Mjadala wa Ushauri na tiba ya maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)

Habari wanaJF,

ninaomba msaada wenu. Mimi ni mwanamke aged 37, kawaida katika mzunguko wangu wa hedhi huwa napatwa na maumivu makali sana hasa day1 na 2. sasa naona tatizo limeongezeka maana ikishapita wiki moja baada ya hedhi ninapatwa na maumivu makali sana ambayo yanaweza kudumu kwa siku nzima au masaa zaidi ya 12.

Maimivu haya huwa chini ya kitovu ni makali kiasi nashindwa kusimama au kunyanyua mguu. Nimetibiwa hospitali mbalimbali lakini naona hakuna alieweza kunipa sababu kamili ya maumivu haya zaidi ya kuhisi labda hutokea kipindi cha kupevuka yai au. Mimi sijabahatika kupata mtoto japo mimi na mume wangu tumepimwa na kuonekana hakuna mwenye tatizo kati yetu na tatizo la maumivu wakati wa hedhi niliambiwa labda baada yakupata mtoto yangeisha.

Naombeni msaada wenu doctors wa jf na yeyote aliekutana na tatizo hili hata ushauri tu utafaa ninateseka sana. huwa natumia diclopar kupunguza maumivu wakati mwingine nazidisha dose ili niweze kupata usingizi.

Nisaidieni niondokane na tatizo hili
 
mke wangu naye alikuwa na tatizo kama hilo ila alipokwisha kuzaa..tatizo lilikwisha kabisa..
 
KILA mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika.


DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.


MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.
Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.


JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.


Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.
Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.

TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.


UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.


Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.



PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)
 
Imekuwa ni kawaida kwa wanawake waliowengi kupata maumivu ya tumbo na kiuno wakati wanakaribia zile siku zao(menstrual period). Wanawake hao wamekuwa wakitumia dawa mbalimbali za maumivu ili kuondokana na adha hiyo ya maumivu. Lakini Asilimia kubwa ya wanawake (siyo wote) wanaweza kuondokana na taabu hiyo kama watakuwa wanafanya mapenzi. Wakati wa kufanya mapenzi mwili huzalisha ganzi maalumu inayosaidia kuondoa maumivu hayo, hasa ikichagizwa na homoni ya furaha (endorphins) na ustareheshwaji wa misuli yote ya viungo vya uzazi. Kwa maelezo zaidi soma hapa. Sex treats hangovers, painful menstruations and common cold - English pravda.ru
 
Hangover na common cold sawa naweza kukubali hiyo ngoma nyingine isikiage tu kwa jirani acha kabisa.
 
ni haramu haramu haramu tena haramu kufanya mapenzi wakati mwanamke yuko katika hedhi. Huu ni uchafu. Inatakiwa asubiri mpaka atakapo kuwa safi. Na hayo madawa unayosema japokuwa yatampunguzia maumivu lakini yatamletea madhara makubwa ikiwemo kansa.
 
Huwezi amini,last year august niliumwa mpaka nikaenda hospital,na nilianza na sindano maumivu yalikua makal sana,daktar akaniulza Una mtoto,nikamjibu hapana,umewah kuharibu/kutoa au ndo umetoa mimba jibu ikawa hapana..wakafkir me mwongo..nikafanyiwa ultra sound na hakukua na shida yoyote akanishauri nibebe mimba tumbo litatulia..ndo mana nikashangaa
hamna kitu kama hicho
watu tumezaa na ikifikia mp
unaumwa mpaka unatambaa bila kujijua!

 
Huwezi amini,last year august niliumwa mpaka nikaenda hospital,na nilianza na sindano maumivu yalikua makal sana,daktar akaniulza Una mtoto,nikamjibu hapana,umewah kuharibu/kutoa au ndo umetoa mimba jibu ikawa hapana..wakafkir me mwongo..nikafanyiwa ultra sound na hakukua na shida yoyote akanishauri nibebe mimba tumbo litatulia..ndo mana nikashangaa
duh huyo doc kiboko
uongo mtupu hakuna lolote!
 
Kuna baadhi wakijifungua maumivu yanakwisha kabisa moja kwa moja.

Kuna wengine yanapotea kwa muda baadae yanarudi, ila ukali unakuwa umepungua.

Kumbe kuna wengine maumivu yanabaki ya ukali ule ule?

Huwezi amini,last year august niliumwa mpaka nikaenda hospital,na nilianza na sindano maumivu yalikua makal sana,daktar akaniulza Una mtoto,nikamjibu hapana,umewah kuharibu/kutoa au ndo umetoa mimba jibu ikawa hapana..wakafkir me mwongo..nikafanyiwa ultra sound na hakukua na shida yoyote akanishauri nibebe mimba tumbo litatulia..ndo mana nikashangaa
 
ukweli kuzaa kunategemeana na homoni za mwanamke wengine hupata ahueni wakizaa lakini wengine huoja joto ya jiwe hadi kiama na ndio laana ya adamu na eva huonekana kikubwa ni kutumia kila njia kupunguza maumvu yanapozidi sana
 
Nina miaka 27, nimekua nikipata hedhi kila baada ya 30 days, inatoka kiasi na maumivu kidogo ya tumbo. Tokea huu mwaka uanze siku zimebadilika sana maana naweza kuona baada ya 28 days, 26 days, 18 days, imekua ikitoka nyingi sana kama mabonge ya damu iliyoganda ikiambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu. Naombeni kujua tatazo ni nini maana nakosa amana kwani hata bila kusema watu wanagundua kwa ninavyohangaika. Note: sina motto na wala sijawhi kufanya mapenzi maisha yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom