saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,399
- 6,419
Mkurugenzi mkuu CPA Habibu Suluo hizo namba zenu tajwa hapo juu hazina msaada toa namba zako za mkononi, unaogopa kusumbuliwa wakati uko kutumikia watanzania? Hizo namba ukipiga kuna vijana hupokea hawana msaada zaidi ya kukuudhi zaidi. Kwa mfano wanakujibu mpigie meneja wa mkoa wako, kwanza huna namba ya huyo meneja wa mkoa wako, pili wamezitoa za nini? Kujikosha kwa Rais.
Tatizo lingine kubwa naloona kuhusu matatizo yanayowapata wananchi kutoshughulikiwa ni waziri mwenye dhamana. Profesa Makame Mbarawa zaidi ya kujishughulisha na miradi ya wizara hajishughulishi kufuatilia matatizo ya wananchi yeye huhangaika na miradi ya wizara.
Mheshimiwa Rais kama unampenda sana kwasababu ni mzanzibari mwenzio mpeleke wizara nyingine au muundie wizara yake na iitwe wizara ya Miradi ya Serikali. Waziri pekee aliyeifaa hii wizara hii ni Dr. Harrison Mwakyembe, yule bwana aliiweza hii wizara. Tuletee mtu kaliba ya Mwakyembe, kwanza mhe Rais unajua nauli tunayopigwa? Pamoja na kwamba nauli imeongezwa mara 2 ndani ya mwaka 1 tendo ambalo halijawahi kutokea nchi hii wenye mabasi wamejiongezea zaidi ya nauli ya Serikali.
Kwa mfano nauli ya Arusha-Babati inatakiwa iwe sh. 8,000 mabasi yanachaji sh. 10,000, hili ongezeko la karibu asilimia 100 maana mwaka juzi nauli ilikuwa sh. 6,000. Wazanzibari mnatupeleka wapi sisi wabara? Kule kwenu hakuna haya. Mambo haya yanaleta hisia mbaya sana, huyu mzanzibari hatufai ktk hii wizara matatizo yetu hayamgusi. TULETEE MWAKYEMBE au anayefanana naye tumechoka wenye mabasi wanatutesa utafikiri hakuna serikali.