Mke wangu ananifuatilia FB

Kama una watoto umezaa naye ukawapime na DNA kabisa huenda umepigwa changa la macho. Huyo mkeo sio mwaminifu hata kidogo na anakuwa mkali sababu anahisi ANACHOFANYA YEYE NA WEWE UNAKIFANYA. Simama kama mtoto wa kiume acha ulegelege kama hii serikali yetu. Simamia mambo yako kwa ukamilifu kuwa mgumu kama ugali wa dona na maharage ya chumvi,usiwe laini kwake kama ugali wa sembe na mlenda . Ameshakufanya poyoyo wake huyo.SHITUKA MACHALE KUNDESA MEKU
 
ukijitoa fb mwisho wa cku atakuganda tena ujitoe na jf .... badili jina mblock maisha yaendelee ...
 
We unampigia sana magoti ndo mana anajua upo weak hata akifanya chochote anajiamini,Be strong na ujiamini,halafu ushawahi kujua siri zake kuwa hajatulia so hiyo ndo chance ya kumgandamiza.Mi girlfriend wangu alikuwa ananifuatilia sana fb na nikamwambia huwezi ukanilinda kama sintakuwa mwaminifu,maana kama akinizingua fb nitaenda myspace,akijua nitaenda tagged,akigundua Jf,akigundua badoo,so ni kazi bure tu
 
We unampigia sana magoti ndo mana anajua upo weak hata akifanya chochote anajiamini,Be strong na ujiamini,halafu ushawahi kujua siri zake kuwa hajatulia so hiyo ndo chance ya kumgandamiza.Mi girlfriend wangu alikuwa ananifuatilia sana fb na nikamwambia huwezi ukanilinda kama sintakuwa mwaminifu,maana kama akinizingua fb nitaenda myspace,akijua nitaenda tagged,akigundua Jf,akigundua badoo,so ni kazi bure tu

Excellent asante kaka nitafanyia kazi
 
Kawaida ya wazinzi huwa hawajiamini, anadhani anayoyafanya yeye na we ndo hivyo, we sema nae tu polepole atakuelewa coz ni mkeo na unampenda nina hakika uta,badilisha.
 
Hapa ishu sio facebook, ishu ni kuwa umeshikwa masikio.........Amka kwanza halafu urudi hapa ndio tukupe ushauri.
 
ulivyogundua ana mahusiano na rafiki yako ulifanyanye.. Poyoyo!!!!!!!????????? ukamwacha tu
 
Ukiona mwenzako anakushuku kila mara jua anaficha ya kwake na wakati mwingine unaweza mbamba akakwambia nafanya kama unavyofanya wewe kumbe ni janja ya kurahisisha maovu yake. Kwakuwa ulishaingia kwenye mikataba ya kudumu bila kupima kina cha maji, endelea kuvumilia si huwa nasikia mkiapishana kuwa ni katika shida na raha?!
 
Embu mchunguze yeye huko FB mwenendo wake, kuna uwezekano mkubwa yeye akawa ana cheat na kuwasiliana na mijaa yake kupitia facebook, na usiangalie comment na like zake, tafuta means ujue inbox ya account yake ya FB ina nini.
 
Jamani waungwana naomba msaada wenu huyu mke wangu mie simuelewi kabisa.

mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa na tabia sana ya kuchunguza simu yangu na hakuwahi kugundua message yoyote mbaya ingawa hata msg isiyo ya kimapenzi ikiingia kwenye simu yangu so long as inatoka kwa mwanamke basi siku hiyo ni vurugu kupita kiasi akidai huyo mwanamke atakuwa bibi yangu ama mpenzi wangu tu. siku mie niliposhika simu yake siku moja, nikagundua msg nyingi za kimapenzi toka kwa wanaume wawili tofauti, anaomba radhi nikamsamehe.

Baada ya muda alikuwa akinisumbua kwa kudai kuwa mimi nina uhusiano na wanawake chungu tele kuanzia wale ninaofanya nao kazi hadi mtaani. Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe yeye ndio ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu. mini ni mvumilivu nilimsamehe ingawa ni baada ua kukana sana na mwisho wa siku akakubali. hayo yakaisha mwaka jana.

Sasa hivi amekuja na mpya. Anasema kila mwanamke ambaye ni rafiki yangu facebook kwamba ni bibi yangu na anakomaa kwelikweli. mie nashindwa hata nimwambie nini ili aamini kuwa mawazo yake sio kweli maana kuna wasichana zaidi ya 1000 kwenye orodha ya marafiki zangu fb na wavulana kama 1000 wengine. kila comment yangu kwa mwanamke yoyote inakuwa ugomvi hauna mfano, kisa eti na comment kwa bibi yangu. kwakweli sina amani kabisa na hali hii inanikosesha raha.

Naomba waungwana mnisaidie nifanye nini maana nahisi kama anaanza tena kuficha uovu wake kwa kunipakazia mie, nahisi tu hilo sijafanya uchunguzi tena.

Hivi hujaunganisha dots tu kwenye huu mtiririko wa matukio? Nyie ndio mnafanya wanawake wanatudharau bwana - wake up. Any way, umeshasema wewe ni mvumilivu nakushauri uvumilie tu na ukigundua tena kuwa ana mabwana huko face book muulize mwanzoni atakana ila ukimlazimisha atakiri tu. Akikiri na kuomba msamaha umsamehe kama kawaida yako ilivyo.
 
Pole weee kwa kuchagua upole wa kondoo. Anaku pre-empt kwa kukususpect ili yeye aliendeleze libeneke nje wakati unaconcetrate namna ya kukana shutuma zake.
 
Shantel inawezekana nikakubaliana nawe. Lakini upole wangu sio uzezeta, tatizo langu huwa sipendi kabisa ugomvi wa kurushiana maneno kwahiyo huwa na-opt kukaa kimya na kisha kumwambia baada ya kuwa ametulia. Pili siwezi kabisa kumpiga kwa sababu najijua nina nguvu na naweza kuua yawe matatizo mara mbili. Tatu dini inanisumbua sana maana tumefunga ndoa vinginevyo huwa nasema bora ningekuwa mwislamu, angeshakula talaka long time. lakini naufikiria ushauri niliopewa humu maana ni kweli hata Mandela alikuwa na ndoa, why kwangu ishindikane. nadhani inaweza kuwa suluhisho kwa njia moja.

Usisingizie dini hapo. Kwenye suala la uzinzi talaka inaruhusiwa kwenye biblia tena ni Jesus mwenyewe aliyetoa kibali.
 
mtoa mada kuna jambo hujatueleza,inawezekena na wewe mkeo alishawahi kukufuma na mahusiano ya nje au alishawahi kukuta messages za utata huko facebook,haiwezekani akae kimachale machale for no reason at all...mpaka hapo tutakapojua na stori ya upande wa pili,we cant help you!?!
 
Mweh!roho inaniuma,nahisi ka naibiwa mimi vile!Anyway inabidi huyo mkeo ashukuru kuwa na mume kama wewe,manake angekuwa na akina sisi,angeifukuza jet kwa mguu.
 
Maisha ni kufurahi na umpendae kama anakuumiza hajali na ushamuweka chini mara nyingi utakufa na presha tuu ni wazi hauko moyoni mwake ! Labda kama wewe unaficha lakini ndio chanzo cha mwenzako kuwa hivyo bila wewe kujua kwa vitu ulivyowahi fanya .

Mimi ni mfuasi mzuri wa upendo naamini kama upo wa dhati watu wote huwa tayari kubadilika kuliko kupoteza pendo lao , so wewe wajua zaidi ila kuwa na msimamo kama wewe msafi !
 
kaka hapo naona umekua na moyo wa huruma sana, inabidii uchukue hatua kama mume ndani ya nyumba, kosa la kwanza kama anaweza megwa na rafiki yako na unamsamehe hiyo kwangu mimi bana siwezi unyounyo na huyo rafiki yangu wakanze maisha kam mke na bwana mimi nitajipanga mbele mbele. nini bana mwanke anataka kukupimia maisha,kama hawezi jenga ndoa yake kama mke muonyeshe mlango uwazii,kuna wale wanao tafuta nafasi kama hiyo ya kutulie nyumbani. na kama ni rafiki yako fb sium block basi kama amekuja sana. usipuchunga daddy naona wewe unapoteza muda wako kila siku ugomvi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom