fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,416
- 7,969
Wanaume wengi sana, tuna dhana kwamba mke ni adui, na mara nyingi tunatumia vitabu vya dini eti vinasema tukae na wanawake kwa akili, kweli? Huyu Mungu ambaye ndiye aliowaumba anaweza kuwatengeneza wanawake wawe maadui kwa wanaume? No, sio kweli, hivyo vitabu vya dini hizo aya za hivyo zimeandikwa na wanaume kwa maslahi ya wanaume. Ewe mwanaume mwenzangu, mkeo ndiye rafiki yako mkubwa, ndiye mwandani wako, mpende, mpe raha, mpe kila aina ya usaidizi.