Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni

Hata kama ni mtazamo wako basi ni potofu,
Umepata wapi mamlaka ya kutoa hukumu hii?
aliyekuambia CCM mbaya ni nani? sera zao ni nzuri tu,kama hujui Nyerere alikuwa CCM! Nani aliyekuambia CHADEMA mbaya au nzuri? CHADEMA nzuri pia sera zao nzuri!

Hayo ya CCM au CHADEMA kuwa mbaya au nzuri umeyasema wewe, mie sijatamka hayo

Vyama vyote vinaharibiwa na wale kupe watu/mafisadi,kama huko in either chama na bado ukafanya kizuri whats wrong with that?
I never said anything against that!
Vipi kama Slaa alipokuwa CCM walijua siyo fisadi kama wao? na akaona kuliokoa taifa aende CHADEMA?
Kina nani walijua? Wewe una uhakika kilichompeleka Dr Slaa CHADEMA ni kupambana na ufisadi? Wakati alipoingia CHADEMA, kulikuwa na habari ya ufisadi gani iliyomkimbizia huko. Suala la ufisadi lililompa umaarufu Dr Slaa limetokea akiwa mbunge tayari, na hii ni sifa tofauti haihusiani na kuhama chama. Una uhakika kama angekuwa mbunge wa CCM asingepinga ufisadi?
Is CCM standard au benchmark kuwa kila anayehama ni mbaya au ana malengo ya ubinafis.
Malengo binafsi huwa yanatimizwa popote ambapo mhusika anaona kuna nafasi hiyo, ndani ama nje ya CCM, ndani ama nje ya siasa. Dr Slaa hajapungukiwa ubinadamu hadi akose kuwa na malengo binafsi.
Yes ni mtazamo wako ila uko wrong! think again, ulishachemsha tangu post ya kwanza , ADMIT IT..

waberoya
Again, who are you to deliver such a verdict, and on what basis? So any opinion that differs from yours is wrong?
 
Kwenye tovuti ya CHADEMA kuna ujumbe kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale, wa chama kilekile, chenye uoza uleule, wakiendeleza yaleyale kwa ari, nguvu na kasi mpya. Binafsi naichukulia hii kama moja ya njia zinazotumiwa na chama kuuelimisha umma juu ya uoza wa CCM. Kiongozi shurti awe kioo. Kama Dr anasimama jukwaani kutuhimiza kuwaunga mkono kwa kuwa CCM inaendeleza uoza huku akishindwa kumshawishi mkewe binafsi naona kama kuna tatizo. Call it democracy or anything !

Gaga una mashida makubwa sana mkuu .Kwa mfano kama Slaa mke wake angelikuwa Muislam na yeye Mkristo na wameamua kuishi kwa imani zao zilivyo na bado Slaa akawa mchungaji mkristo ana hubiri Ukristo ungalisemaje ?

Swala lao la msingi ni ndoa ambayo ina kanuni moja kwamba Slaa ni dume na Mume wake na yule ni Mke now imani zao katika vyama is not an issue to me .Leo Rose Slaa anatoboa juu ya wizi wa CCM huko waliko na ndani ya CCM the same thing being done by Slaa , nina amini kwamba wangalikuwa wote CCM nia ile ile njema ya kuwatetea Watanzania wa Jimbo lao na kata yao na Watanzania wote kupitia Bunge ingalifanyika .
 
Kweli halifichiki pembe la ng'ombe.... Mrs Slaa ni msanii wa nguvu sawa na mumewe .....
 
Kiongozi shurti awe kioo. Kama Dr anasimama jukwaani kutuhimiza kuwaunga mkono kwa kuwa CCM inaendeleza uoza huku akishindwa kumshawishi mkewe binafsi naona kama kuna tatizo. Call it democracy or anything !

Kuna tatizo kwa base ipi hiyo, maana sio kisheria sasa on what base?
 
Mkuu FMES,
Tatizo lililopo ni la kisiasa kwani mke wake anakuwa sehemu ya mafisadi walewale kulingana na kaulimbiu ya chama.
 
Tatizo lililopo ni la kisiasa kwani mke wake anakuwa sehemu ya mafisadi walewale kulingana na kaulimbiu ya chama.

Mkuu Gee,

Ni kwamba sio wanachama wote wa CCM ni mafisadi, na sio kwamba viongozi wote wa CCM ni mafisadi kuna baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao ni mafisadi. Kauli mbiu ya chama chochote cha siasa Tanzania, sio lazima iwe ni ukweli wa siasa wa taifa, ni kauli mbiu tu ya kile chama cha siasa,

kama kuna tatizo lingine la DR. Slaa na mkewe, lisemwe tu tujue lakini hatuwezi kujificha nyuma ya a couple kua na itikadi tofauti kama kigezo cha uaminifu wao kwa vyama vyao vya siasa na taifa, au kwa sisi wananchi, that is asking for too much kutoka kwa wananchi kama sio viongozi.
 
Wananchi itabidi wapigwe msasa kuhusu Partisan na Bi Partisanships...
 
Mushi,
Hilo zoezi la kutupiga msasa kwa Bongo linaweza kuwa gumu kuliko unavyofikiri.
 
1. Dr. Slaa & Mrs.; siasa ndani ya familia ni ajira,
Mkuu haya maneno yanaweza kuwa na ukweli, iwapo utathibitisha hapa kuwa kabla ya kuwa mbunge, Dr. Slaa alikuwa hana kazi yoyote, lakini kama alikuwa nayo basi hii kauli unahitaji kuifuta, maana ni kumpaka matope Dr. Slaa bila sababu ya msingi politically au iwe personally!

Mkuu FEMS,
Sidhani siasa kuifanya iwe ajira ni jambo baya au ni kwa vile mtu hana ajira nyingine. La hasha, ni uamuzi tu anapoona kuwa siasa ni ajira bora zaidi kuliko nyingine. Pengine ni kwa kupenda kuihudumia jamii au ni kwa maslahi binafsi. Lakini kilicho wazi hapa ni kuwa wote, Dr. & Mrs. Slaa wameamua kuacha mengine yote, including utumishi kanisani, na kuifanya siasa iwe ndio ajira yao kuu.

2. Dr. Slaa upinzani wake kwa CCM umetokana na hasira ya kunyimwa nafasi ya uongozi ndani ya CCM na si wa kiitikadi.
Yaani unasema sisi wananchi tuache kutafuta njia za kuyasaidia majimbo yetu kwa kuwazikiliza baadhi ya viongozi mafisadi wa CCM?

Chama ni ideology, kwa hiyo kabla ya Dr. Slaa kunyimwa nafasi CCM, ina maana alikuwa hakubaliani na siasa za CHADEMA. Kwa hiyo kwa yeye kujiunga CHADEMA ni reaction ya yaliyomkuta CCM na sio kuwa alishabihiana na agenda za Chadema. Alifanya jambo zuri kwani alielewa walichotaka wananchi, lakini haukuwa uamuzi wa kiitikadi.

4.Dr. Slaa kiongozi ndani ya CHADEMA ambaye anakubaliana na m'kiti wake 100% bila kuangalia maslahi ya chama na hivyo kutokusaidia chama kuepuka migogoro.
Migogoro ya siasa ipo katika kila chama cha siasa dunaini haikwepeki, na ndio demokrasia yenyewe, sio kwamba viongozi wa chama cha siasa lazima wakubali tu kila wanachoambiwa na wengine,

Kwenye migogoro ndani ya vyama itategemea uko upande gani. Kama yupo katika upande wa kuiminya demokrasia, kama walivyofanya walipomsimamisha marehemu Wangwe uongozi, basi kuna haki ya kuwajibishwa na wanachama na wapigakura wake.
 
hapa kwa kweli hatumsaidi Dr. Slaa na anything kama hii ishu, ila ninaamini tumefikia mahali tuna-abuse tu kuwepo kwake hapa JF.

Infact recently tumenza kushindwa kuitumia nafasi ya DR. slaa kisiasa na kuwepo kwake hapa na tumeanza kuitumia nafasi yake na kuwepo kwake hapa kama adhabu kwake

Mkuu FMES,
Kwanza naomba tuondoe mawazo ya kuwa, mwanasiasa anapodadisiwa ni sawa na kum-abuse. Ni muhimu tukadadisi yote yaliyopo machoni petu ili watakapofanya maamuzi tuwe tunaelewa ni hisia zipi zilizowapeleka kwenye hayo waliyoamua. Dr.Slaa sidhani kama alikuja humu mtandaoni kuhubiri tu na sisi tuwe wasikilizaji. Tupo wengi wenye mawazo tofauti naye ambao tungependa ayasikie hata kama yatakuwa yanamhusu yeye binafsi. Naomba tuachane na mawazo kuwa kwa vile yupo humu, basi awe immune from critisism.

Ni vizuri tunapompa zana za kufanyia kazi yake bungeni, majukwaani n.k., lakini pia tumuweke kiti moto kwa yale yanayomhusu. He is still a political figure just like JK, Lowassa, Mtikila etc. Hatuhitaji atujibu tunapotohoa background yake na ya spouse wake, lakini tusiache kufanya hivyo katika jitihada zetu za kumuelewe vema, kwa vile tu ni mwenzetu humu JF.
 
Kithuku,

..kweli kabisa, Dr.Slaa ni msanii.

..hebu fikiria alivyokuwa akimuandama Sumaye kwa "kashfa" ya kukodisha shamba la eka 7 kibaigwa, wakati Mkapa na Yona wamejinyakulia kiwira.

..katika listi ya mafisadi hajamtaja mu-Iraqw mwenzake Dr.Idiris Rashidi[former governor wa BOT].

..upotevu wa fedha BOT ulianza wakati Dr.Rashidi akisimamia fungu la fedha za misaada toka Japan. kamati ya Bunge iliyoongozwa na Edward Ayila ilipendekeza Dr.Rashidi achukuliwe hatua kali.
 
Mkuu Gee,

Ni kwamba sio wanachama wote wa CCM ni mafisadi, na sio kwamba viongozi wote wa CCM ni mafisadi kuna baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao ni mafisadi. Kauli mbiu ya chama chochote cha siasa Tanzania, sio lazima iwe ni ukweli wa siasa wa taifa, ni kauli mbiu tu ya kile chama cha siasa,

kama kuna tatizo lingine la DR. Slaa na mkewe, lisemwe tu tujue lakini hatuwezi kujificha nyuma ya a couple kua na itikadi tofauti kama kigezo cha uaminifu wao kwa vyama vyao vya siasa na taifa, au kwa sisi wananchi, that is asking for too much kutoka kwa wananchi kama sio viongozi.

POINT of Wondering

Juzi ZITO kule tarime aliwataka wana taarime wasichague chama cha mafisadi CCM.
 
Umepata wapi mamlaka ya kutoa hukumu hii?

Again, who are you to deliver such a verdict, and on what basis? So any opinion that differs from yours is wrong?

Mamlala niliyotumia kutoa hukumu ni ile uliyoitumia kusema Slaa na mkewe ni wasanii..., Kutofautiana na mimi sio kuwa huko wrong, ila sitaweza kuacha kusema huko wrong, eti kwa sababu yeyote atakayesema huko wrong atakuwa kama analazimisha uwaze sawa na yeye.,I havent condemned you, I have criticised, sina mahakama wala jela ya kukuweka, hata ningekuwa navyo mtu kama wewe unatakiwakueleweshwa tu.Maana kama mpaka sasa huelewi ulipoanguka, jela haitakusaidia

Tangu nazaliwa hata leobinadamu amabo huwa wanakubali wamekosea ni wachache, hasa pale wanapofikiri wakiwazacho hakipingwi au kuwa challenged.unapouliza maswali maswali yote yanakuwa kama na wewe unalizwa the same na Slaa! umepata wapi mamlaka ya kuwaita wasanii.....

Pia nimeona hata unapomfumania mtu kwenye ugoni bado huwa wanajitetea, tena utetezi wao ni mzuri. Mafisadi,majambazi, wauaji wote mahakamani huwa hawakosi utetezi.

Yote katika yote 'message sent' haijalishi utatolea maelezo gani Narudia tena comment yako ya kwanza ulichemsha....., wanandoa kutofautiana katika itikadi ni kawaida siyo usanii.Kuna mke mshabiki wa YANGA mume SIMBA...., kuna mke Mkatoliki mume mwislamu...n.k wala sio wasanii....! are they?

Endelea kujitetea au kujibu post hii..., kwangu I am done with you, I am simply saying..Message sent,ukikubali sawa, ukikataa sawa pia.

waberoya
 
Dr. Slaa na CHADEMA sio the subject of the story. Huwezi kuanza story hivyo. Hata kama sio nia yenu, it smacks of male chauvinism and crummy journalism. Na mimi sikwenda hata darasa moja la Uandishi, kwa nini nyinyi wahariri hamuoni hivyo vitu?

mara zote tumekushauri do something about it; kama waandishi na wahariri hawafanyi vile unavyotaka wafanye show them the way. You tried, and you failed miserably. You have to appreciate what people do siyo kila wakati kuwa na hizi generalized kandialing? Mara waandishi mko hivi, mara vile. Kwanini wewe usioneshe mfano wa jinsi uandishi uwe. Of course utasema "sijasomea uandishi" so how do you know what is wrong unless you pretend to know how it ough to be?

Kwanini umtake Kuhani awe mwandishi? Yeye kuonyesha mfano ndiyo itasaidia vipi, mbona mifano ya kuigwa ipo mingi sana. Halafu vacuum ya critics itajazwa na nani? Unaweza ku-criticize kauli zake ukitaka; that way we will benefit.

"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.

Pengine kuna kitu huyu mama alitaka kutuambia. Hata mimi amenichanganya.

.
 
Nafurahi sana mada kama hii inapotokea JF kwa kuwa inatuwezesha wengi wetu wenye uchungu wa kweli kweli kuwagundua wanafiki kwenye hii vita ya mustakabhali wa taifa. Unaposukumwa na wito wa kuitendea mema nchi yako, bila shaka swala la chama linatakiwa lichukue nafasi ya pili. Mbunge ni mwakilishi na mteteaji wa wote bila kujali itikadi na kama hili lingezingatiwa, Tanzania tungekuwa tunapaa haswa.

Mtu akihamasika na akashawishika kuwa ana nia, sababu na nguvu za kuweza kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa uendeshaji wa nchi, anajiunga katika siasa. Hivi sasa sheria zetu tuliojiwekea wenyewe ni kuwa ili ugombee nafasi yoyote ya kisiasa lazima utokane na chama cha siasa. Sasa kama chama chako kimekunyima hii fursa kuna mawili - ujiunge na chama kingine ufanikishe malengo yako ama ubwage manyanga kama wengi wanavyofanya na ubaki tu mpiga debe.

Kwenye nchi zingine ungeweza kugombea kama mtu huru asiyefungamana na chama chochote na ukiwa na ushawishi wa kutosha utapeta tu. Tatizo la Tz ni kuwa mara nyingi hatuangalii uwezo wa mtu bali tunajali anatoka chama kipi na matokeo yake hatupati viongozi bora bali bora viongozi. What a shame !! Tunashindwa kuelewa kuwa hakuna chama chochote cha siasa kisichoitakia Tanzania mema kwenye malengo yake. Chama chenye viongozi wabovu huishia kutetea ufisadi kwa kuwa kinategemea ufisadi kubaki madarakani.

Adui mkubwa wa giza ni mwanga na kwa kuwa maovu mengi yanatendeka gizani, watu kama Mh. Dr. Slaa wanakuwa mwiba kwa ufisadi kwa sababu wanaleta mwanga. Kama matendo kama ya Dr. na Mama Slaa ni usanii sidhani kama huo mwanga ungemulika lakini tulio na macho tunauona ati. Si ajabu watakuwapo kundini wasiouona na hapa ndipo kuna usanii wa kweli kweli ama wamevaa vitambaa vyeusi usoni?
 
Utafanya kosa la karne kujaribu kumwamini MWASIASA anapoibua UOVU wa mwanasiasa mwenzake.

Pila utafanya kosa la karne kujaribu kuamini ama kumtafsri mtu kutokana na maandikp yake badala ya matendo.

Mimi ningekuomba unieleze ILANI ya hao wapiganaji iliyowaingiza 2005 bungeni ni mangapi wameyatekeleza waliyo waahadi wananchi ktk majimbo yao?
 
Siasa adilifu ni njia ya kupata ruhusa/ridhaa ya wananchi kutoa huduma kwa namna unayopenda au unayodhani utafaidisha wananchi na wewe pia.

ni sanaa, ni kipaji, ni utaalamu, ni imani nk.
LAkini kwa kuwa ni njia ya kutufikisha tunakotaka kwenda, then waacheni wawe wanasiasa wa chama chochote, mradi lengo ni kuhakikisha bajeti yetu inatumiwa kama ilivyopangwa. Isichotewe kwenye mifuko mingine.
Kama wanataka kuila, waombe hela ya kula wasisingizie hospitali halafu wakaila hiyo hela.
Sadakta muungwana.Hapa si suala la usani hapa ni fedha za wananchi zinatumikaje.Kama ni usanii basi usanii wa Dr Slaa na Mkwe ni mzuri .
 
Kakweli nimeshindwa kuona point ya msingi ya kumshambulia DR. slaa kwa sababu yeye na mkewe wana itikadi za siasa zinazotofautiana, naomba kunawa mikono hapa maana sioni elimu hapa zaidi tu ya ku-showoff.

Dr. Slaa naomba tu uelewe kuwa kuwa kuna tunaothamini uongozi wako shupavu usio yumba na wenye faida kubwa kwa taifa letu, hasa sisi wanyonge wa Tanzania, na Mungu akupe nguvu na maisha marefu zaidi uendelee hivyo hivyo bila kuyumba.

Ahsante Wakuu.
 
Nafurahi kwamba mkuu nawe pia umeona hili, hakuna kitu kama commitment kwa itikadi wanayodai kufuata katika vyama vyao, ni wajanja hawana tofauti na wacheza ngoma ambao wanaongeza manjonjo ya unenguzi kwa kufuata kelele za washangiliaji! JK, Slaa na mkewe, wote wasanii tu!

Sio kweli, wapo wanasiasa ambao ni committed kama Dr. Slaa, Hon. Zitto na the likes pia wapo wanasiasa ambao ni wasanii, wanajulikana hakuna haja ya kuwataja. Msanii anajulikana kwa maneno na matendo.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom