TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 8,859
- 23,119
Wakuu habari zenu,
Shemeji au wifi yenu ni mjamzito karibu anafunga mwezi wa tatu. Mimba bado ni changa.
Kuanzia mimba ilipotimiza miezi miwili amekuwa akilalamika sana tumbo kumuuma kwenye kinena. Maumivu yalianza taratibu lakini sasa imefikia hatua mpaka anashindwa kuamka. Wakati mwingine anakuwa anaishiwa nguvu hawezi hata kuamka.
Hospitali tumeenda mara nyingi sana. Anaishia kupimwa ultra sound na kupewa dawa za kutuliza maumivu. Madaktari wanasema mimba ipo salama ila aache kufanya kazi ngumu. Tumekuwa tukijitahidi sana asifanye kazi ngumu hata kunyanyua ndoo ndogo ya maji anajizuia. Lakn haipiti siku tumbo likaacha kumuuma.
Hii itakuwa ni nini? Kama kuna mtu anauzoefu na changamoto kama hiyo tunaomba uzoefu pengine utasaidia.
Muwe na jioni njema.
NB: Hii ni mimba ya mtoto wetu wa pili, ya kwanza haikumsumbua, ya pili iliharibika ilipokuwa na miezi sita. Yaani navurugwa sana.