MJADALA WA UMEME ITV: Renatus Mkinga apotezwa ghafla

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Katika mjadala wa ITV unaoendelea leo saa 10.30pm kulikuwepo wachangiaji mbalimbali wakiongozwa na Chua kama mwenyekiti. Lakini Ghafla RENATUS MKINGA kapotezwa Ghafla na kuwekwa Jamaa wa uchumi.

Kwa jinsi mjadala ulivyokuwa mkali Renatus mkinga alikuwa anamwaga data za uhakika ghafla kaondoliwa katika mjadala

Je Kuna agizo lolote la kumtoa??
Kwanin hawakutoa wengine ?
 
Huu ni uchakachuaji wa Uhuru wa Maoni wa khali ya juu.
Pa1 na huu unafiki uliofanywa na itv kwa kuwanyima Wananchi fursa yakupata Kuelimishwa juu ya Madudu yanayofanywa na serikali kupitia hii Wizara ya Nishati pa1 na Ndg yake Ewura na Wananchi walala hoi kubebeshwa mzigo wakulipia gharama kubwa za umeme nampongeza sana Mkinga kwa Elimu aliyoitoa kwa Umma kwa ujasiri wa khali ya juu.
 
Wana JF naomba msaada wenu kwa kilichotoke kwa Mzee Mkinga ambaye alikuwepo kwenye mjadala wa kipima joto ITV kuhusu kupanda bei ya Umeme.

Kwana kabisa huyu mzee alichelewa kufika, na kipindi kikawa kimeanza. Lakini baada ya kuwasili kwa mzee huyu alipewa nafasi na kushusha nondo zake kama kawaida kuhusu matatizo yanayoikumba nchi hii hasa Tanesco. Katika maelezo yake Mzee mkinga ambaye ni mwnachama wa TANU kwa jinsi alivyojitambulisha na haamini katika CCM ya sasa aliituhumu serikali pamoja na wanasiasa kushindwa kuendeleza vyanzo vipya vya umeme na kubaki kuihujumu Tanesco na kuiingiza kwenye mikataba feki kama IPTL, Songas, Agreko, Richmond na DOwans na baadae kuiachia Tanesco na wananchi wakibeba hiyo mizigo kama inavyotokea kwa sasa katika malipo ya Dowans 185 bil.

Ila cha kushangaza ni huyu mzee pamoja na kuongea kwa hisia mambo yote haya na kupenda kuongezewa muda wa kutoa ufafanuzi zaidi, ilifika muda wa mapunziko Commercia Break.

Baada ya mapunziko sikumwona tene huyu mzee na hadi kipindi kinafika mwisho hakuonekana sasa sijui alikumbwa na kitu gani. Je ulifika muda wake akaondoka au aliondolewa kwenye kipindi?

Tafadhali wenye taarifa kama ITV au Chuwa tupe ufafanuzi au Kama Mzee Mkinga uko humu tunaomba ufafanuzi wa kilichotokea maana hii si kawaida na watu tulikuwa tunafuatilia michango yake.

Peoples Power Katiba Mpya Lazima Maana.
 
Hilo litakuwa jambo jema kama alienda huko, kama na MS wimbo wa katiba mpya uko kichwani muda wote basi lazima ipatikane.

Vizuri sana MS umejitahidi.
 
alienda kushughulikia katiba mpya ya chadema

Kuwa harakati za kudai katiba mpya ni ajenda ya Chadema hilo halina mjadala, kuwa madai ya katiba mpya ni ajenda ya Watanzania wote hilo pia halina mjadala kwa sababu CHADEMA ni chama cha Watanzania wote wanaopenda kuuona nchi hii ikibaki kitu kimoja.

Ajenda ya udini na ubaguzi ambayo wewe na watu wenye akili finyu kama za kwako ndiyo sumu mbaya kuliko zote ambazo imeweza kutumbukizwa katika taifa hili, wanaojificha nyuma ya pazia la udini kuficha uhalifu wao wote ni wahalifu ambao wanatafuta namna ya kutafuta hifadhi. Hawa ni hawana tofauti na wahalifu wengine kama akina Dudus
 
Guys you must be serious a bit when mentioning the world chadema, katiba siyo hoja ya chadema!!! chadema tuliwaambia humu kabla ya uchaguzi na sisi wengine sio wanachadema.

Ebu futa mawazo ya uchadema unaposema neno katiba

Halafu kutumia maneno ya 'ufinyu wa akili' haikusaidii wewe, unapiga upepo, hamuoni mtu unamtukana!!??? are you hurting him?? HOJA tu humu ,hata kama yuko kinyume na wewe mjibu kwa hoja avutike upande wako

is just a piece of advice!
 
Advice taken
 
Mnasumbuka na MS anacheza na akili zenu tu,anataka kupata zaidi hisia zenu anajua vitu gani hampendi ndiyo anawachomekea wala usifikiri anampenda kweli Zito
Tuje kwenye Mada hata mimi nilishangaa sana yule mzee sikumuona wenye data watuletee.kuhusu katiba mpya ni hoja ya nani? ni ya watanzania siyo CDM wala CCM B"s.
 
Ndugu zangu mimi swli langu linabakia pale pale Mzee Mkinga alienda wapi jana baada ya kuchangia tu kama mara mbili.

Naona tunabadilisha thread iwe ya katiba mpya. Hii inaonyesha ni jinsi gani watu walivyo serious na swala la katiba mpya.

Katiba Mpya lazima.
 
Guys you must be serious a bit when mentioning the world chadema, katiba siyo hoja ya chadema!!! chadema tuliwaambia humu kabla ya uchaguzi na sisi wengine sio wanachadema.

Ebu futa mawazo ya uchadema unaposema neno katiba

Halafu kutumia maneno ya 'ufinyu wa akili' haikusaidii wewe, unapiga upepo, hamuoni mtu unamtukana!!??? are you hurting him?? HOJA tu humu ,hata kama yuko kinyume na wewe mjibu kwa hoja avutike upande wako

is just a piece of advice!

Waberoya, Issue kubwa nadhani ni MS kuwa na tabia ya kuwatoa wachangiaji nje ya mada na kuanzisha malumbano ambayo hayaendani na hoja ya msingi iliyo kwenye thread hii.
Naomba nipe jibu au na wewe ulishangaa baada ya mzee mkinga kutoonekana?

Katiba mpya lazima.
 
Siwezi kushangaa nikisikia Mzee Mkinga alitolewa kwenye kipindi kwa amri ya Mengi with JK barking orders behind him, and of course with Rostam barking orders further behind the latter!!

If you are surprised, then you dont know Mengi or this country well...
 
Hivi kama kweli ndio hivyo, tutafanyiwa hivyo mpaka lini maana ni kuwafumba watu macho, Lakini siku hata hao wakurugenzi na wamiliki wa vyombo vya hibari visivyo vya kweli siku inchi hii ikichukuliwa na upinzani wataenda wapi?

Maana kinachofanyika sasa ni kubaka democrasia ambayo CCM na serikali yake wamekuwa wakiihubiri kwa Miaka 49. Na umaskini wote tunaosababishiwa.

Peoples power.
 
Wana JF naomba msaada wenu kwa kilichotoke kwa Mzee Mkinga ambaye alikuwepo kwenye mjadala wa kipima joto ITV kuhusu kupanda bei ya Umeme.

Kwana kabisa huyu mzee alichelewa kufika, na kipindi kikawa kimeanza. Lakini baada ya kuwasili kwa mzee huyu alipewa nafasi na kushusha nondo zake kama kawaida kuhusu matatizo yanayoikumba nchi hii hasa Tanesco. Katika maelezo yake Mzee mkinga ambaye ni mwnachama wa TANU kwa jinsi alivyojitambulisha na haamini katika CCM ya sasa aliituhumu serikali pamoja na wanasiasa kushindwa kuendeleza vyanzo vipya vya umeme na kubaki kuihujumu Tanesco na kuiingiza kwenye mikataba feki kama IPTL, Songas, Agreko, Richmond na DOwans na baadae kuiachia Tanesco na wananchi wakibeba hiyo mizigo kama inavyotokea kwa sasa katika malipo ya Dowans 185 bil.

Ila cha kushangaza ni huyu mzee pamoja na kuongea kwa hisia mambo yote haya na kupenda kuongezewa muda wa kutoa ufafanuzi zaidi, ilifika muda wa mapunziko Commercia Break.

Baada ya mapunziko sikumwona tene huyu mzee na hadi kipindi kinafika mwisho hakuonekana sasa sijui alikumbwa na kitu gani. Je ulifika muda wake akaondoka au aliondolewa kwenye kipindi?

Tafadhali wenye taarifa kama ITV au Chuwa tupe ufafanuzi au Kama Mzee Mkinga uko humu tunaomba ufafanuzi wa kilichotokea maana hii si kawaida na watu tulikuwa tunafuatilia michango yake.

Peoples Power Katiba Mpya Lazima Maana.

Presha ilimpanda alienda hospitali, si mnajua tena huyu mzee huwa ana presha
 
Iweje jana presha impande na kwa nini hatukujulishwa na mtangazaji. Mbona siku zote anachangiaga mpaka mwisho jana kuna nini?
 
Mimi pia nilishangaa sana,yule mzee alikuwa mwiba kwenye kile kipindi kama kawaida yake,lakini baada ya kuzungumzia jinsi pesa zilizotolewa na serikali kama stimulus package zilivyoliwa na wajanja ana majina ya hao wajanja na walikulaje akaondoka. Isije ikawa aliondolewa,maana tumesikia mambo ya magazeti kuzuiwa kuchapwa na mengine kuharibiwa kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom