Mjue Vice President wa Makampuni ya Alibaba Duniani: Judy Wenhong

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,072
Judy Tong Wenhong alijiunga na kampuni ya Alibaba mwaka 2000 (mwaka mmoja tu baada ya kampuni hiyo kuanzishwa), kama mtu wa mapokezi (Receptionist) kwa kuwa hakufanikiwa kupata nafasi aliyoiomba awali ya Afisa biashara.

Watu wake wa karibu walimshauri aache kazi, lakini aliendelea kufanya kazi ktk kampuni hiyo changa hadi mwaka 2004 alipotaka kuondoka lakini mmiliki wa kampuni hiyo Jack Ma' alimwomba asiondoke na kuahidi kumpa 0.2% ya hisa za kampuni hiyo endapo ingeorodheshwa katika soko la hisa.

Judy alikubali na kuendelea kufanya kazi na kupanda ngazi kuwa Customer care service Manager na baadae Human Resource Manager. Mwaka 2006 alimuuliza Jack Ma' kuwa ni lini Alibaba itaorodheshwa kwenye Soko la Hisa, Jack alimjibu "hivi karibuni" na alimhakikisha mwaka 2006 kampuni hiyo ingeanza kuuza Hisa. Lakini hadi mwaka 2006 unaisha Alibaba haikufanikiwa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa.

Jack Ma' aliomba radhi na kumuomba Judy aendelee kufanya kazi Alibaba. Mwaka 2010 mtaji wa Alibaba ulifikia thamani ya $100M lakini bado haikufanikiwa kujiorodhesha kwenye soko lolote la hisa duniani.

Mwaka 2014, Alibaba ilijiorodhesha kwenye Soko la Hisa la New York (NYSE) na kuuza hisa moja kwa $68 katika Soko la awali (IPO). Alibaba iliweka rekodi ya kuwa kampuni ya kwanza kupata fedha nyingi katika uuzaji wa hisa kwenye hatua ya awali. Ilipata kiasi cha $21.8bln sawa na TZS Trilioni 48 za kitanzania, na kuifanya kuwa kampuni ya teknolojia yenye thamani kubwa kuliko Amazon, Google, Microsoft etc.

Jack Ma' akampa Judy 0.2% ya hisa zote ambazo zilikua na thamani ya $100M sawa na TZS Bilioni 250 za kitanzania. Alibaba iliendelea kuuza hisa zake na kukuza mtaji wake kufikia thamani ya $170.8bln, sawa na TZS Trilioni 392 za kitanzania.

Kutokana na thamani ya hisa za kampuni kuongezeka, 0.2% ya hisa za Judy nazo ziliongezeka thamani kutoka $100M hadi $320M sawa na TZS 740 Bilioni za kitanzania. Hii ilimfanya kuwa mmoja wa mamillionea wapya ndani ya Jamhuri ya Watu wa China. Kwasasa ni Mwanamama Judy Wenhong ni Makamu wa Rais wa makampuni ya Alibaba duniani.
 
kila mtu na mda wake
 
Hadithi hii inatufundisha hasa wadogo zetu, wanaomaliza chuo, wasichague kazi na wawe na subira...

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Kwa mahesabu ya kibongo bongo hela anayolipwa ni kubwa kiasi fulani lkn kwa mahesabu ya level za Us , Ulaya, Japan na China yenyewe hiyo hela ni ndogo sana yaani kampuni inapiga trilions za kutosha halafu yeye bado anapewa vi bilioni kadhaa tu isitoshe mchango wake kwenye kampuni unaweza ukawa unaingiza pesa zote hizo achilia mbali skilled labours wengine

Huyo hata kwa Mond haoni ndani

Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
 
Dah..ninyi mashabiki wa wcb mna tabu sana yaani huyu ukamfananishe na bosi wenu? Kwa wasanii wa afrika wanaoongoza kwa kipato ni Akon ana usd80m anafata black coffee usd60m kisha Davido ana usd16m,Don jazzy usd10m star boy wa nane ana usd4m bosi wenu hayupo kwenye hyo list niletee hp bosi wako ana ngapi maana huyo bi mkubwa ana usd 320m yaani kamfunika hadi Akon ni 740b za kitanzania kobongobongo diamond kapiga sana hatua ila tusiwe vipofu kumfananisha na watu wenye mkwanja!
 
Tumekupata Billionea wa Tandale.
 
Bado hiyo hela ni ndg sana kubalance kazi anayoifanya na anacholipwa kulinganisha na kile kampuni inachokipata

Back
Top Bottom