Mke kubadili jina la ukoo baada ya kuolewa!

tzjamani

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
995
30
WanaJF,

Nawatakia maandalizi mema ya V-Day. Naamini kila siku inatkiwa iwe ya kivalentine.

Ninatatizwa na suala tajwa hapo juu - Mke kubadili jina la ukoo(surname) baada ya kuolewa na kuchukua uko wa mumewe.

Kumekuwa na mabadiliko kwenye suala hili ...

1. wanawake wengine hawabadili kabisa yaani wanabaki na majina yao ya ukoo kama kabla hawajaolewa
2. wanawake wengine wanabadili kwa kuungisha majina yote mawili. mfano Mr. K. Ali ana mchumbia Miss. M. John baada ya kuolewa Mrs. L . John-Ali.
3. Wengine wanaachana na majina yao, kwa mfano wa 2. atakuwa anaitwa Mrs. M . Ali

1. Je kuna umuhimu gani wakubadili au kutobadili?
2. Madhara yake ni nini?
3. Historia yake ilianza lini na wapi?

Asanteni
 
kulikuwa na ulazima wa kuhusisha majina hayo ya makinda na r aziz?

kuwa heshima kidogo........
 
huwa sioni umuhimu wowote wa kuongeza jina la mtu nisiye na nasaba nae mbele yangu,labda kama nna mpango wa kuchukua mkopo ili unisaidie kulipa hahahahahaha
 
huwa sioni umuhimu wowote wa kuongeza jina la mtu nisiye na nasaba nae mbele yangu,labda kama nna mpango wa kuchukua mkopo ili unisaidie kulipa hahahahahaha

mhh we usiseme hivyoo

what if last name ya mumeo ni kikwete au nyerere?hutabadili?
 
Umuhimu wa kubadili ni kuungana kwa kuanzisha familia yenu.

HAkuna madhara kwani mkiachana ana weza kurudisha jina lake la zamani.
 
Kwangu mimi naona haina umuhimu na kuna baadhi ya kazi inabidi utumie jina lako kamili bila ya mume, na vile vile kuna baadhi ya kazi lazima ubebe jina la mume.
Binafsi sitabeba jina la mtu niliejuana nae ukubwani kisa cha kukana wazazi wangu ebo!
 
kubadili jina kwa mwanamke ni alama ya kwamba ameshaacha kwao na sasa ana-belong to her husband's clan.
Hiyo ni mila na desturi toka biblical times. Ni vizuri mwanamke akibadili surname, ila halazimishwi
 
!Nadhani kukubali kuolewa inatosha kutuunganisha!Jina langu ntabaki nalo kama atakavyobaki na lake!
 
nakwambia sibadili hata kama la Obama nini hao uliowaja,labda tu niwe nataka unilipie deni hapo ntabadili.

Mumeo kama mpenzi wako akiomba ubadili jina kwa nini umkatalie? Je una sababu zipi za kumwelewesha?
 
Kwangu mimi naona haina umuhimu na kuna baadhi ya kazi inabidi utumie jina lako kamili bila ya mume, na vile vile kuna baadhi ya kazi lazima ubebe jina la mume.
Binafsi sitabeba jina la mtu niliejuana nae ukubwani kisa cha kukana wazazi wangu ebo!

Kama unamopenda kweli akakuomba kwa nini usikubali? Mpe sababu zinazoeleweka si ugomvi.
Je uko tayari suala la jina liwafarakanishe mpaka kuvunjika kwa ndoa?
 
nakwambia sibadili hata kama la Obama nini hao uliowaja,labda tu niwe nataka unilipie deni hapo ntabadili.

Njemba nyingine hufurahia pale mke anapoamua kubadili jina. Ni katika kumfurahisha mwenzio na kuongeza ukaribu wenu. Kuna njemba nyingine hili la kukataa kubadili jina huwa ni issue kubwa sana.

Kwa wasomi huwa ni tatizo maana vyeti vyote vya shule hakuna jina la kiume! Italaozimu kuapa upya. Mambo ya passport etc..... Abaki na jina lake tu!
 
haya hii beijing sijui hatimayake nini kwahiyo kwa sababu ya kumjua ukubwani aiwezi kukusababisha utumie jina lake labda awe ana kulipia ada au mkopo siyo nzuri na wala siyo utu sasa where is the true love
 
Hii imetokana na kuingiliana kwa tamaduni.
Sisi waafrika zamani mtu akiolewa alibaki na majina yake, kwamfano Chausiku Malima, lakini ameolewa na John Masatu, Au Mkunde Msuya,lakini ameolewa na Kiolonzo Mshana.

Zilipokuja dini mambo yakabadilika. Watu wakawa wanaitwa Mrs William kwa sababu ameolewa na John William. Ndipo watu wakaanza kubadili majina. Maeneo ya pwani bado watu wanatumia majina yao, kwamfano Mwanaidi Salum takuwa anaitwa binti Salum kwa maana ya kuwa ni mtoto wa kike wa salum hata kama kaolewa na Rashid Mwinjuma.
Kinachonichekesha ni pale ninaposikia bibi wa miaka 97 akiitwa binti Ally, huwa naona kama imekaa kushoto, anyway lakini hio ni mtazamo wangu ambao haupaswi kuingilia tamaduni.
Kwahiyo basically hakuna matatizo ni chaguo la mtu
 
I think its people's own choice in life, I am one of those who use both 2 names,

I still have my father's name then put - and my husband's surname

I have a different view for if I cling to my father's name in the name of feminism, then I might as well resort to all my three maiden names b'coz my dad's name is a 'he' and in the spirit of feminism, I should be nsiande kyekue manka .....

It has always been that a male's name got to be at the end of your name, to complete it! Whether u r married or single , so adding an additional name for me doesn't flinch me in anyway!

That's my own views! I respect others too..
 
haya hii beijing sijui hatimayake nini kwahiyo kwa sababu ya kumjua ukubwani aiwezi kukusababisha utumie jina lake labda awe ana kulipia ada au mkopo siyo nzuri na wala siyo utu sasa where is the true love
Mi sioni kama ni matokeo ya Beijing..Ni utaratibu ambao mtu anajiwekea. Kwani akibadili jina ndo mapenzi yataongezeka?

Kila mtu abaki na jina lake tu.
 
I think its people's own choice in life, I am one of those who use both 2 names,

I still have my father's name then put - and my husband's surname

I have a different view for if I cling to my father's name in the name of feminism, then I might as well resort to all my three maiden names b'coz my dad's name is a 'he' and in the spirit of feminism, I should be nsiande kyekue manka .....

It has always been that a male's name got to be at the end of your name, to complete it! Whether u r married or single , so adding an additional name for me doesn't flinch me in anyway!

That's my own views! I respect others too..

good point of view
 
mi naona ni ushamba na ulimbukeni! Tuna mtu tunafanya nae kazi hapa tukiwa kwenye vkao au hata mahali panapohitaji utambulisho huinuka na kusema naitwa Mrs. Fulan bila hata kutaja jina lake la awali, hapo anapoumbuka kwa kuulizwa ndo jina uliloajiriwa nalo? Hapo huambiwa ajitambulishe upya kwa majina yanayo tambuliwa na waajiri! What a shame mbele za wa2! Nawashaur wanao yahusudu majina hayo wayatumie kwenye function hivi ambapo mara nying wanakuwa wameambatana na wenzi wao. Mapenzi huanza kwa kasi kwa mpenzi mpenzi na mwishowe huwa mshenz! Hapo kama umechange jina hadi kazn lol! Utaliona mzigo. Mim hata ingekuweje siwez change majina nlopewa na wazazi wangu, kwanza ni utumwa!
 
Nadhani huu ni utamaduni ulioambatana zaidi na hali ya 'protocal' kupitia wakubwa wetu nasi kuiga.
Kwa mujibu wa imaan yangu ya kiislamu...hairuhusiwi mume kumuoa mke halafu mke abadili jina lake na kuanza kutumia ubini wa mumewe, HAPANA HII.
Ila kwa hali ya kidunia iambatanayo na 'protocal'...hali hiyo hulazimika kuwa, ni mambo yasiyo na msingi saana katika uwili wa wanandoa. Fikiria; mkiachana basi tena ubini unakufa, lakini ubini wa baba haupotei hata kama ameshatoweka duniani.
 
Back
Top Bottom