MJADALA: Je, Pikipiki gani ni bora kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa Tanzania?

Bro,bora pkpk za china kwa sababu zina spea nying,lakin boxer ina nying fek na sio imara kama ile iliyokuja nayo na kingine n kwamba, boxer inataka upate fundi mzuri wa ingine hasa ikiua rings piston,huwa inasumbua sana na inataka vitu original,uchukua fek,itakusumbua,ni hayo tu....
Spare za boxer zipo nyingi tu, fake na original zimesambaa kila mahali.....
 
Et mtu ana mil 2.5 mtu anakushauri jichange uchukue crt 250/450
Rmz 250
Ktm 450
Kx 450 2stroke au 4 stroke unajua bei ya tairi zake pindi zitakapo isha huko kijijini kwenu umeona wanauza spare zake ngoja niishie hapo nisiji nikaonekana wa ajabu bure

Na wewe unae omba ushauri kwa upande wangu kachukue tvs 125 au haojue 125 mayai au sunlg boxer yenewe sio saana kwasababu ya inahitaji fundi wa kueleweka achana na evil...... Atakusababisha ujute pengine yeye ni tajiri ana mahera ya kuzitunza hizo kawasaki zake
 
Pikipiki yoyote inafaa na ni imara endapo tu utazingatia yafuatayo:
  • nunua toleo halisi /original
  • Ijue tabia yake (soma user manual)
  • Jali vilainishi na mafuta: epuka petrol za mtaani, imrchanganywa, ina uchafu, imepigwa jua na kubadilika rangi iko km dizeli, tembeakoki ya mafuta iwe kwenye full sio reserve.
  • Jali muda wa kubadili oil (huu ndio uhai wa injini). usichanganye changanye aina za oil. zoeza aina moja hasa nzito. usiogope bei maana wahangaza walisema CHEAP IS EXPENSIVE
  • Ikiwashwa km injini imepoa sana (asubuhi) iache silencer angalau dk 5 ipandishe oil na injini apate joto (usipandishe kwa kuvuta moto/accelerator)
  • Wajati wa kuendesha; badili gia kwa mpangilio ukisaidiwa na mwongozo wa rpm/mzunguko wa injini. sio km vijana wanabandika na kubandua. ndani ya dk 1 ameshafuta gia zote pikipiki ikiwa na muungurumo km helikopta
  • Usibebe mizigo kupindukia, utaua shock ups/springs na kupunguza ufanisi wa injini/puling capacity maana itahitaji nguvu za ziada kuhimili load na itajilipa kwenye tenki, kukata vyuma hasa chassis na carrier, kuchubua foronya na rangi mwisho waswahili ukiwemo wewe wataanza kuponda chombo sio imara
  • Jaza upepo wa magurudumu itakiwavyo angalau 55 au 60 kuepuka kurika taili, kupunguza spidi (barabara korofi haitakiwi presha kubwa, chombo itakutetemesha na kukukata mgongo. weka 40-50, fundi tyres wana ushauri murua)
  • Usimpatie dereva usiyemwamini uendeshaji wake. hapa usidanganywe na leseni yake
  • Inapobidi, isinyeshewe
  • Epuka kuosha injini ikiwa ya moto. rejea physics kutanuka na kusinyaa. utakegeza nati muhimu za injini na michubuko au kudhoofisha ile steel ya vyuma.
  • Weka vipuri halisi hata kwa gharama kiasi.
  • Tumia fundi mmoja na mwaminifu kwa matengenezo makubwa hasa injini na umeme. awe anakumbuka kipi akifanya previous services.
  • Zingatia sheria za usalama barabarani, rough overtaking na khchomekea kumewaacha wengi kwenye nyumba za milele wakisubiri ufufuo na maelfu hawana miguu, mikono, ngozi za uso n.k

-MWISHO SI KWA UMUHIMU: TOA SADAKA, FANYA MAOMBI UWE KARIBU NA MUUMBA MAANA HAYA NI MAJENEZA YANAYOTEMBEA
 
Click.. Sijajua bei gani zile bike za kibishoo nzuri sana kwa mizunguko ya mjini hata nje ya mji nikimaanisha ukitaka kufanya cruise tour..na bei yake yamoto.. Sikumbuki bei halisi..
Ninaitumia click tangu 2012, na iko poa ingene haijaguswa.
Bei zinategemea na model na cc
Ila mpya zinaanzia 6m
Used 3 mil
 
Jamaa umemtajia mwenzio mikipiki kama vile anataka za mashindano

yani mi baja ya juu juu imekaa kukimbizana kimbizana tuu kama watu wa mereran

Mkuu we kama hutaki makuuu vuta TVS yako uchune kimyaaaa

ushasema ni matumizi binafsi inakutosha hiyo TVS vizuri tu au Boxer

Nunua piki piki ambayo ukiichoka unaweZa iuza ndani ya siku tu ishapata mteja

wewe sasa jichanganye ununue hiyo midude aliokushauri charldzosias

ukija kutaka kuiuza utakoma,utakaa nayo mpk uzeeeni we tafuta ndoa tu.

hiyo bajeti yako wala usitake makuuuu
hahahaha daaah umeshuka point sana mkuu
 
Tafuta pikipiki hizi,kwa matumizi yako binafsi na vimizigo vya hapa na pale:
1.Honda CGL 125
2.Honda CG 125
3.Honda Ace cb 125(ila hizi nadhani ni za south africa kama sikosei)
Machaguo ya kwanza ndo mjapan mwenyewe na zote zina starter.

Nina Honda CG 125 huu mwaka wa 8 sasa kitu piru bado,nna jamaa yangu alinunua mapikipiki yenu ya kihindi na mchina kwa miaka mi5 ila ukiziweka pamoja yangu bado inaonekana mpya na tunapiga na kufanya mizunguko inayofanana kwakua mishe tunafanya pamoja.

Narudia tena na tena jikaze kwenye bei pikipiki ni za mjapani tu!
 
Ni wazi kua pikipiki imara ni za Mjapan.
Sasa basi kwa bajeti yako nakushauri usifanye makosa tafuta pikipiki ya mjapan na unaweza kuongezea pesa kidogo ila usiogope maana unanunua mkataba haswa.

Tafuta pikipiki hizi,kwa matumizi yako binafsi na vimizigo vya hapa na pale:
1. Honda CGL 125
2. Honda CG 125
3. Honda Ace cb 125(ila hizi nadhani ni za south africa kama sikosei)
Machaguo ya kwanza ndo mjapan mwenyewe na zote zina starter.

Nina Honda CG 125 huu mwaka wa 8 sasa kitu piru bado,nna jamaa yangu alinunua mapikipiki yenu ya kihindi na mchina kwa miaka mi5 ila ukiziweka pamoja yangu bado inaonekana mpya na tunapiga na kufanya mizunguko inayofanana kwakua mishe tunafanya pamoja.

Narudia tena na tena jikaze kwenye bei pikipiki ni za Mjapani
 
Back
Top Bottom