'Mke Wangu Anamaliza Pesa Kuwanunua Gigolo'

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
4393914.jpg

Nyota wa filamu Deuce Bigalow kulia akiigiza kama Gigolo kwenye filamu yake ya " Male Gigolo" akiwa na mteja wake mwanamke mwenye urefu wa futi saba.
Ndoa ya miaka 20 ya mfanyabiashara mmoja tajiri nchini Italia inakaribia kufikia tamati kwasababu mke wake anapenda kutumia pesa vibaya kununua makahaba wa kiume 'GIGOLO'. Mfanyabiashara mmoja nchini Italia amefungua kesi mahakamani kuivunja ndoa yake baada ya kugundua kuwa mke wake anatumia pesa nyingi kuwahonga makahaba wa kiume "Gigolo".

Mfanyabiashara huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni aliamua kumuajiri mpelelezi achunguze mienendo ya mkewe baada ya kuona pesa katika akaunti yao ya pamoja zinatoka kwa wingi.

Ripoti ya mpelelezi huyo ndiyo iliyopelekea ndoa hiyo ikaribie tamati yake baada ya kubainisha kuwa mke wa mfanyabiashara huyo tajiri alikuwa akitumia pesa nyingi kuwalipa Gigolo na kutumbua nao raha kwenye klabu za starehe.

Mfanyabiashara huyo ameamua kuivunja ndoa yake na mkewe huyo ambaye wameishi pamoja kwa miaka 20 sasa.

Kumekuwa na ongezeko la wanaume makahaba nchini Italia kutokana na wanawake wengi matajiri wenye umri kati ya miaka 30-40 kupenda kuwanunua magigolo dhumuni kubwa likiwa ni ngono.

Kumekuwa pia na ongezeko la tovuti zinazotoa huduma za kukodisha magigolo. Tovuti hizo huweka picha za wanaume wanaojiuza wakiwa katika mapozi mbalimbali na hivyo kuwapa nafasi wanawake kuchagua wanaume wanaotaka kutumbua nao raha.
 
Kuna shida kwenye ndoa yenyewe ndio maana huyo Mama kaenda kununua vijana wamridhishe nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom