Mjadala bungeni ukawa na warioba, hoja rasmi ya rasimu yawekwa kando

Aug 1, 2012
35
27
Bunge maalumu lipo katika mjadala ambao kwa mujibu wa ratiba ya bunge maalum hoja iliyopo mezani ni kujadili taarifa za kamati za bunge maalumu juu ya sura ya kwanza na ya sita katika rasimu ya katiba, cha kushangaza hadi sasa mjadala unaonekana kuwekwa kando na mjadala uliopo sasa ni ukawa na warioba huku wakimtuhumu warioba kunajisi maoni ya wananchi na kuleta maoni yake, pia kuonesha kuwa warioba ni mtoa rushwa hivyo ni hasira ya kutopewa nafasi ya kugombea nafasi mwaka 1991 katika uchaguzi mkoani mara, lakini pia wakitoa shutuma kwa ukawa juu ya kuondoka kwao na kususia mjadala kwani wao ni vibaraka kwa kuvunja muungano, lakini pia sio wenye mapenzi mema na nchi.
Cha kushangaza ni hiki pamoja na wao kujadili nje na mjadala wamekuwa wakitoa hoja ya kuunga mkono hoja ya serikali mbili ambayo haiko mezani na kusema wao ni waumini wa serikali mbili pasipo utafiti wowote wa kuonesha jinsi ya kutatua kero za muungano zilizopo sasa.je kwa mjdala huu tutapata katiba mpya? Hata kama wao ccm na hao walio nao wanawewza kutoa katiba kwa kumshambulia warioba na ukawa? Mimi bado naona uhalalai wa utafiti wa warioba na tume yake lakini pia madai ya ukawa ni ya msingi kwani msingi wa viongozi lazima utokanae na kuheshimu maoni ya unaowaongoza hususani wananchi.
Ccm jifunzeni kuheshimu maoni ya watanzania huwezi tengeneza muafaka wa klitaifa kwa kuchukua maoni ya viongozi wa ccm tuu peke yao bila ya kutaka maoni ya wananchi wengi.
 
Tuanze na wewe. Kwenye tume ya Warioba ulisema unataka muungano wa aina gani? Kama hukushiriki kutoa maoni halafu unalalama ni ufinyu wa bajeti ya akili yako.
 
Tuanze na wewe. Kwenye tume ya Warioba ulisema unataka muungano wa aina gani? Kama hukushiriki kutoa maoni halafu unalalama ni ufinyu wa bajeti ya akili yako.

Tatizo lako una jazba kama mtu mwenye njaa, sasa sijui ndio style ya kujenga hoja au? Nilipendekeza serikali Tatu, tena kwa kuonesha jinsi mbili zilivyoshindwa kutatua kero na kunesha utaratibu wa tatu kutatua kero za muungano. usiwe na tabia ya kukurupuka nakulopoka tuu kisa warioba kachukua mawazo ya wengi na hapa ndio unathibitisha ufinyu wa bajeti yako ya ubongo mana umefilisika kabisa katika kufikiri sasa umeamua kuruhusu domo lilopoke ya lkutoka mdomoni bila kushirikisha ubongo
 
Hivi warioba na ukawa ni sura ya ngapi vile?

Jibu wanalo ccm na wapambe wao

Kwasasa wanajadili sura hizo za walioba na Ukawa muda wote....pale bungeni na sijui kama ndani ya rasimu kuna sura hizo.
 
Umeweka pamba masikioni utasikiaje hoja zinazochangiwa? wenzio tumezisikia hoja na utetezi wa s2 tunachokosa ni maoni ya wanaopinga hoja. katika kutoa hoja lazima uzivunje hoja za unaotofautiana nao hivyo Majina (for reference) ya uliotofautiana nao lazima yatajwe!!
 
Back
Top Bottom