Mkapa awaliza wanakijiji Lushoto

Mina shauri hao wanakijiji wajichangishe watafute wakili wampeleke mkapa mahakamani!

Mahakama ipi hiyo? Kungekuwa na mahakama na sheria zinazotekelezwa Tanzania ungekuta Mkapa yuko Jela au nje kwa dhamana akisubiri hukumu kwa kesi zake za kuiuza nchi kwa wawekezaji uchwara, yeye mwenyewe na familia na marafiki wakiwa miongoni mwa wachwara hao.

Sitamsahau mkapa kwa kujidai kubinafsisha mashirika ya umma yote, hata yale ambayo yalihitaji tu kubadilisha uongozi (managament contract). Alifanya hivyo kwa kuwa mengi ya mashirika alifaidika nayo kwa ile 10% au kupewa vitega uchumi. Hivi ni nani anakumbuka lile panga or something of that nature cha dhahabu alikadidhiwa na kampuni moja ya madini?? Je aliliacha Ikulu kama mali ya serikali/archive au ni lake?? Aliye na zile picha za hongo/rushwa ile adondoshe hapa maana ilikuwa open na media ilirusha. sitakusahau kwa ufisadi wako wa kinafiki wewe mkaa kanisani kiti cha mbele wakati hata ndoa na familia imara huna.
 
Vangi,
Ni kweli tumesahau. Lakini nakuhakikishia hatutasahau jinsi alivyoanzisha biashara akiwa Ikulu. Hatutasahau jinsi alivyouza NBC kwa bei chee kwa Makaburu kwa kupewa kitita cha hongo. Hatutasahau jinsi alivyojimegea mgodi wa Kawira. Hatutasahau jinsi alivyoingiza kampuni ya ndugu zake kwa mabavu ya Ikulu kutusimamia TANESCO. Hatutasahau jinsi alivyojinunulia dege la fahari kwa hela zilizojaa rushwa. Hatutasahau jinsi alivyotuwekea mazingira ya kumpata Kikwete kuwa rais wetu mpya. Hatutasahau, na ukitaka ninaweza kuendelea tena na tena........

Hilo dege alilojinunulia aliondoka nalo?
 
Tusiwe kama "machizi" chini ya ubepari Mkapa hajafanya kosa,halafu keshasema mwenyewe tatizo ni maadili ya uongozi kupewa kipaumbele,hapo inaonyesha ni kwajinsi gani viongozi wetu wametofautiana na wananchi,vigezo vya kumchagua rais ndivyo sivyo,nandio maana tukishampata rais tunashangazwa na madudu,hatupimi,tunaangalia tu kama ni CCM haya twende,bado tu mentality kama ya enzi za mwalimu kuona upande ambao ni tofauti na CCM ni "kivuli"
Hadi hapo tutakapopata kiongozi atakeyesema sasa hii ndiyo dira yetu na mwelekeo na hizi ndizo mechanisms zitakazotufikisha huko,other than that tunacheza tu kwenye tope kama mentaly incompetents.
 
Pamoja na kulaumiwa, kimsingi hatujui makubaliano ya Mkapa na wananchi yalikuwaje anapohamia pale Mkuzi kijijini. Ninachokumbuka ni kwamba Mkapa alihamia pale kwa kukaribishwa na Mhe. brigedia mtaafu Hassan Ngwilizi ambaye alikuwa mtu wa karibu sana wa Mkapa. Mkuzi ni nyumbani kwao Hassan Ngwilizi na ni majirani na Mkapa.
Kwa ninavyoijua Lushoto, ardhi ya kule imejaa sana kuliko uwezo wake (carrying capacity), hata hizo hekta zilizotajwa na mwandishi haziwezi kupatikana kwa eneo la Mkuzi pekee, labda uchanganye na vijiji vingine vya kata ile ya Kwai kama vile Kwemakame na Kwekanga.
Kimsingi nadhani mwenye makubaliano ya wanakijiji na Mkapa juu ya kuepeana ardhi angetupa taarifa hizo, kwa sababu eneo alipojenga Mkapa panapakana na msitu wa hifadhi ambao umetunzwa vema sana, sidhani kama atakuwa 'Kajiuzia".
 
Tusiwe kama "machizi" chini ya ubepari Mkapa hajafanya kosa,halafu keshasema mwenyewe tatizo ni maadili ya uongozi kupewa kipaumbele,hapo inaonyesha ni kwajinsi gani viongozi wetu wametofautiana na wananchi,vigezo vya kumchagua rais ndivyo sivyo,nandio maana tukishampata rais tunashangazwa na madudu,hatupimi,tunaangalia tu kama ni CCM haya twende,bado tu mentality kama ya enzi za mwalimu kuona upande ambao ni tofauti na CCM ni "kivuli"
Hadi hapo tutakapopata kiongozi atakeyesema sasa hii ndiyo dira yetu na mwelekeo na hizi ndizo mechanisms zitakazotufikisha huko,other than that tunacheza tu kwenye tope kama mentaly incompetents.

Hiyo Ardhi alinunua au aliwanyang'anya?
Sikumbuki kusikia malalamiko ya kunyang'anywa ardhi huko Lushoto. Si wamesikia wamang'ati walivyopambana kulinda ardhi yao isitwaliwe hivi majuzi?

Na kwa nini wanataka vibarua visivyowatosheleza? Kuna mashamba kule segera, wakalime mazao yao ili wauze kwa bei kubwa kuliko kuwa vibarua!
 
Chini ya ubepari hiyo ardhi mbona kiduchu tu?Watajuuta kuburuzwa wananchi wa Tanzania....Hadi watakapojuwa kuwa viongozi wanaowachaguwa ndiyo wenye kuweka sera zinazo waathiri moja kwa moja kama ilivyotokea huko Lushoto ndiyo wataingiza akili.
 
Mbona nasikia sehemu alipokuwepo Mkapa lilikuwa shamba la setla hata kabla yeye hajafika? Kama alinunua kwa huyo setla hao wananchi kawadhulumu vipi?

Amandla........
 
Wabongo bwana, yaani tumesahau yote aliyofanya Mkapa kwa nchi yetu. barabara zote alizojenga, Dar - Mwanza sasa hivi ni safari ya masaa tu ukilinganisha na siku za nyuma ambapo tulikuwa tunakwenda kwa siku mbili. uwanja wa taifa, madaraja, alivyoinua uchumi nchi yetu ikaanza kupata heshima kimataifa, tumesahau kwamba aliikuta nchi ikiwa imekwisha kabisa.
Tumesahau kazi ngumu aliyoifanya ya kulipa madeni aliyokopa Mwinyi na kuirudisha nchi kwenye mstari, tumesahau pia kazi ngumu aliyoifanya mkapa ya kurudisha heshima ya mfanyakazi ambaye wakati wa mwinyi alipoteza kabisa thamani, tumesahau alivyofuta kodi ya kichwa, alivyofuta ada za shule ili kuwezesha wengi waende shule na mengine mengi ambayo hatuwezi kuyahesabu. Leo tunamdhihaki na kumnyanyasa namna hii. Kwakweli binadamu hatuna wema jamani. Muacheni mzee wa watu apumzike. kaifanyia makubwa nchi yetu. hata kama aliiba, alichokifanya pia kinaonekana. Hawa wapinzani wanapewa ruzuku kila siku, hatujawasikia hata wamesaidia kusomesha watoto yatima. Waende zao huko bwana. Mwacheni Mkapa wetu.
Pamoja na mazuri yote hayo (kwa mujibu wako), je ndo tumpigie vigelegele akifanya FYONGO?
Dawa ya malaika muasi ni Jahanam ya MOTO, kama Mkapa hatorudisha aliyoiba basi moto wa ahera unamngoja bila shaka.
Hatutanyamaza mpaka anyooke
 
Madongo anayopata mbona tayari ni moto! huyu jehanamu kaianzia duniani ila ana ngozi ngumu kama ya tembo la sivyo angeshakubali makosa na akasamehewa yakaisha, naomba mungu aniongezee siku mpaka nione mwisho wa huyu chinga kwani naamini kuna siku ya siku atalipa vyote alivyokwapua kutoka kwa watanzania na kama si 2010 au 2015 basi 2020 penalt zitaamua nani mshindi, namwombea saaana afike huko
 
Mahakama ipi? Hizi mahakama za Kikwete zinazosema "muacheni mzee apumzike"? Au wameanzisha mpya?

You have said it all, Mahakama za Kikwete? Hakuna mahakama bali michezo ya kuigiza ya kuwapeleka wakina Mramba mahakamani wakati huohuo anachagulia kuwa bosi wa Tanroads wa mkoa! Nchi imepata kiongozi msanii na inaendeshwa kisanii, lakini ole wenu CCM kwani kila mnalolifanya gizani ipo siku litawekwa kwenye mwanga kama ilivoanza kutokea. Mkapa & Kikwete, you wont get away for all the evils you have commited and letting your fellow evils commit.
 
Haya makaburi yalishasahaulika watz, inakuwaje leo kwenye majonzi?

1. Mkapa kwa nini ulijiuzia mgodi?
2. Mkapa kwa nini uliiuza NBC kwa marafiki zako kwa bei chee?
3. Mkapa kwa nini ulianzisha meremeta na deep green?
4. Mkapa lakini ulijitahidi kukusanya kodi
5. Mkapa kwa nini uligawa chuo cha TANESCO kwa waislam?
6. Mkapa kwa nini ulimuua Gen. Imrani Kombe?
.

Hayati huwa hasemwi kwa mabaya
 
Wabongo bwana, yaani tumesahau yote aliyofanya Mkapa kwa nchi yetu. barabara zote alizojenga, Dar - Mwanza sasa hivi ni safari ya masaa tu ukilinganisha na siku za nyuma ambapo tulikuwa tunakwenda kwa siku mbili. uwanja wa taifa, madaraja, alivyoinua uchumi nchi yetu ikaanza kupata heshima kimataifa, tumesahau kwamba aliikuta nchi ikiwa imekwisha kabisa.
Tumesahau kazi ngumu aliyoifanya ya kulipa madeni aliyokopa Mwinyi na kuirudisha nchi kwenye mstari, tumesahau pia kazi ngumu aliyoifanya mkapa ya kurudisha heshima ya mfanyakazi ambaye wakati wa mwinyi alipoteza kabisa thamani, tumesahau alivyofuta kodi ya kichwa, alivyofuta ada za shule ili kuwezesha wengi waende shule na mengine mengi ambayo hatuwezi kuyahesabu. Leo tunamdhihaki na kumnyanyasa namna hii. Kwakweli binadamu hatuna wema jamani. Muacheni mzee wa watu apumzike. kaifanyia makubwa nchi yetu. hata kama aliiba, alichokifanya pia kinaonekana. Hawa wapinzani wanapewa ruzuku kila siku, hatujawasikia hata wamesaidia kusomesha watoto yatima. Waende zao huko bwana. Mwacheni Mkapa wetu.
Hayo aliyafanya kwa sababu ulikuwa ni wajibu wake na alikuwa analipwa pesa ndefu na watz kwa kazi hiyo.

Sasa mnataka mtu apewe sifa au shukrani kwa kutimiza majukumu yake yaliyomuweka ofisini.
 
Pamoja na kukumbuka mazuri aliyofanya basi ni vile vile lazima asahihishwe mabaya aliyofanya. Overal a president is elected and paid for an Excellent Job; not for stealing. Ni vizuri kumwajibisha Mr. President all the time ajue "to do the right thing"
Tanzania kanajengeka ka utamaduni ka kumsifia mtu anayetimiza majukumu yake tena wakati mwingine chini ya kiwango.
 
Back
Top Bottom