzi yake binafsi bila kufuata ushauri sahihi wa watendaji walio chini yake.

Atafanya anachokiona yeye ni sahihi na chenye manufaa kwake binafsi. Hufikia hatua ya kuwatishia, kuwahamisha, kuwapa onyo na kuwachukia sana wale wote anawaona wanasimamia misingi bora ya kazi na haki na wanaoutakia mema mfuko.

Amekuwa mtu wa kujikomba kwa wakubwa ili aendelee kubaki hapo. Ameufanya mfuko huo kuwa kama mali yake na kusahau kuwa ni mali ya umma. Unatuumiza siye wanachama masikini na umeshachuma vya kutosha sasa utuhurumie na utuachie mfuko wetu watanzania. Tanzania hii inabidi ibadilike kama tunataka maendeleo hasa kwenye sekta hii ya afya.

Mungu msimamia haki anilinde na kunisaidia kwa sina sababu ya kuamini kuwa nimemsingizia mtu. Nawakilisha.
 
Hivi huzielewi nyakati hizi!!? Ni ya chukua chako mapema ,,uchakachuaji mtupu,halafu jinsi wanavyowalazmisha watu wachange basi! Niliwahi kuzunguka hapa mjini,ka tyre ya gari. Ajili ya vijisenti vyangu vya nssf ,we acha tuuu! Sijui hii ni nji gani?lakini kila jambo lina mwisho wake nakwambia!ipo siku watu watakomalia haki zao za msingi af ndo tutajua kipi kichwa upi mkia alaaa!
 
huo mfuko mzima wa bima wa afya ni kero tupu....unaweza kuamini mtu kajiandikisha mwezi januari 2011 na anakatwa makato kwenye mshahara wake toka januari 2011 na mpaka leo hajapewa kitambulisho kitakachomwezesha kutumia huduma za afya?
kutengeneza kitambulisho, iwe cha kubandika picha au smart card inachukua dakika chache sana lakini miezi mitano inapita watu hawajapata vitambulisho na wanakatwa makato....
wizi tuuu umewajaa baadhi ya watendaji.
 
Back
Top Bottom