Mke wangu ana majini huwa ananipiga hadi nazimia

francis ole kaparo

New Member
Jul 24, 2015
1
2
Wakati namuoa sikujua kama ana majini, hata hivyo nikiri kwamba sikufanya utafiti wa kutosha kabla ya kumuoa tulidumu kwa miezi sita tu katika uhusiano na kisha kuoana, tuna miaka 4 sasa.

Miezi 4 baada ya ndoa, usiku tukiwa tumelala nilishtuka kuona mke wangu ananipiga kabali ya nguvu nikadhani naota, nilitumia nguvu zote kumtoa bila mafanikio.

Nilikua nimetoa ulimi wote nje, sijawahi kuwa mlokole ila nikajikuta tu nasema moyoni yesu nisaidie, ghafla akaniachia na kujishangaa kwanini amenikaba huku akinikumbatia na kulia.

Asubuhi akaniambia hata yeye hakujua kwanini alifanya hivyo nilikua nikijikanda shingo wiki nzima ndipo nikapona.Mara ya pili nilikuja na bia za kopo nyumbani, nilikua nimetoka baa, alipoziona tu alinirukia na kunikandika ngumi nzito sana iliyonitupa chini na kuzimia hapo hapo.

Akachukua kisu na kuanza kumfukuza nacho mdogo wangu wa kiume aliekua amefunga chuo na hufikia kwangu, alimkimbiza hadi nje ya geti, dogo akaita watu Duka la jirani wakaja ndani, wakamkuta ametupa kisu akilia pembeni yangu huku akinitikisa ndipo wakanimwagia maji nikawa nimezinduka.

Wiki moja mbele tulikaa kikao cha familia pande zote mbili, wazazi wake wakatueleza kuwa binti ana tatizo la majini mwaka wa pili hawajui lilitoka wapi ila wakasema kwa sasa limezidi, hivyo wakaomba nimvumilie tuweze kulitatua pamoja
Ingawa wazazi wangu walikasirika kwanini hawakutuambia tangu mwanzo suala hilo?

Wakati akiwa mjamzito hali ilitulia hakuleta shida hadi alipojifungua, mtoto alipokua na miezi sita, tulikua tunakula usiku, huku mtoto amekaa akicheza, ghafla wife akaanza kuzungusha macho kushoto na kulia na kumshika mtoto na kuanza kumzungusha hewani akitaka kumrusha.

Niliingiwa na nguvu za ajabu nikamrukia, mtoto akaanguka pembeni, akachukua kisu tulichokua tunakatia ugali nikawa namkwepa huku nikipiga kelele za kuita majirani, wakaja majirani na wapita njia wakaruka ukuta na kuja kuniokoa, mtoto alivunjika mkono mimi nilikua na majeraha sehemu mbali mbali, tukapelekwa Muhimbili usiku huo huo na kutibiwa
ndipo mtoto tukamwamishia kwa wazazi wa mke wangu analelewa huko hadi sasa kwa usalama wake.

Wadau wa Jf nimefika pahala nimeshindwa ndoa hii, hivyo nahitaji kujua taratibu za kutoka kisheria, ndoa yetu ni ya kikristo, naweza kuja kufa siku moja, tumekwenda sehemu mbali mbali, ikiwemo makanisa mbali mbali lakini anapona kwa muda mfano hata miezi hata 5 cha kushangaza siku isiyo na jina tatizo linarudi kwa kasi tena mara pili yake, ilfika pahala alitaka kunifyeka nyeti na kisu nikamfungia kwa nje bedroom.

Sasa hivi hata nikipiga kelele vipi za kuomba msaada kwa majirani hawaji tena, maana walishanionya niachane nae siku nyingi, wazazi wangu pia walishanipa baraka za kuachana nae siku nyingi, nikawa namvumilia tu nikiamini huenda atapona lakini wapi

Ndugu bobby dolat ambae ni work mate wangu na pia yupo humu Jf ndie alinishauri kuja humu kuzungumza nanyi tatizo hili, nilimuomba aandike kuniwakilisha lakini alisema niandike mwenyewe ita sound vizuri zaidi, namshukuru sana kwa kazi ya ku edit.

Nimekuja kwenu kujua nifanye nini baada ya njia zote kushindikana,kuna mganga kutoka Kenya nilimleta kwa gharama kubwa amekaa kwetu mwezi mzima ameondoka shida ipo vile vile na zaidi ya yote kwa mara ya kwanza anakimbia nje mbio kanga inaanguka anabaki na chupi tu watu wanamkamata na kumsitiri kisha kumrudisha home.

Kwa sasa wazazi wake wamemchukua wameomba wakae nae kwanza kwa muda hali imekua mbaya,kabla ya kuondoka alipiga marafiki zangu watatu walikuja kunipitia twende sehemu, ilikua ni aibu kubwa kwangu, yaani hata uwe na nguvu vipi huwezi kumshinda.

Kuna yeyote kati yenu aliekutana na shida kama hii na aliitatuaje?

Je, shida kama hii inapona kabisa na kupotea kabisa?

Taratibu za kuvunja ndoa kama hii yangu zikoje?
 
Mapepo yakiondoka kama yata rudi ni mara saba ya yaliyo ondoka sasa,kazi kwako
huyo achananaye tu labda ni mapepo ya ukoo familia yake ina mikataba nayo ndio sababu hawakukwambia, ipo siku utakufa

hii ni kama yule jamaa aliyekata watu kwa kisu kwenye daradara mapepo ni baraa sana duh hadi mtoto noma hii
 
Duh pole sana me nakushauri umpeleke kwenye maombi atafunguliwa tu sa ukemuacha utakua ujamsaidia ebu msaidie atoke kwenye icho kifungo
 
Mpe tuzo ya kuweza kuishi na jini ndani yake.

Muulize kama ajini lake limewahi kumpiga baba yake???????????
 
Umesema hukuwahi kuwa mlokole, ila ulivosema Yesu nisaidie alikuachia.

Hujajua kama hiyo ndio solution? Tatizo lako hutaki kuokoka. Mapepo siku zote ukimtaja Yesu huwa yanakimbia. Sijui huo ukristo wako unakusaidiaje kama huwezi kukaa na kuomba au kujipambanua mwenyewe.

Mganga hata siku moja hawezi kukusaidia maana yuko ktk ufalme huohuo.

Chakufanya: nguvu ya uponyaji wa mkeo ipo ndani yako maana nyie ni mwili mmoja hata kama mkeo anamaagano ya aina gani. Amua kumuita Yesu ili akusaidie kwa kuomba na ikiwezekana okoka au tafta watu wa kukuongoza kuokoka. Huwezi kuwa unaenda kwa walokole kutafta msaada tu ili upone baadae unarudia uozo wako.

Lazima uamue kukaa hukohuko na damu ya Yesu itakusaidia hautapata shida tena.

Najua umefungwa akili yako ili usijue cha kufanya. Lakini amua kuwa Yesu hata kwa uelewa wangu huu mdogo, nimeamua kuja kwako ili unisaidie ktk shida yangu, naye atakusaidia.

Uamuzi ni wako, kubaki na dini ili uendelee kuteseka au kuamua kuokoka ili upone.
 
Imani ina nguvu ya kuhamisha hata milima. Kama anaamini anaweza kupona na Aombe Mungu huku akiamini na atapona tu
 
Uganga hautibiwi kwa uganga au niseme pepo hatolewi kwa pepo

Nenda kwa YESU ndio suluhisho la matatizo yenu
mkuu ila kuna siku nilikua nazungumza na dada mmoja akasema kilaa kitu kinachanzo aliemuingizia pepo ana lqke uenda either mama au huyo dada alishamfanyia mtu kisanga huko awali lazima familia ijitathimini kuna mahali tu ilikosea

uwezi pata mapepo from no where lazima kuna chanzo na tatizo ni either wife au familia ya wife wa jamaa

sawa yesu yupo na mambo ya namna hiyo lakini kama ulikosea mwanzo lazima uombe msamaha ndo ujikabidhi kwa yesu if you believe so vinginevyo YANrudiii
 
Umesema hukuwahi kuwa mlokole, ila ulivosema Yesu nisaidie alikuachia.

Hujajua kama hiyo ndio solution? Tatizo lako hutaki kuokoka. Mapepo siku zote ukimtaja Yesu huwa yanakimbia. Sijui huo ukristo wako unakusaidiaje kama huwezi kukaa na kuomba au kujipambanua mwenyewe.

Mganga hata siku moja hawezi kukusaidia maana yuko ktk ufalme huohuo.

Chakufanya: nguvu ya uponyaji wa mkeo ipo ndani yako maana nyie ni mwili mmoja hata kama mkeo anamaagano ya aina gani. Amua kumuita Yesu ili akusaidie kwa kuomba na ikiwezekana okoka au tafta watu wa kukuongoza kuokoka. Huwezi kuwa unaenda kwa walokole kutafta msaada tu ili upone baadae unarudia uozo wako.

Lazima uamue kukaa hukohuko na damu ya Yesu itakusaidia hautapata shida tena.

Najua umefungwa akili yako ili usijue cha kufanya. Lakini amua kuwa Yesu hata kwa uelewa wangu huu mdogo, nimeamua kuja kwako ili unisaidie ktk shida yangu, naye atakusaidia.

Uamuzi ni wako, kubaki na dini ili uendelee kuteseka au kuamua kuokoka ili upone.
kabla yq kufikiria kwenda kwa yesu lazima atizame nyuma kilikua nini kuna jambo huko nyuma sio bure
 
Tatizo ni moja tu,huna imani na kile unachokitegemea,ulianza kwenda makanisan ila ulipoacha nayo huwa yanarudi kwa kasi sana,sasa wewe ukaenda kwa waganga tena...amini katika mungu kisha okoka kweli kweli
 
Back
Top Bottom