Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,803
- 59,283
Lizzy nilipo oa nilimuomba mwenzangu abadili jina akagoma, nimuacha wala sikumlazimisha. Bahati nzuri nikapata kazi nje ya nchi akatakiwa aombe ruhusa ya kazini kwao ili aje anitembelee. Aliambiwa hujaolewa na kama umeolewa kwa nini unatumia jina hili? kama unataka ruhusa basi fanya utaratibu wa kubadili jina. Ilibidi aombe kubadilisha jina. Akapewa ruhusa. Alipofika huku ilibidi nimuombee health insurance akaambiwa utafuata jina la mumeo hata kama kwenye passport yako unatumia la baba yako maana ndiye anakatwa kwenye mshahara wake. Pia kazini kwangu nilipowasilisha document zake za kumuongeza kama dependant wangu walikataa kusajili jina lake. Ikabidi tutumie la kwangu ndiyo mambo yaende sawa kwa ujumla ulikuwa sumbufu moja kwa moja. Yeye mwenyewe alikili kuwa alilazimisha kitu bila kujua madhala yake. Kwa Ushauri tuu LIZZY jaribu kuwa mpole.
Mhhhh sijawahi kuona au kusikia usumbufu wa aina hiyo kwasababu tu mtu anatumia jina lake badala ya la mume!!Kwani hamna vyeti vya kuonyesha kwamba kweli mmeona???Sijui mtu akiolewa zaidi ya mara moja atabadili jina mara ngapi!!!