Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Uingizaji na usambazaji wa kemikali bashirifu hufanyika chini ya udhibiti wa hali ya juu wa mamlaka za kitaifa na kimataifa kuzuia uwezekano wa kuchepushiwa katika utengenezaji wa dawa za kulevya aina ya heroin na cocaine.
Taarifa zinasema Profesa Manyele, ambaye juzi alihojiwa kwa siku nzima, alichukuliwa tena jana mchana kwa mahojiano zaidi yaliyofanyika makao makuu ya DCEA, Upanga jijini Dar es salaam.
Hadi tunakwenda mitamboni Profesa Manyele alikuwa bado mikononi mwa DCEA, kwa mujibu wa taarifa ambazo Mwananchi ilizipata, na kuna taarifa zaidi kuwa huenda akaendelea kushikiliwa hadi leo.
Kuhojiwa kwake kwa siku mbili kumetokea sambamba na uamuzi wa Rais Magufuli kumuondoa Mihayo Msikhela kutoka katika nafasi yake ya kamishna wa operesheni wa DCEA, na kumteua Luteni Kanali Frederick Milanzi kushika wadhifa huo.
Juzi, Rais John Magufuli alifanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam na Kamishna Mkuu wa DCEA, Rodgers Siyanga aliyemhakikishia kuwa mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini yanapata mafanikio makubwa.