Isaack Newton
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 535
- 224
Habarini wakuu!
Nimeleta suala hili kwenu wataalamu wa sheria ili mnisaidie.
Nafanya kazi kampuni fulani ambayo baada ya tamko la serikali kuhusu kuongezewa mishahara kwa sekta binafsi, kampuni imeshindwa kumudu hilo ongezeko la mishahara.
Mwajiri alichokisema ni kwamba yeye kashindwa kumudu kulipa huo mshahara mpya, sasa anachotaka kukifanya ni kwamba anasajili kampuni yake iwe kama local company na sio international company ili atulipe wafanyakazi kama local, sasa amesema sisi wenyewe TUSITISHE MKATABA.
Sasa je kisheria imekaaje, mtu unalazimishwa kuvunja mkataba afu usaini tena, kwa uelewa wangu mdogo ninaojua ni kwamba mwajiri ndo anisitishie mkataba maana mimi sijataka kusitisha mkataba. Wataalamu wa sheria za mikataba naomba msaada wenu.