Mjadala wa hukumu ya mahanga [segerea] na haishi [sumbawanga] mjini.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Wakuu.
Nia sio kuingilia maamuzi wala kile kinachoitwa kuingilia uhuru wa mahakama. Binafsi napata Tabu kuziweka kwenye urari hukumu kati ya Makongoro Mahanga wa jimbo la Segerea na ile ya Hilal Haeshi wa jimbo la Sumbawanga mjini.

Naona tuhuma za Mahanga zilikuwa wazi kutokana na aina ya ushahidi kama jinsi zilivyo kuwa wazi hadi kumuengua Haeshi. Wabobezi naomba msaada.
 
Mkuu kila mtu yuko flabagasted. Tunajiuliza majaji wameweka professional zao chini na kutoa hukumu kwa kuogopa MKULU au ViPi? Ushahidi mkubwa tena wa wazi bado jaji anakuwa very irrational bila aibu anaminya haki ya mtu kumfurahisha mzee kicheko!!. Naamini utafika wakati ambao watarudisha mezani professional zao ili watende haki lakini watajikuta too late wameshakuwa washtakiwa. Mbaya zaid watahukumiwa na sheria walizokataa kuzitumia ingawaje walizijua na hapo watasikia uchungu wa kuzikwa ukiwa hai.
 
Ukisoma kwa makini utaona ya kuwa Mpendazoe katika madai yake alisema walimkamata Dr Makongoro na masanduku ya kupiga kura.Alipotakiwa kumleta shahidi mmoja tu wa wale waliomkamata na kumpeleka polisi,Mpendazoe badala ya kumleta shahidi, yeye akapeleka gazeti lililoandikwa Makongoro akamatwa na masanduku ya kupiga kura
 
Waliomshitaki Lema huko Arusha hata ushahidi wa kagazeti walikosa na bado walishinda!!!!!
 
Nimepata nafasi ya kusoma hiyo hukumu; ni uzembe tu wa petitioners kutoa ushahidi, na pengine wakili wake alaumiwe;
1. Kwamba mtendaji alikamatwa na matokeo feki na Mpendazoe kwenye Amended Petition alisema ana ushahidi wa CD ambao angeuleta Mahakamani, lakini hakuupeleka.
2. Kwamba kuna kijana alikamatwa na mihuri na karatasi za matokeo na angepeleka CD, hakuipeleka mahakani pia.
3. Kwamba Makongora alikamatwa na masunduku kumi, alipeleka gazeti ambalo hata halikumtaja mtu zaidi ya kusema mgombea wa chama fulani; na hata hivyo hakukua na ushahidi uliotolewa mahakani.
Etc! Kwa kifupi ni kwamba hawakuthibitishwa madai yao "beyond reasonable doubts", Na hata yule aliyeamua kesi ya lema hakuwa na ushahidi wa kumvua Lema ubunge; Wakati hukumu ya Lema imejaa mapungufu kibao; hukumu ya Mahanga ni uzembe wa walalamikaji kuwa makini na ushahidi walioupeleka mahakani, inawezekana wakili hakuwa fit kivile.

I humbly submit.
 
Back
Top Bottom