Mjadala huru: Mfumo wa kumpata Makamu wa Rais unatufaa kama Taifa?

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Kila jambo linapotokea kwenye mwelekeo wa maisha ya mtu, kawaida huwa linaleta fundisho la mbele yake ya safari.

Elimu ya maisha wakati mwingine huhusisha pia, misukosuko, kufiwa n .k hii yote ni katika kuyaelekea mazuri ya ndoto yetu.

Kwa hapa Tanzania kulingana na yaliyotokea, bila ya shaka tunayo ya ķujifunza, kuyarekebisha na ama kuyaboresha na au kuyaacha kama yalivyo, kwani yote ni sawa iwapo yanatuacha imara bila shida yoyote kulingana na matukio kama hayo.

Palipo na watu (wenye busara na waliojaa hekima) pakitokea jambo lolote lenye kutatanisha juu ya misingi yao kuhusu mwelekeo wao kama binadamu, huwa halipiti hivihivi bila kupitishwa kwenye mchakato wa namna ya kuliweka sawa!

Watakaa kutaka kufanyia rejea ya jambo hilo iwapo bado linapaswa liendelee kuwa vile vile kama lilivyokuwa awali ama kuwepo na mabadiriko machache kukabiliana na changamoto ya wakati huo. Mimi nazungumizia mfumo wetu wa kumpata mgombea mwenza wa nafasi ya Uraisi.

Mfumo huu ni kweli kwamba kama Taifa hatuna la kujifunza na ama kuboresha kidogo?

Natolea mfano wa matamshi ya aliyekuwa Rais wetu hayati JPM, nanukuu ningependa kusema jambo hili ambalo sikupaswa kulisema mbele yenu wana CCM, 2015 nilipoteuliwa kupeperusha bendera ya Chama kuomba kura ya Urais, jmajina niliyokuwa nimeyapendekeza kuwa wagombea wenza wa Uraisi, miongoni mwake ni jina la Hussein Mwinyi, lakini kwa kuwa WANAWAKE wana nguvu, basi Mama Samia akapita akiwa katika ukumbi wa Chimwaga pale Dodoma kwenye mkutano mkuu wa CCM kupitisha jina la mgombea Urais kule Zanzibar!

Hoja yangu iko hapo.

Mfumo huu wa anayegombea uraisi ndiye anayependekeza nani awe makamo wake wa Raisi, Kutokana na hili lililotokea na ambapo ni kwa mara ya kwanza kama Taifa kumpoteza Rais wetu katikati ya mhula wake, kama Taifa, mfumo huu bado unatufaa?

Au vetting ipite hadi kwa wagombea wenza?

Naibariki Tanzania nchi yangu njema na nzuri kuliko nchi zote Duniani

Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wetu wote wa Tanzania, uwalinde na maadui wote wa ndani na nje

Amina
 
Mfumo unatufaa, ila pale panapotokea Rais Amefariki .....Nani awe Rais? Habari gan kuhusu Uchaguzi ? Na uitishwe baada ya muda gan?.

Suala hili ni muhimu sana, Kikawaida, Watu huchagua Rais, hawamchagui Makamo, Ivo Rais alochaguliwa na Watu anapofariki, ilipaswa Uchaguzi Mpya uitishwe ili tena watu wamchague Kipenzi wao .
 
Kila jambo linapotokea kwenye mwelekeo wa maisha ya mtu, kawaida huwa linaleta fundisho la mbele yake ya safari

Elimu ya maisha wakati mwingine huhusisha pia, misukosuko, kufiwa n .k hii yote ni katika kuyaelekea mazuri ya ndoto yetu

Kwa hapa Tanzania kulingana na yaliyotokea, bila ya shaka tunayo ya ķujifunza, kuyarekebisha na ama kuyaboresha na au kuyaacha kama yalivyo, kwani yote ni sawa iwapo yanatuacha
Imara bila shida yoyote kulingana na matukio kama hayo

Palipo na watu (wenye busara na waliojaa hekima) pakitokea jambo lolote lenye kutatanisha juu ya misingi yao kuhusu mwelekeo wao kama binadamu, huwa halipiti hivihivi bila kupitishwa kwenye mchakato wa namna ya kuliweka sawa!

Watakaa kutaka kufanyia rejea ya jambo hilo iwapo bado linapaswa liendelee kuwa vile vile kama lilivyokuwa awali ama kuwepo na mabadiriko machache kukabiliana na changamoto ya wakati huo,

Mimi nazungumizia mfumo wetu wa kumpata mgombea mwenza wa nafasi ya Uraisi

Hoja yangu iko hapo,

Kama kungekuwa na vetting ya kweli ya kumchagua rais, basi Magufuli hakupaswa kabisa kuwa rais wa nchi hii. Hiyo umakamu ni jambo dogo, tatizo hasa lipo kwenye kumpata rais.
 
Ingawa ni nje ya mada
 
Ingawa ni nje ya mada

Kwa sehemu kubwa mada yako imejikita kutoka kuonyesha rais huyu sio sahihi, bali aliyepita. Ndio nikakusaidia, ili tupate makamu wa rais sahihi, lazima tuanzie kwenye mchakato wa kumpata rais sahihi. Hapo nikakupa mfano kuwa Magufuli hakupaswa kwa rais, iwapo vetting sahihi ingefanyika.
 
Mkuu Tindo wewe ni kati ya wana Jf wakongwe, mlioshiba busara na wenye kujenga hoja!

Kinachonisikitisha mpaka hapa kukuhusu! Kwanza uzi huu hajamtaja mtu kwa majina yake!

Nasikitika kwamba, wewe unataka kuwa sababu ya kujaribu kuharibu uzi huu kwa sababu zako tu na Magufuli wako!

Kwa sababu nafahamu, badala ya watu wajikite kwenye hoja, unawafanya wajikite kumjadili Magufuli ambaye hajatajwa hapa!

Kwa heshima yako, ningependa kukuomba, mchango wako kuhusu mambo yanayoweza kuibadiru jamii yetu ni wa mhimu kuliko kukaa unamzungumzia Magufuli ambaye hawezi kutusaidia tena?

Asante
 
Kwani kati ya Jakaya Kikwete,Salim Ahmed Salim na Mark Mwandosya,nani alikuwa anafaa kuwa Rais?
 
Mkuu Tindo wewe ni kati ya wana Jf wakongwe, mlioshiba busara na wenye kujenga hoja!

Kinachonisikitisha mpaka hapa kukuhusu! Kwanza uzi huu hajamtaja mtu kwa majina yake!

Nasikitika kwamba, wewe unataka kuwa sababu ya kujaribu kuharibu uzi huu kwa sababu zako tu na Magufuli wako!

Kwa sababu nafahamu, badala ya watu wajikite kwenye hoja, unawafanya wajikite kumjadili Magufuli ambaye hajatajwa hapa!

Kwa heshima yako, ningependa kukuomba, mchango wako kuhusu mambo yanayoweza kuibadiru jamii yetu ni wa mhimu kuliko kukaa unamzungumzia Magufuli ambaye hawezi kutusaidia tena?

Asante

Mkuu narudia tena, hizi mada za kuchimba tunazifahamu, na nia yenu mbovu tunaianika mapema. We hutaki mabadiliko bali una nongwa na rais aliyeko madarakani. Kama unashida na jinsi makamu wa rais anavyopatikana, ungesisitiza upatikanaji wa katiba mpya, maana huko ndio kuna utaratibu mzuri wa upatikanaji wa viongozi wote, na sio makamu wa rais tu.
 
Mfumo unatufaa, ila pale panapotokea Rais Amefariki .....Nani awe Rais? Habari gan kuhusu Uchaguzi ? Na uitishwe baada ya muda gan?.

Suala hili ni muhimu sana, Kikawaida, Watu huchagua Rais, hawamchagui Makamo, Ivo Rais alochaguliwa na Watu anapofariki, ilipaswa Uchaguzi Mpya uitishwe ili tena watu wamchague Kipenzi wao .
Mkuu carlos The Jackal, hii ni hoja
 
Mkuu narudia tena, hizi mada za kuchimba tunazifahamu, na nia yenu mbovu tunaianika mapema. We hutaki mabadiliko bali una nongwa na rais aliyeko madarakani. Kama unashida na jinsi makamu wa rais anavyopatikana, ungesisitiza upatikanaji wa katiba mpya, maana huko ndio kuna utaratibu mzuri wa upatikanaji wa viongozi wote, na sio makamu wa rais tu.
Mkuu, nakubaliana kutokubaliana!

Ila ulichojadili hapa cha mhimu na umaana, ni hoja ya katiba!

Mengine haya unanilisha maneno!
 
Kila jambo linapotokea kwenye mwelekeo wa maisha ya mtu, kawaida huwa linaleta fundisho la mbele yake ya safari

Elimu ya maisha wakati mwingine huhusisha pia, misukosuko, kufiwa n .k hii yote ni katika kuyaelekea mazuri ya ndoto yetu

Kwa hapa Tanzania kulingana na yaliyotokea, bila ya shaka tunayo ya ķujifunza, kuyarekebisha na ama kuyaboresha na au kuyaacha kama yalivyo, kwani yote ni sawa iwapo yanatuacha
Imara bila shida yoyote kulingana na matukio kama hayo

Palipo na watu (wenye busara na waliojaa hekima) pakitokea jambo lolote lenye kutatanisha juu ya misingi yao kuhusu mwelekeo wao kama binadamu, huwa halipiti hivihivi bila kupitishwa kwenye mchakato wa namna ya kuliweka sawa!

Watakaa kutaka kufanyia rejea ya jambo hilo iwapo bado linapaswa liendelee kuwa vile vile kama lilivyokuwa awali ama kuwepo na mabadiriko machache kukabiliana na changamoto ya wakati huo,

Mimi nazungumizia mfumo wetu wa kumpata mgombea mwenza wa nafasi ya Uraisi

Mfumo huu ni kweli kwamba kama Taifa hatuna la kujifunza na ama kuboresha kidogo?

Natolea mfano wa matamshi ya aliyekuwa Rais wetu hayati JPM, nanukuu ningependa kusema jambo hili ambalo sikupaswa kulisema mbele yenu wana CCM, 2015 nilipoteuliwa kupeperusha bendera ya Chama kuomba kura ya Urais, jmajina niliyokuwa nimeyapendekeza kuwa wagombea wenza wa Uraisi, miongoni mwake ni jina la Hussein Mwinyi, lakini kwa kuwa WANAWAKE wana nguvu, basi Mama Samia akapita akiwa katika ukumbi wa Chimwaga pale Dodoma kwenye mkutano mkuu wa CCM kupitisha jina la mgombea Urais kule Zanzibar!

Hoja yangu iko hapo,

Mfumo huu wa anayegombea uraisi ndiye anayependekeza nani awe makamo wake wa Raisi, Kutokana na hili lililotokea na ambapo ni kwa mara ya kwanza kama Taifa kumpoteza Rais wetu katikati ya mhula wake, kama Taifa, mfumo huu bado unatufaa?

Au vetting ipite hadi kwa wagombea wenza?

Naibariki Tanzania nchi yangu njema na nzuri kuliko nchi zote Duniani

Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wetu wote wa Tanzania, uwalinde na maadui wote wa ndani na nje

Amina
Mfumo ni mbovu kabisa.

Tena katiba ndio mbaya kabisa inasema rais aliyeko madarakani akifariki leo makamu wa Rais anakuwa Rais ambapo ilitakiwa Makamu wa Rais ashikilie madaraka kwa miezi 6 then uchaguzi mkuu uitishwe .

Kwa plan hii, makamu wa Rais anaweza kula njama Rais afe mapema ili yeye achukue madaraka kiulaini.

Sijajua kwanini JPM hakufanyiwa au haukufanyika uchunguzi wa kifo chake kabla ya mazishi yake?
 
Sasa mkuu Tindo, kawaida ulitaka hoja kama hizi zisijadiliwe kabisa kwa sababu kufanya hivi ni kuonyesha chuki dhidi ya utawala uliopo?

Kwa maoni yako unataka mambo kama haya tusiyajadili hadi aliyepo atakapoondoka siyo?

Tutafika kweli?
 
Wafuasi wa Magufuli ndio wanaoongoza kudai mabadiliko ya katiba sasa hivi

Maisha kweli yanaenda kasi sana, hawa watu ndio walikuwa wakiwazodoa Chadema kuwa wananchi wanataka maendeleo sio katiba,
 
Maisha kweli yanaenda kasi sana, hawa watu ndio walikuwa wakiwazodoa Chadema kuwa wanataka katiba mpya sababu wapate madaraka
Acha majira yaseme menyewe!

Wakati ukifikaga kwenye jambo, huwa halinaga mpinzani!

Hizi zingine ni blabalaa tuu
 
Wafuasi wa Magufuli ndio wanaoongoza kudai mabadiliko ya katiba sasa hivi

Maisha kweli yanaenda kasi sana, hawa watu ndio walikuwa wakiwazodoa Chadema kuwa wananchi wanataka maendeleo sio katiba,
Wamegundua mapungufu ya katiba ndio kilikuwa chanzo cha kifo chake.
 
Wananchi wanataka maendeleo, sio katiba
Hao wananchi gani unaowazungumzia Mkuu?

Wanaoibiwa kodi zao na ma CCM

Umeisikia ile ripoti ya CAG juzi lakini?

Hayo maendeleo unayosema yatafikaje ikiwa pesa zote mnagawana tu hapo juu?

Mnaogopa mbinyo wa katiba?
 
Sasa mkuu Tindo, kawaida ulitaka hoja kama hizi zisijadiliwe kabisa kwa sababu kufanya hivi ni kuonyesha chuki dhidi ya utawala uliopo?

Kwa maoni yako unataka mambo kama haya tusiyajadili hadi aliyepo atakapoondoka siyo?

Tutafika kweli?

Kila tukijadili hoja ya katiba mpya ambayo ndio inabeba hicho kilio chako, huwa mnasema katiba haileti ugali mezani. Tatizo la msingi liko ndani ya katiba yetu ambapo rais anapewa madaraka makubwa ya uungu mtu ,wakati imedhihirika wazi kuwa hatuna viongozi waadilifu, na kibaya zaidi madaraka hayo yanatumika vibaya, mfano halisi ni wakati wa utawala wa rais aliyefia madarakani. Ww unataka kutuonyesha tatizo ni nafasi ya makamu wa rais tu, kisa huyu aliyepo haumpendi.
 
Back
Top Bottom