LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 13,535
- 18,422
Kuna mama mmoja alifiwa na mume wake, fasta akauza nyumba kabla ya ndugu kusanuka wamtimue akaenda kununua nyumba nyingine na akahamia huko akawa amewapoteza maboya ndugu wa mume wake wasimletee undava. Mwingine naye alifiwa na mume ndugu wa mume wakavamia nyumba wakitafuta hati ya nyumba na kuziteka mali za ndugu yao ili mwanamke asiwawahi ujanja na kujimilikisha mali bila ndugu wa mume kupenda. Wanandugu nao ni washenzi, wakati ndugu yao na mke wake wanachuma mali wao waliwasaidia? Tuwatetee wajane kwa nguvu zote wasidhulumiwe na ndugu za waume zao