Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Mke wa Lowassa azindua kitabu
Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.
Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.
Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo, alisema.
Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.
Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.