Mkoa wa Kikodi Wa Kariakoo Waweka Rekodi Kwa Kukusanya Kodi Shilingi Bilioni 40.8.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,728
Kariakoo imeanza kurudi Kwenye ubora wake wa kuwa Kituo Cha Kimataifa Cha Biashara..

MKOA wa kikodi wa Kariakoo umevunja rekodi kwa kukusanya Sh bilioni 40.8 sawa na asilimia 102 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na TRA na wafanyabiashara wa Kariakoo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete.

Kidata amesema mkoa wa kikodi wa Kariakoo wenye wafanyabiashara 30,000 umekusanya Sh bilioni 40.8 sawa na asilimia 102 kwa mwaka uliopita wa fedha 2022/2023 ambapo awali Kariakoo haijawa mkoa wa kikodi walikuwa wakikusanya Sh bilioni 14 kwa mwaka.
 
Kariakoo ni just section yenye wafanyabiashara 30,000 tuu ,huko kwingine ni Mkoa mzima
Unadhani kwanini Dar es Salaam ambayo ndio mkoa mdogo wao kwa Tanzania Bara, lakini una mikoa ya kikodi kibao?
Jibu ni potentiality ya huo mkoa tafauti na mikoa mingine pamoja na ukubwa wao wa bure, the same for Kariakoo to be a Tax Region.
 
Unadhani kwanini Dar es Salaam ambayo ndio mkoa mdogo wao kwa Tanzania Bara, lakini una mikoa ya kikodi kibao?
Jibu ni potentiallity ya huo mkoa tafauti na mikoa mingine pamoja na ukubwa wao wa bure, the same for Kariakoo to be a Tax Region.
Usiseme ni Bure,Dar haijawa hivyo Kwa sababu ya nature Bali uwekezaji wa Serikali over 60 years
 
Mwenye chati ya mikoa yote kwa ujumla KAMA MIMI aweke hapa watu wasio nayo wafananishe...

Kama wote hamna basi
Rubish kabisa, manawaza ngono tu.
 
Back
Top Bottom