Mjomba we yamekukuta!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Sitasahau siku moja nilikuwa nakatiza mitaa ya sahare Tanga.Nilikuwa nimeboreka tu kukaa school wikiendi nikaamua kuranda randa mitaa hiyo japokuwa nilikuwa siijui vizuri.Basi katika tembea tembea,nikafuata njia moja pana tu japokuwa sikujua inaelekea wapi.Njiani nilikutana na akina dada watatu wanasukana.Sijui kwa nini niliamue vile,ila niliamua kutowasalimu,nikapita makavu full kuwachunia.Wale akina dada wakaacha kusukana huku wakiniangalia kwa mshangao.Duh!nilipofika mbele nilikutana na bonge la ukuta yaani njia ndo imeishia hapo halafu hakuna njia mbadala ya kuchepuka.No way out,ilibidi nirudi nilikotoka kwa njia ile ile.Nilipowafikia wale akina dada walikuwa hoi kwa kicheko,'hehehee!,haloo!watu bwana,naona hajamkuta mwenyeji wake.Toka siku hiyo nimeshika adabu,salamu muhimu kwa kila ninayemkuta.vipi wewe,umewahi umbuka kwa chochote kile au kushuhudia mtu akiumbuka?,jiachie utupe story yako!
 
mi hizi mvua za juzi dar ziliniabisha, sikujua kumbe nilivaa viatu vyenye tundu kwa chini. Sasa katika pilika pilika za hapa na pale nikafika kwenye nyumba moja ambayo ilinilazimu nivue viatu. Wee! Mbona ilikuwa kimbembe hizo sox.
 
Jamaa yangu mmoja alipitiliza kituo bila kupenda asubuhi baada ya kujenga banda lililosababishwa na binti mmoja aliyesimama mbele yake. Alishuka kituo cha 3 baada ya banda kuvunjika. Bahati mbaya alikuwa kachomekea
 
Jamaa yangu mmoja alipitiliza kituo bila kupenda asubuhi baada ya kujenga banda lililosababishwa na binti mmoja aliyesimama mbele yake. Alishuka kituo cha 3 baada ya banda kuvunjika. Bahati mbaya alikuwa kachomekea
ahahahaaah!mkuu umeniacha hoi sana,ladies hawajui tu,wanatutesa sana na usiombe ikawa umevaa suruali ya kitambaa laini,utafoji mkongojo wa mzee utembee kwa kuinama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom