Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.
Wananchi wa nchi hii wamezoea, kwamba hawawezi kumwajibisha kiongozi huyo kwa njia yoyote ile; na Bunge ambalo sheria inaruhusu kumwajibisha jinsi wawakilishi wa Bunge hilo wanavyopatikana kwa fadhira za mtu huyo huyo mmoja (Rais), halina uwezo wa kumwajibisha mtu huyu.
Bila shaka yoyote, Rais wetu Samia yote haya aliyajua, na hasa baada ya kuona ni namna gani mtangulizi wake alivyokanyaga kila kitu kutimiza matakwa yake.
Kwa hiyo Samia hakuwa na hana hofu yoyote juu ya kufanya aliyonuia kuyafanya siku nyingi, kama angepata fursa hiyo ya kuyafanya
Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote
Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.
Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu. Nitaorodhesha mambo aliyoyafanya au kutoyafanya ili kufanikisha IGA hii iliyoletwa kwetu ifanikiwe. Kumbuka wakati wote, yeye anajua hakuna lolote wananchi wanaloweza kufanya kumzuia au kumuwajibisha sasa au baadae.
1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.
2. Kufanya viini macho ili kupoteza lengo.
Paliwahi kuwepo mjadala wa kufufua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na yeye Rais aliwahi kueleza kuwa kuna timu ya majadiliano na waChina. Hili halikufika mbali, kabla ya kugeukia kwenye ujenzi wa hatua za mwanzo sisi wenyewe.
Wakati haya yakiendelea, imebainika sasa kwamba DPWorld tayari walikuwa kwenye kibarua cha kutengeneza IGA na wataalam wetu hapa ambao haijulikani walipatikana kwa mpango upi kushughulikia kazi hiyo. Bila shaka ni sahihi pia kusema kuwa ni watu walioaminiwa kutengeneza kitu alichokitaka mteuzi wao kwenye nafasi hiyo.
3. TICTS - abaki/asibaki? moja ya viini macho kuzuga watu, bila shaka hata wao TICTS hawakujua hatma yao itakuwa vipi. Wakati wote huu wa sintofahamu, DP World na wataalam wetu wapo kazini wakisuka IGA ya kutukomesha sisi.
4. Mara BUUUUU! DP World anaingia kwa kishindo kikubwa. Sasa ndipo watu wanaanza kuunganisha doti
Bendera yetu na picha ya Rais wetu juu ya jengo refu kabisa duniani; mara fununu za viongozi kwenda kwenye EXPO Dubai kimya kimya na Rais kukaa huko kwa siri kubwa, kumbe anatia saini mkataba wa kutuuza!
5. Mkataba unavujishwa? Juhudi kubwa zinaanza kufukia mahandaki. Hapana, huo siyo Mkataba, hayo ni "Makubaliano tu, ikiambatana na upotoshaji mwingi mwingine, toka kwa waziri na mtu mwingine aliyeaminiwa sana kusimamia kujua kilichomo ndani ya Mkataba/Makubaliano" hayo. Mtaalam wa sheria mbobezi (tunaambiwa), Hamza Johari ndiye mkuu wa timu. Watu wanajiuliza, na Mwanasheria mkuu wa Serikali alishiriki vipi hadi kufika kwenye hatua hii?
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa". Hakuna anayejua kiwango cha ushiriki wake kwenye mkataba huo, na kama yeye, kwa nafasi yake anakubaliana na yaliyomo kwenye mkataba. Sijasikia akisema lolote juu ya hayo.
6. Taratibu na Hatua sahihi za kuingia mikataba kama huu (IGA) - Je, sisi kama taifa tunao utaratibu wowote tuliojiwekea wa kuingia kwenye mikataba kama hii? Huu siyo mkataba wa kwanza Tanzania iliouingia, je hiyo mingine kulifanyika mambo gani ambayo yamezoeleka kufanywa, lakini safari hii ikawa ni tofauti?
Hili ni swali lililo wazi, kama kuna utaratibu maalum, je ulifuatwa, hata kwa kiasi fulani tu?
jambo la kwanza linaloniingia akilini ni "Vikao vya Baraza la Mawaziri". Kwa mtizamo wangu, jambo kubwa kama hili haliwezi kufanyika bila ya uwepo wa angalao kikao cha Mawaziri kulijadili..
Vikao hivi vya Baraza la Mawaziri siku hizi vimekuwa kama ni siri kubwa sana, hata kule kutaja tu kulikuwepo na kikao siku hizi ni nadra sana, hata bila ya kutaja yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kwa hiyo hili ni swali tu kuuliza kama kulikuwa na kikao cha kujadili, au kujulishwa tu kwamba kuna mpango wa ujio wa DP World na hatua zilizokuwa zikifanyika kuwakaribisha hapa.
Kama Mawaziri nao hawakuwa na habari, hilo litakuwa jambo la kushangaza sana linaloongeza uzito katika hoja za andiko hili.
7. Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..
a) Kundi la wabunge lililopelekwa Dubai, ni utaratibu upi uliotumika kuwachagua hao waliokwenda? Wanazo sifa maalum ambazo zingewawezesha kutambua mambo ambayo hayana manufaa kwetu?
b) Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyeti katika kazi wanayokwenda kuifanya huko walikokwenda? Walipewa Mkataba wausome wajue yaliyomo kabla hawajaondoka hapa?
Hawa wabunge ni akina nani hasa?
Kama maswali yote haya hayana majibu, maana yake ni kwamba hii ilikuwa ni mbinu tu, iliyotegeshwa kuhalalisha maovu juu ya nchi yetu, maovu waliyoyajua walioandaa mkataba huo na washirika wao wote.
c) Bungeni wakati wa kikao cha Bunge, ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo kwa wabunge hao maalum? Hawa wabunge walijua kilichokuwemo kwenye huo Mkataba? Mbona hta mmoja wao hakujitokeza na anagalao kutaja tu hata kifungu kimoja alichokuwa nacho mashaka? Hawa wote waliandaliwa kwa maksudi kwa ushirikiano na uongozi wa Bunge?
d) Ushirikiwa wananchi, wanapewa masaa 24 kuleta maoni yao. Maana ya hili ni kwamba hapakutakiwa kuwepo na mchango wa wananchi ili lengo la kuhujumu nchi litekelezwe.
DPWorld wanao uzoefu mkubwa sana katika maswala haya ya Mikataba, kwa sababu kila sehemu walikokwenda wamekutana na chngamoto chungu nzima zilizowakabili.
Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao. Mkuu wetu hana uzoefu wowote, na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye, ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.
Hapa ndipo tulipofikia sasa hivi.
Ingekuwa ni nchi nyingine, Mkataba huu usingemwacha huyu mkuu abaki salama, tena akiendelea kwenye madaraka yake kana kwamba hakuna lolote lililofanyika.
Lakini hii ni Tanzania. Yeye kishasema "Ameziba masikio", wenye kupiga kelele wapige kelele hadi wachoke wenyewe; lakini DP World hakuna wa kumzuia kuja hapa.
SAWA.
Sasa tumebaki na moja tu tunaloweza kulitegemea kuondokana na hujuma hii juu ya nchi yetu.
Je, tunaweza kumpata kichaa mwingine (bila ya baadhi ya mambo ya aliyetangulia mbele ya safari) atuondolee uchafu huu ndani ya nchi yetu? (Bila kujali hasara tutakayoingia kwa kuvunja mkataba (kwani kuendelea na mkataba wa aina hii ni hasara kubwa zaidi ya kulipa hiyo fidia tutakayodaiwa).
Na kwa kuwa ni 'kichaa', bila shaka baadhi ya hawa wahujumu watachukuliwa hatua bila ya kuwaonea aibu.
IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania.
N.B. Sikutegemea na wala siyo kawaida yangu kuandika gazeti, lakini leo acha iwe hivyo, kwani hakuna namna.
Samahani kwa makosa ya kiuandishi kama yamo kwenye andiko hili..