Mkasa wa kweli: najuta kwenda honeymoon - nilichofanyiwa sitakuja kusahau

NAJUTA KWENDA HONEY MOON –NILICHOFANYIWA SITAKUJA KUSAHAU -05

Nusu saa mbele.Nikiwa peke yangu. Pale pale kwenye meza alitokea muhudumu wa ile Hotel. Alitembea kwa hofu. Aliangalia kushoto na kulia, ni kama hakutaka kuonwa . Alinisogelea na kuninongoneza.

“ Unaitwa chumba namba saba.Fanya haraka uende.” Aliniambia.

“ Nani ananiita?” Nilimuuliza.

Hakunijibu. Aligeuka na kuondoka kwa tahadhari kama mwanzo.

“ Mbona kama hataki kuonwa?.” Nilijiuliza.

“ Chumba namba saba..” Nilijikuta nimetamka. Ubongo wangu ulijiuliza ni nani wa kuniita chumba namba saba. Niliwaza na kuwazua sikupata majibu. Kwa mbali nilihisi uenda Sam ndiye aliyemtuma.

“ Atakuwa Sam kaniita, kwa yaliyotokea ukute hataki aonekana na Mimi, ndio mana kaniita kisiri .” Niliwaza.

Nilisimama na kuelekea ndani.

Nikiwa naelekea ndani niliangaza kila pande ya Hotel , Maeneo yote sikuwaona ndugu wa Sam.

“ Wameenda wapi?” Nilijiuliza.

Sikujali hilo. Moja kwa moja nilienda chumba namba saba. Niligonga mlango.

“ Karibuu….karibu sana Judy..” Alinikaribisha. Alikuwa Gaby. Kaka yake Sam.

“ Mmmmh! hapana shem. Kuwa chumbani wawili mbona sio sahihi.Naomba tuongelee kwenye korido.”

“ Lingekuwa swala la kuongelea kwenye korido nisingehangaika kukuita huku. Ningekuja pale pale mezani nikakuambia. Naomba ingia ndani. Wala usiwe na mashaka.” Aliniambia.

Niliingia na kwenda kukaa kwenye kiti .

“ Mbona umekaa mbali . Njoo ukae hapa.” Aliniambia.

Alinitaka nikakae kitandani.

“ Hapana. Hapa nilipokaa panatosha .” Nilimjibu.

Hakuongea. Alisimama na kunishika mkono. Alinivuta na kunikalisha kitandani.

“ Mmmmh!” Niliguna. Taa nyekundu iliwaka kichwani.

“ Mbona unaniangalia hivyo?” Aliniuliza .

“ Kunikarisha hapa sio busara. Mkeo au ndugu wengine wakija itakuwaje?” Nilimuuliza.

Badala ya kunijibu , alicheka.

“ Hakuna atakayefika hapa. Kuwa na amani. Jiachie na uwe huru.’ Aliniambia.

“ Mmmmh!”

“ Kuna jambo uliongea pale mezani limenipa shauku kidogo. Naomba nifafanulie vizuri. Umesema Baba mdogo alikuja chumbani kwenu na kumpiga vibao Mumeo?” Aliniuliza.

Swali lake liliufanya moyo wangu upate amani kidogo. “ Hatimaye nimepata mtu aliye tayari kunisikiliza.” Nilijisemea.

Nilimueleza tukio nzima.

“ Hii kali. Kwahiyo alikuwa anatokea gizani anampiga kibao kisha anapotea tena gizani?” Aliniuliza.

“ Ndio, ilikuwa hivyo, lakini mdogo wako alikuwa hafanyi lolote. Alikuwa anasema hajamuona.”

“ mmmmmh…” Aliguna.

“ Pole sanaaaa…” Aliniambia. Alinishika kwa nguvu na kunikumbatia. Nami nilimkumbatia. Nilijisikia faraja kumpata mtu wa kunisikiliza . Akiwa amenikumbtaia alianza kunipapasa mgongoni.

Akili yangu ilihama. Nilijisikia furaha kujaliwa. Nilijikuta nashindwa kumzuia, badala yake nami nilimpapasa. Tulipapasana kwa dakika kadhaa.

Muda ulivyoenda hisia zangu zilibadilika.Naye zilibadilika pia. Tulijikuta tunanyonyaa ndimi na kushikana maungo ya uzazi.

Alininyanyua na kunilaza kitandani. Ajabu. Sikuwa mbishi wala sikuwaza kuhusu kinachotokea. Aliendelea kushika maungo yangu na kunichombeza sehemu mbali mbali za mwili wangu. Alinivua nguo, nami nilimvua zake.

“ Subiri kwanza..” Aliniambia.

Alishuka kitandani na kuvaa nguo zake. Alifungua mlango na kutoka nje. Aliniacha nikiwa nimeduwaa.

“ Hii inamaana gani? Au alikuwa ananijaribu?” Nilijiuliza.

“ Hapana.” Nilitamka.

“ Huu mtego.” Niliwaza.

“ Lakini mtego gani wa kufanyiwa honeymoon?” Nilijiuliza.

“ Vyovyote vile. Dawa ni kuondoka humu ndani.” Nilijisemea.

Nilishuka kitandani na kuzifata nguo zangu. Nilizivaaa. Nilisogea mlangoni na kufungua mlango. Nilichungulia nje. Macho yangu yalikutana na macho ya Sam.
Nakuja
Mbona kimya mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom