Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande asema pamoja na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Nyerere, watanzania tutegemee migao zaidi!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Nilishangazwa Sana na kauli aliyoitoa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, eti pamoja na mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere, kukaribia kukamilika, watanzania tutegemee mgao zaidi wa Umeme, Kwa kuwa mahitaji ya Umeme wa nchi hii ni Megawatt 60,000😎

Maneno hayo aliyatoa katika mjadala maalum, ulioandaliwa na Mwananchi Twitter Space.

Hivi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, anatufanya watanzania wote hatuna akili, tusiokumbuka maneno yaliyotolewa na viongozi wetu wakuu wa nchi, kabla ya kukamilika Kwa mradi huo mkubwa kabisa wa nchi, ambao watanzania tumekamuliwa zaidi ya shilingi trillion 7 kuwa mradi huo ndiyo utakaokuwa mkombozi Kwa nchi yetu, Kwa kuwa mradi huo unategemea kuzalisha Umeme wa Megawatt 2,115 na tutazalisha Umeme wa "surplus" ambao kama nchi tunategemea kuwauzia Umeme nchi za jirani, na hivyo kutengeneza pesa nyingi za kigeni.

Hivi Hawa viongozi wetu wanatuonaje watanzania, kiasi cha kupenda kutuongopea watakavyo?

Inavyoelekea huyo Maharage Chande, anatuandaa watanzania kisaikolojia, Ili tutakapoona mgao unaendelea, basi tujue kuwa KAZI INAENDELEA, ya kuuza majenereta yao😞

Mimi naona muarobaini wa tatizo hili sugu la kuongopewa watanzania wakati wote na viongozi waandamizi wa serikali hii ya CCM, ni kuwapiga chini watawala Hawa wa CCM na kukiingoza chama kingine Ili kiingoze nchi.

Bila hivyo matatizo ya watanzania hayatakuja kutatuliwa na watawala hawa wa CCM Hadi mwisho wa Dunia hii😎

====

Chande: Bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa viwanda

Muktasari:

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande amesema mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kuendesha uchumi wa viwanda.

Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema, licha ya juhudi za Serikali kuongeza vyanzo vya umeme likiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa uchumi wa viwanda.

Ameyasema hayo leo Desemba 21 katika mjadala wa Mwananchi- Twitter Space unaoendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

Amesema Mradi wa Bwawa wa Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kukamilika mwaka 2024 ni sehemu ya hatua za kupunguza changamoto hizo.

“Mradi huu utaleta umeme mwingi kwenye gridi, lakini mradi huu ni moja kati ya hatua ya safari ndegu ambayo tunayo kama nchi ya kuzalishaji kusafirisha na kusambaza umeme,” amesema Chadema leo Desemba 21, 2022 wakati wa mjadala.

Katika ufafanuzi wake, Chande amesema utafiti uliofanyika katika majarida mbalimbali unaonyesha ili uwewe na umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na kukuza uchumi kila watu milioni moja wanahutaji megawati 1,000.

“Kwa idadi ya watu milioni 60, utaona tunahitaji umeme megawati 60,000 lakini kwa sasa tuna megawati 1500, tukileta hii 2115 tutakua na takribani megawati 3,800. Tunakazi kubwa ya kuongeza uzalishaji wa umeme,” amesema Chande.

Katika hatua nyingine, Chande amesema kama hakutakuwa na changamoto, ratiba ya kukamilisha mradi huo inabaki kuwa mwaka 2024.

“Hakuna aliyetegema Covid19, utaona pia kama bwawa hilo ikitokea changamoto tutatoa taarifa lakini mambo yakienda vizuri Juni mwaka 2023 tutakuwa tumemaliza,” amesema

Kesho Desemba 22, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua hatua ya kuanza kujaza maji katika bwawa hilo lililokamilika asilimia 79 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa Sh6.5trilioni zitakazokata kero kabla ya 2025.

Bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 33.2 za maji eneo la Mto Rufiji mkoani Pwani, lilianza kujengwa 2019.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Nilishangazwa Sana na kauli aliyoitoa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, eti pamoja na mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere, kukaribia kukamilika, watanzania tutegemee mgao zaidi wa Umeme, Kwa kuwa mahitaji ya Umeme wa nchi hii ni Megawatt 60,000😎

Maneno hayo aliyatoa katika mjadala maalum, ulioandaliwa na Mwananchi Twitter Space.

Hivi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, anatufanya watanzania wote hatuna akili, tusiokumbuka maneno yaliyotolewa na viongozi wetu wakuu wa nchi, kabla ya kukamilika Kwa mradi huo mkubwa kabisa wa nchi, ambao watanzania tumekamuliwa zaidi ya shilingi trillion 7 kuwa mradi huo ndiyo utakaokuwa mkombozi Kwa nchi yetu, Kwa kuwa mradi huo unategemea kuzalisha Umeme wa Megawatt 2,115 na tutazalisha Umeme wa "surplus" ambao kama nchi tynategemea kuwauzia Umeme nchi za jirani, na hivyo kutengeneza pesa nyingi za kigeni.

Hivi Hawa viongozi wetu wanatuonaje watanzania, kiasi Cha kupenda kutuongopea watakavyo?

Mimi naona muarobaini wa tatizo hili sugu la kuongopewa watanzania wakati wote na viongozi waandamizi wa serikali hii ya CCM, ni kuwapiga chini watawala Hawa wa CCM na kukiingoza chama kingine Ili kiingoze nchi

Bila hivyo matatizo ya watanzania hayatakuja kutatulowa na watawala Hawa wa CCM Hadi mwisho wa Dunia hii😎
Haya wengine tulishayaona siku nyingi tu:

 
.....Kariba HEP limepunguza uzalishaji wa umeme kisa mvua chache, Tanzania tunahitaji umeme unaozalishwa na upepo, nyukilia, hizi tunazoziona ni mbembwe tu,kumbuka gas ya mtwara, coal kule kiwira zote ni blah blah tu
 
Back
Top Bottom