Mke atuhumiwa kumpiga mumewe kwa rungu na kupelekea kifo chake

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja Mkoani Iringa amempiga na rungu mumewe hadi kupelekea kifo baada ya kuwepo kwa ugomvi kati yao.

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limethibitisha kumshikilia mwanamke aitwaye Aurelia Kalolo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 kwa kosa la kumpiga kichwani kwa kutumia rungu mumewe, Williad Ngamema ambaye ni Balozi wa Kitongoji cha Iwengi Kijiji cha Ukumbi, Kata ya Ukumbi na kumsababishia kifo.
View attachment 2749055
View attachment 2749056
Baadhi ya ndugu jamaa pamoja na majirani ambapo wamesema kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara kati ya wawili hao na siku ya tukio walikuwa na ugomvi tangu asubuhi ambapo jirani mmoja alipita nyumbani na kukuta wanagombana huku mke akiwa ameshika rungu hivyo akawasuluhisha na mwananke akaondoka na kwenda klabu inayouza pombe aliporudi nyumbani usiku ugomvi uliendelea na akampiga mumewe kwa rungu hadi kufariki.”

Mtendaji wa kijiji hiko cha Ukumbi Mariam Kaduma amesema alipatiwa taarifa saa tisa usiku na alipofika nyumbani kwa wanafamilia hao alikuta mume amefariki hivyo akamshikilia mwanamke huyo na kupiga simu polisi ambao walifika na kumkamata na upelelezi unaendelea.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Lazaro Nyamoga amefika pia msibani na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na familia ambapo amesema balozi huyo ndiye alikiwa anategemewa na familia.

Chanzo: JAMBO TV
Kinachowatesa watu wa Iringa ni pombe na ulevi uliopitiliza.
 
Siku hizi wamekua wababe sana
FB_IMG_1664957154217.jpg
 
Wakinamama wamekuwa wakatili sana Marne hi,hi inanikumbusha kitendo cha jamaa angu kuchomwa kisu na mkewe kifuani akiwa amelalaa,na mwanamke kutokomea almanusra tumpoteze
 
Sema kama amemkung'uta rungu Moja huyo gerezan hata mwaka hakai atatolewa ,coz itasomeka ameua bila kukusudia.

Ila kama amemtia zaidi ya rungu mbili means huyo jera maisha
Ko mkuu unamaanisha tukitaka kuua tupige rungu moja la uhakika 🤔
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja Mkoani Iringa amempiga na rungu mumewe hadi kupelekea kifo baada ya kuwepo kwa ugomvi kati yao.

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limethibitisha kumshikilia mwanamke aitwaye Aurelia Kalolo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 kwa kosa la kumpiga kichwani kwa kutumia rungu mumewe, Williad Ngamema ambaye ni Balozi wa Kitongoji cha Iwengi Kijiji cha Ukumbi, Kata ya Ukumbi na kumsababishia kifo.
View attachment 2749055
View attachment 2749056
Baadhi ya ndugu jamaa pamoja na majirani ambapo wamesema kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara kati ya wawili hao na siku ya tukio walikuwa na ugomvi tangu asubuhi ambapo jirani mmoja alipita nyumbani na kukuta wanagombana huku mke akiwa ameshika rungu hivyo akawasuluhisha na mwananke akaondoka na kwenda klabu inayouza pombe aliporudi nyumbani usiku ugomvi uliendelea na akampiga mumewe kwa rungu hadi kufariki.”

Mtendaji wa kijiji hiko cha Ukumbi Mariam Kaduma amesema alipatiwa taarifa saa tisa usiku na alipofika nyumbani kwa wanafamilia hao alikuta mume amefariki hivyo akamshikilia mwanamke huyo na kupiga simu polisi ambao walifika na kumkamata na upelelezi unaendelea.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Lazaro Nyamoga amefika pia msibani na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na familia ambapo amesema balozi huyo ndiye alikiwa anategemewa na familia.

Chanzo: JAMBO TV
Ulanzi si pombe nzuri.
 
Wakinamama wamekuwa wakatili sana Marne hi,hi inanikumbusha kitendo cha jamaa angu kuchomwa kisu na mkewe kifuani akiwa amelalaa,na mwanamke kutokomea almanusra tumpoteze
Kibao kimegeuka rafiki.
 
Back
Top Bottom