Mjadala kidogo kuhusu search engine

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Sijawahi kusikia au pengine kuona mtumiaji wa mtandao asitumie search
engine kwa ajili ya kutafuta mambo yake mbali mbali , wengi wetu huwa
tunatumia sana search engine wakati wa mwanzo tusipojua pa kupata kitu
Fulani kwa njia ya mtandao ,tukisha pata kitu hicho huwa tunahifadhi
link hizo kwenye favorites au huwa tunafanya bookmark link hiyo
kwenye kwenye tovuti Fulani .

Kwahiyo katika maisha ya kawaida ya watembeleaji wa mitandao kila mtu
huwa anafungua search engine kwa ajili ya kutafuta jambo Fulani , mimi
mfano ni mpenzi wa google , wengine ni bing , yahoo na aina zingine za
search engine


Wakati fulani niliwahi kujadili jambo Fulani linalohusu maisha ya
search engines huko mbeleni katika mjadala huo , nilimwambia mmoja ya
wachangiaji kwamba watajidi wa siku zijazo katika masuala ya search
engine ni wale watakaokuwa na search engine ambazo zinatumika kwa
ajili ya kutafuta kitu au vitu maalumu , mfano madaktari wa meno wao
wanatakiwa kuwa na search engine yao ambayo ina ina mambo muhimu
kuhusu meno na masuala mengine yanayohusiana na afya za meno , fundi
wa magari nae ni hivyo hivyo .


Kwa siku za karibuni nimeona search engine nyingi zinazokuja ambazo
zinatumika kuhifadhi kumbukumbu ya vitu Fulani peke yake mfano
ukitembelea Free PDF Books, PDF Search Engine - Toodoc pamoja na www.gettheirdocs.com search
engine hizo hapo kazi yake ni kutafuta Documents za aina mbali mbali
ambazi ziko katika mitandao mbali mbali kisha unaweza kudownload moja
kwa moja , kama unavyoona hapo ukitembelea ina sehemu ya kukuwezesha
wewe kuweza kuconvert document hiyo kwenda kwenye PDF au kutoka PDF
kwenda Word moja kwa moja unapopata document hiyo pia unaweza
kudownload na mambo mengine mengi .


Ingawa search engine kubwa kama google ina jaribu kuboresha seach
engine zake kwa kuweka vitu kila mara , wakati mwingine search engine
hiyo inakuwa slow halafu inakuwa inavitu vingine ambavyo havina maana
au kupotosha kwa urahisi zaidi au sehemu ambapo search ingine hizi
kubwa zinashida kama uchina au iran zinaweza zisisaidie zaidi kwahiyo
watu watatumia search engine hizo ambazo zinakuwezesha kutafuta vitu
maalumu tu .


Search engine za kutafuta vitu maalumu ni nzuri na nyepesi sana
kutumia sema kati ya matatizo ambayo nimeyaona mpaka sasa hivi ni
ngumu mtu kufanya reference ya kile alichodownload kama sio makini ni
tofauti na google ambapo unaona kwa urahisi kitu unachodownload
kimetoka wapi , pia inawezekana watu wakapitisha baadhi ya makala na
kazi zao zingine za kupotosha kwa urahisi zaidi ambazo ni za
propaganda au kwa maslahi ya kibiashara .


Pia utaona kuna sehemu ya kuconvet kwenda word au PDF , kuna baadhi ya
tovuti zimehifadhi documents ambazo ni secured lakini unapotumia hizo
search engine zinazokuwezesha kuconvert wakati mwingine ina convert
hata kama iko secured na kufanya mabadiliko katika Document husika ,
hayo ni baadhi ya madhara yake lakini ni nzuri sana .


Mwisho kuna suala la usalama wa watembeleaji wa search engine
maalumu , wahalifu na wengine wanaweza kuweka documents au program
ambazo unaweza kudownload kwa ajili ya kukupeleleza au kukushambulia
huko mbeleni , ingawa baadhi ya antivirus zinaweza kutambua ila sio
kwa asilimia 100


Kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania huu ndio wakati wake kwa serikali
kuwa na miradi endelevu ya search engines kwa ajili ya nchi hii yaani
unapotaka taarifa muhimu kuhusu tanzania uingie katika tovuti ya taifa
ambapo kutakuwa na database ya taarifa muhimu na za kweli kuhusu
baadhi ya vitu ndani ya nchi na watu wake , naamini serikali na wadau
watapata faida kubwa sana katika matangazo na mambo mengine yanayohusu
maendeleo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom