HERY HERNHO
Member
- Mar 4, 2022
- 70
- 313
Inatimia miaka saba leo Jumapili tangu tetemeko kubwa la pili la ardhi kuutikisa mkoa wa Kumamoto unaopatikana kusini magharibi mwa Japani.
Tetemeko hilo lililokuwa lenye kiwango kikubwa zaidi cha saba kwenye kipimo cha matetemeko nchini Japani lilitokea katika mji wa Mashiki Aprili 16 mnamo mwaka wa 2016, siku mbili tu baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la kwanza.
Maafisa wanasema jumla ya idadi ya watu waliofariki inafikia 276, wakiwemo watu waliofariki miaka kadhaa baadaye, kutokana na matatizo ya kiafya au sababu zinazohusiana na msururu wa matetemeko ya ardhi.
Katika eneo la Aso, Daraja la Aso Ohashi lilianguka kutokana na maporomoko makubwa ya ardhi ambayo pia yaliharibu barabara kuu za kitaifa na reli ya Japan Railway Hohi Line.
Ujenzi mpya wa miundombinu unakaribia kumalizika kufuatia ujenzi wa Daraja la Shin-Aso Ohashi.
Majaribio ya uendeshaji wa treni pia yameanza kwenye reli ya Minami Aso Railway Line kabla ya kufunguliwa tena kwa reli hiyo yote kulikopangwa kufanyika Julai 15.
Utafiti uliofanywa na mji wa Kumamoto mwaka huu unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya washiriki walisema kumbukumu zao za matetemeko hayo zinapungua.
Katika juhudi za kuvirithisha vizazi vijavyo mafunzo yaliyotokana na janga hilo, mji huo umetenga Aprili 16 kama siku ya kuwakumbuka waliofariki.