Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Mimi ni kama mkimbizi nyumbani kwangu. Kabla ya kuoa, nyumbani kwangu kulikuwa ndio kimbilio baada ya mihaingaiko yangu ya kutwa nzima, lakini tangu nimuoe mke wangu huyu ambaye nimedumu naye kwa miaka mitano sasa, nimejikuta nikiwa ni mkimbizi kwenye nyumba yangu mwenyewe. Ndivyo alivyoanza simulizi yake rafiki yangu huyu maarufu kwa jina la Udandala.
Mke wangu ni mama wa nyumbani na ili tusaidiane katika kuyakabili maisha, niliamua kumfungulia duka ili aweze kujiajiri. Cha kushangaza, pato halionekani na biashara haiongezeki, kila nikimdadisi sababu ya biashara kuzorota wakati nilimpa mtaji wa kutosha, yeye hukimbilia kuwalaumu majirani wanaoishi jirani na lilipo duka lake kuwa ni washirikina. Mke wangu huyu anapenda sana kutumia muda wake mwingi kunichunguza niko wapi, nafanya nini, na kwa nini, mpaka nakereka kwa kweli. Nikiacha simu mezani, ataichukuwa na kuibofyabofya na kusoma meseji zote na kupekua phonebook ilikuchunguzaina namba gani zenye jina la jinsia ya kike na kuzikariri (ni mzuri wa kukariri namba usipime) na kuwapigia kwa minajili ya kuwaanzishia ugomvi, wakati mwingine hutumia njia za ki-intelijensia ili kujua wanapokaa au wanapofanya kazi na akishajua huwafuata huko huko na kulianzisha.
Nikienda naye matembezini, kila msichana tutakayepishana naye atamtoa kasoro, na kama ni kwenye Mghahawa au Bar basi atawatoa kasoro wahudumu wote watakaotuhudumia. Kama msichana yeyote anatokea kuniangalia ndiyo inakuwa balaa, maana ugomvi utaanzia hapo kwa maswali ya ajabu-ajabu kama, ‘kwa nini yule msichana anakuangalia sana?' Mimi nakosa jibu, kwa sababu siwezi kujua sababu ya mtu mwingine kuniangalia. Kwa tabia hiyo, mara nyingi tunajikuta tukiwa na malumbano yasiyoisha, badala ya kujadili juu ya maisha yetu na familia yetu au namna ya kuongeza kipato katika familia. Kwa upande wa kipato ninachopata hata hakitoshi kuweka akiba maana mwenzangu bajeti zake ni za juu sana. Hata kama kila kitu kipo ndani lakini matumizi yetu yanafikia kiasi cha elfu 20 kwa mlo wa siku. Ingawa tupo sita ndani ya nyumba, yaani mimi, yeye, msichana wa kazi, mdogo wake na mke wangu (ambaye ameajiriwa hivi karibuni na hajaanza kujitegemea) na watoto wetu wawili wa miaka 7 na miaka 5, lakini mimi na mdogo wake hatuli pale nyumbani mchana kwa sababu tunaenda kazini. Hivi kweli nyumba zote zenye kipato cha kawaida inakuwa hivyo? Kama nikisafiri kikazi na kumuachia laki mbili, hata kama nitakaa kwa siku tano tu, nikirudi nnitaambiwa hela zimeisha na alikuwa anakopa dukani kwake, na hilo deni nitatakiwa kulilipa.
Anapenda watoto waende shule zenye kuibuka kama uyoga kwa kufuata uzuri wa majengo na zenye majina ya saint... Mtakatifu... English Medium... Academic School bila hata kuangalia pato letu kama linakidhi hayo matumizi. Kwa mfano huyu mwenetu wa kwanza kwa miaka miwili tu ameshamhamisha shule takriban tatu akisingizia kuwa walimu hawajui kufundisha, ha uhamisho huo mara zote unanighrimu, lakini mwenzangu wala hajali.Kitu kingine anachonikera zaidi ni kunilinganisha na watu au ndugu anaowafahamu... ‘Ona mwenzako fulani amejenga nyumba kubwa kama nini.' au 'Ona fulani amenunua GX100 mpya kabisa tena kaagiza Japan, lakini wewe umezubaa tu.' Wakati yeye ananilinganisha, lakini tangu nimfungulie hiyo biashara hajawahi hata siku moja kuchangia chochote pale nyumbani zaidi ya kunitaka nimuongeze mtaji kila mwenzi.
Anashindwa na huyu mdogo wake tunayeishi naye, ni binti mdogo kabisa, lakini kila akipata mshahara anachangia kwa kununua mahitaji ya pale nyumbani, ingawa huwa sipendi afanye hivyo. Huyu mke wangu hajawahi kuwanunulia watoto hata leso au soksi lakini kazi yake ni kunilaumu kila uchao. Kama nikimuhoji kwamba yeye anachangia nini katika familia ananikata kalma na kudai kwamba yeye ni mwanamke na hapaswi kufanya hivyo. Anaenda mbali zaidi na kudai kwamba hata vitabu vya dini vinasema, mwanaume atakula kwa jasho lake na mwanamke atazaa kwa uchungu, ambapo tayari alishatekeleza jukumu lake la kunizalia kwa uchungu watoto wawili, na sasa ni jukumu langu kuhakikisha familia inapata mkate wa kila siku, yeye haimhusu. Kinachonishangaza, yeye anawaita wanawake wengine wasiiolewa kuwa ni Malaya, machangudoa, wachuna buzi, eti ni wawindaji wa waume za watu, ila yeye ni mke mwema kwa mumewe, Hivi waume za watu ndio wakuteswa kwenye ndoa zao wenyewe!? Hivi mapenzi ya kweli ni yapi katika ndoa? Hebu niambie Mzee Mtambuzi, hivi kweli naweza kujivunia ndoa hii yenye mashaka makubwa kiasi hiki?
Hebu wana JF fungukeni hapa, nimshauri nini huyu mwenzetu mbaye ndoa yake inaonekana kumuelemea?