mkataba wa ajira

kekuwetu

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
327
98
jamani naomba kuuliza hivi kama mtu ameajiriwa na akasaini mkabata lakini hakupewa copy ya mkataba na mwajiri (mwajiri amebaki nayo) je anaweza kumdai mwajiri mkataba wake hata kama amefanya kazi kwa muda mrefu? je mwajiri akikataa ana haki ya kumshitaki?
 
Ndiyo:
(1). unaweza kumdai mwajiri mkataba wa kazi hata kama ni muda mrefu umepita bila we kuwa nao(pengine hukupewa kabisa mkataba wakati unaanza kazi au ulisaini mkataba lkn hukupewa nakala)
(2). Unaweza kumshitaki mwajiri kwa mamlaka husika (CMA au kuomba ushauri Idara ya Kazi) ukidai kupewa mkataba wako wa ajira (ukijikita kwenye applicationa and interpretation of the Law)
 
mkataba wa ajira ni haki yako. unahaki kupewa nakala baada ya kusaini mkataba wewe na mwajiri wako, na ikitokea hajakupatia pia unahaki kudai kopi for your reference purposes na pia kama itatokea mtafaruku wowote kati yenu uwe na written document zinazoonesha makubaliano yenu pamoja haki zako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom