Mkiona mgonjwa wenu hawezi kupona, mrudisheni akafie nyumbani. Akipelekwa tu Mortuary mtadaiwa mamilioni msiyoyaweza

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,224
Nchi hii imekuwa ya hovyo sana, huduma za afya na matibabu zimekuwa mbovu na duni kabisa.

Kila siku tunasikia sehemu mbalimbali watu wakifa kwa uzembe wa madaktari na manesi.

Mbaya zaidi mgonjwa akifa haraka haraka anakimbizwa mortuary ambako kama hamna mamilioni kadhaa, ndugu yenu atazìkwa na halmashauri, mazishi yasiyo na heshima wala staha wala stara.

Wito wangu kwa Watanzania wenzangu, mkiona mgonjwa wenu hana dalili za kupona hospitali, mrudisheni nyumbani kuepuka kadhia ya kudaiwa mamilioni mengi wakati wa kuchukua mwili wake.
 
Nchi hii imekuwa ya hovyo sana, huduma za afya na matibabu zimekuwa mbovuna duni kabisa.

Kila siku tunasikia sehemu mbalimbali watu wakifa kwa uzembe wa madaktari na manesi.

Mbaya zaidi mgonjwa akifa haraka haraka anakimbizwa mortuary ambako kama hamna mamilioni kadhaa, ndugu yenu atazìkwa na halmashauri, mazishi yasiyo na heshima wala staha wala stara.

With wangu kwa Watanzania wenzangu, mkiona mgonjwa wenu hana dalili za kupona hospitali, mrudisheni nyumbani kuepuka kadhia ya kudaiwa mamilioni mengi wakati wa kuchukua mwili wake.
Waambie CHAWA wanaoanzisha nyuzi za kusifia humu JF kila siku kina CHOICE VARIABLE,LUCAS MWASHAMBWA, JIDULABAMBASI,KABENDE MSAKILA nk wachangishane wakakomboe maiti ya Mtoto wa miaka 5 iliyozuiliwa Muhimbili kisa inadaiwa 2,400,000
 
Kuna Siku Nilikuwa Muhimbili pale wodi ya Mwaisela napiga michango nakuta Familia ya Kiarabu ya watu kama watatu wanalia,nikamdodosa mmoja akaniambia Shangazi Yao kafariki wanafanya process za kuchukua mwili,nikamuuliza amefariki lini?akajibu Leo wakati tunamleta kufika hapa kumbe alikuwa amefariki kwenye gari,wamefika pale Dr anawaambia mbona alishafarki!Wanataka kugeuka na Mwili wa Shangazi wanaambiwa hapana upelekwe Mochwari.Jamaa waling'ang'aniwa mpaka maiti ikapelekwa Mochwari Sasa msala kuitoa.
 
Huu ni upuuzi, hospitali mtamdai nini mtu aliyefiwa na mgonjwa wake, si aruhusiwe tu achukue maiti yake akaizike? Kuna jamii mtu wao akifa fisi wanaachiwa wale mzoga huo, sasa kama kafia hospitalini wakianza kudai gharama kubwa mbona wanaachiwa tu wawape wanafunzi wa udaktari wakajifunzie kupasua viungo kama spacemen
 
Ukiona mambo kama haya elewa unaishi in a shithole country, kila family ilitakuwa iwe na uchaguzi na uamuzi wa wapi maiti yao ikahifadhiwe, kama nchi tulitakiwa tuwe na private undertakers, means unapeleka mwili wa mpendwa wako kwa undertaker unayemtaka,pia ni wajibu wa undertaker wako kukuandalia death certificate kutoka home affairs, sio uchafu uliopo hapa nchini, Ile idara ya vifo na mirathi ilitakiwa futilia mbali uchafu ule, sawa na msajili wa vyama futilia mbali, vyama vikajisajili NEC.
 
Kuna Siku Nilikuwa Muhimbili pale wodi ya Mwaisela napiga michango nakuta Familia ya Kiarabu ya watu kama watatu wanalia,nikamdodosa mmoja akaniambia Shangazi Yao kafariki wanafanya process za kuchukua mwili,nikamuuliza amefariki lini?akajibu Leo wakati tunamleta kufika hapa kumbe alikuwa amefariki kwenye gari,wamefika pale Dr anawaambia mbona alishafarki!Wanataka kugeuka na Mwili wa Shangazi wanaambiwa hapana upelekwe Mochwari.Jamaa waling'ang'aniwa mpaka maiti ikapelekwa Mochwari Sasa msala kuitoa.
Duuuh!! Mbaya sana hii
 
Ipo siku watu watakuja kususia miili ya waliofariki ikae huko huko mortuary ijazane sijui wataila nyama!!
 
Nchi hii imekuwa ya hovyo sana, huduma za afya na matibabu zimekuwa mbovu na duni kabisa.

Kila siku tunasikia sehemu mbalimbali watu wakifa kwa uzembe wa madaktari na manesi.

Mbaya zaidi mgonjwa akifa haraka haraka anakimbizwa mortuary ambako kama hamna mamilioni kadhaa, ndugu yenu atazìkwa na halmashauri, mazishi yasiyo na heshima wala staha wala stara.
Huwa hatuamini kama atakata moto!
Wito wangu kwa Watanzania wenzangu, mkiona mgonjwa wenu hana dalili za kupona hospitali, mrudisheni nyumbani kuepuka kadhia ya kudaiwa mamilioni mengi wakati wa kuchukua mwili wake.
 
Ipo siku watu watakuja kususia miili ya waliofariki ikae huko huko mortuary ijazane sijui wataila nyama!!
Mmoja toka Lindi alisusa,kamleta mkewe alipewa referral kuja pale mkewe kajifungua bahati Mbaya kaondoka,huku na huku Wanataka Mil 3 hiyo nauli ya kuja tu ndugu walimchangia kazunguka wiki mzima Kila ofisi wapi.Karudi temeke alikofikia kaweka Msiba siku tatu, baada ya hapo watu wakatawanyika arobaini Lindi.Ninyi na hiyo Mochwari yenu mtajijua.
 
Akili kubwa hiyomaisha magumu bado ukamuliwe na Kodi ya Maiti kweli!!!hapana
 
Mmoja toka Lindi alisusa,kamleta mkewe alipewa referral kuja pale mkewe kajifungua bahati Mbaya kaondoka,huku na huku Wanataka Mil 3 hiyo nauli ya kuja tu ndugu walimchangia kazunguka wiki mzima Kila ofisi wapi.Karudi temeke alikofikia kaweka Msiba siku tatu, baada ya hapo watu wakatawanyika arobaini Lindi.Ninyi na hiyo Mochwari yenu mtajijua.
Tena huko Lindi ndio wanachagua MATAGA sana ataenda kuwasimulia wenzake kilichomkuta hospitali DAR.
 
Hii kero ya miili kuzuiwa iliyoletwa na serikali ya CCM ipelekeni kwa waziri kiongozi mwenezi makonda itatuliwe on the spot.
Sasa hivi tunayo hii fursa ya kupeleka kero zetu. Tuitumie otherwise mwakani huyu akipewa ubalozi itakua business as usual.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom