Hussein Bashe: Wakulima wa Katavi, Kiteto na Sumbawanga wasiuze Mahindi chini ya Tsh. 800 kwa kilo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 54, leo Juni 23, 2023.



Tanzania kutokomeza Ugonjwa wa Malaria ifikiapo mwaka 20230
Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel amesema hadi sasa kuna mikoa zaidi ya 9 nchini iliyo na kiwango cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria chini ya 1% huku mikoa mingine mingi ikipinguza ukubwa wa tatizo hili.

Amesema hadi kufikia mwaka 2023, Tanzania inaweza kuingia kwenye orodha ya nchi zisizo na ugonjwa huu duniani.

Hussein Bashe: Wakulima wa Katavi, Kiteto na Sumbawanga wasiuze mahindi chini ya Tsh. 800 kwa kilo
Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Jonathan Msambatavangu amesimama kuomba mwongozo wa Spika kuhusu utaratibu mpya uliowekwa na Serikali kwenye kuuza mahindi, jambo lililofanya kushuka kwa bei ya Mazao.

Hoja hii imeungwa mkono na Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa CCM, Momba alietaka Bunge liijadili na kutoka na msimamo wa pamoja.

Wazo hili limeungwa mkono na Wabunge wengine na kisha Spika wa Bunge akaruhusu mjadala.

Sophia Mwakagenda (Viti Maalum) amedai vituo vya Serikali vinavyonunua mahindi vipo mbali na wananchi, baadhi husafiri hadi kilomita 100. Amedai pia baadhi ya wanunuzi wa Serikali wamekuwa sio waaminifu, hukataa mazao hayo na kuyanunua pembeni ili wapate faida kubwa.

Ameishauri pia Serikali kuruhusu Soko huria ili wakulima wapate faida.

Naye Mbunge wa Geita Vijijini Mhe. Joseph Kasheku amesema wabunge wamuogope Mungu kwani mwanzoni walilalamikia mazao kuwa na bei kubwa.

Amesema yeye ni mfanyabiashara, na serikali ilichofanya ni kuweka utaratibu mzuri unaoweza kufanywa na wafanyabiashara wengine. Mhe. Msukuma amedai kuwa kuachia soko bila udhibiti inaweza kusababisha Serikali kupoteza mapato.

Aidha, hoja ya NRFA kukosa uwezo wa kununua mahindi yote umejadiliwa na maelezo ya Serikali yanayotolewa Bungeni na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe hayana uhalisia kwa wakulima. Serikali iwaache wakulima wauze mazao yao popote.

Deus Clement Sangu, Mbunge wa CCM jimbo la Kwela amedai kuwa mchakato wa upatikana kwa vibali sio mrahisi kama unayopigiwa chapuo na wengi. Ameishauri Serikali kuchana na mpango huu kwa mwaka wa fedha 2023/24 ili ijipange kuanzia mwakani.

Akichangia hoja hii, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijafunga mipaka bali imetoa utaratibu wa namna ya kuvuka hiyo mipaka. Amewashauri wafanyabiashara kuchukua leseni na kuuza popote wanapotaka, kinachofanywa na Serikali ni kurasimisha biashara ya mazao kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema Serikali ya CCM na Rais Samia hawawezi kuanzisha mipango inayomkandamiza mtanzania na Serikali haijazuia uuzwaji wa mazao nje ya Nchi. Mfumo wa kutoa export permit unafanya kazi muda wote.

Mhe. Bashe amesema watu wanaotoka nje ya nchi wataua soko kwa wakulima na wanaotaka kununua mazao ya watanzania waingie wasajili kampuni na kununua mazao kutoka kwenye kampuni za watanzania.

Amesema wakulima wa Katavi, Kiteto na Sumbawanga wasiuze mahindi chini ya Tsh. 800 kwa kilo.
 
Mkuu kiuhalisia Kuna Mambo mengi haupendezwi nayo kwasasa ndani ya Nchi hii na Kuna sehemu niliona umetoa maoni kuhusu orodha ya Viongozi ambao Samia hapaswi kuwaomba ushauri kuhusu suala la Bandari na DPW je unadhani baada ya Samia2030 Kuna vijana waliopo Sasa katika Siasa na Uongozi wa mihimili nchini ambao ni sahihi wa kuaminiwa kupewa dhamana ya kuongoza hili Taifa? Mi baada ya Magufuli kufariki baada ya Samia nilitamani Nchi ikimatwe na Jeshi hata kwa miaka 10 uku tukiendelea kuandaa Watu sahihi wataolisaidia hili Taifa point yangu ni kwamba hawa tulio nao sasa wamejaa ukanda,udini,ukabila,u gang nk nk nk hofu yangu wakipewa tutarudi katika Yale makundi ya akina Pac na Biggie.
 
Molel atokomeze kwanza kwashakoo kwa watoto ina athari mbaya sana... ajiangalie yeye alivyokaa kaa na kile kisura chake cha ajabu hadi kakosa akili shauri ya kuugua kwashakoo utotoni.
 
Haya mambo ya kuuza chakula nje kweli haileti maana,ni kuumiza walaji, ni kweli mkulima anatakiwa kupata pesa lakini sio kwa kuwaumiza walaji,ni serikali inatakiwa kumuwezesha huyu mkulima kumudu gharama za kilimo ili hata akiuza hapa ndani apate pesa.Na hata hivyo wanaofaidika kupeleka mazao nje sio wakulima ni wafanyabiashara,asilimia kubwa ya wakulima wa Tanzania wanavuna mazao tayari wameshakula pesa,mkulima anakopeshwa tangu anaanza kulima mpaka anavuna.
 
Back
Top Bottom